Ni muda wa diamond platinumz kutembelea nyota yao

eastmea

Senior Member
Jul 28, 2018
159
133
Bila shaka najua haupingiki diamond ni msanii namba moja Africa mashariki lakini aliweza kitengenrzewa beef na msanii pendwa wa muda wote alikiba hii ikiwa katika kufaidisha media lakini ki uhalisia hawa jamaaa hawana vigezo vya kulinganishwa.katika beef hili Media zilifaidika kwa kiasi kikubwa pia msanii alikiba alifaidika zaidi tofauti na diamond ambaye beef lilikuwa halimuongezei chochote
Hivyo basi hakuna asiyefahamu msanii mkubwa Africa, diamondplatinumz ameanzisha media yake ambayo haijafikisha hata mwaka lakini inazidi kukuwa kwa kasi siku zinavyozidi kwenda hii ni kutokana na kushindanishwa na media ambayo ni kubwa Tanzania (clouds) ki ukweli katika ushindani huu clouds haimuongezei chochote hii ni kutokana na mizizi yake ambayo ameshaiweka lakini anayefaidika na huu ushindani ni diamond (wasafi TV ) hii ni kutokana na yeye yupo katika wakati wa kujitangaza zaidi kwani clouds wao tayali washajitangaza toka zamani
Hivyo basi ni muda wa diamond kutembelea nyota yao kama wao walivyomfanyia kupitia alikiba.
Katika kuandaa matamasha clouds hawajawahi kushindanishwa na tamasha lolote lakini toka wasafi festival itangazwe kumekuwa na mvutano wa mashabiki wakitaka kujuwa ataibuka kidedea siku ya tarehe 24 na kama wasafi wakiibuka kidedea watajizolea safa nyingi na upande wa pili watapokea kejeli nyingi kutoka kwa mashabiki. Pia mvutano huu najua umekuja kutokana na wasafi kusubilia fiesta imalidhike alafu wenyewe waanze kwanii anayekuwa wa mwisho kumaliza ndo huwa anatazamwa sana na kuonekana wa kwanza hajafanya lolote kwani hata ukiangalia komaa concert (Efm) ni tamasha linalojazaga sana kupitia haya matamasha lakini halipewi kipaumbele kwenye huu ushindani kutokana na wao kuwa wa kwanza kumaliza na ndo maana mnaona wasafi festival inazungumziwa sana kutokana na wao kuwa wa mwisho kumaliza ambapo awali ilikuwa inajulikana fiesta ndio tamasha la kufungia mwaka
 
Si kila linalosemwa na mange kimambi nila ukweli, mengine ni chuki tu dhidi ya diamond, kama sky ameanzisha dizzim tv atashindwa diamond, kuna vitu havi make sense, wenye kujua ukweli ni management na watu wao wa karibu na diamond
 
Back
Top Bottom