Ni muda sasa Aljazeera kuwapumzisha wana habari wao na vita Gaza wataisha

Adolph Jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
5,560
8,641
Kumekucha tena.

Ni Asubuhi nyingine naamka na kuangalia taarifa za leo weekend kupitia Aljazeera na vyombo vingine (siyo vya Tz) nakutana na mazishi ya mwana habari wa Aljazeera..

Namkumbuka pia mwanadada mwingine aliyeitwa Shireen Abu Akleh, aliyeuwawa pale Jenin ukingo wa Magharibi (West Bank) kwa kifo cha kujitakia (niwie radhi maana nitatoa sababu).

Kifo cha mwanahabari Shireen Abu Akleh.

Kilitokea karibu na kambi ya wakimbizi jenin Palestine. ambapo jeshi la Israel walikuwa na operation maalum hapo kwenye hilo eneo lililopo chini yao, sasa kulikuwa na makabiliano ya risasi baina ya jeshi la IDF na wanamgambo wa Palestine....

Huyu mwana habari katoka kwenye kikosi chake pamoja na msaidizi wake mmoja na kwenda kufuata milio ya risasi akiwa na kamera mkononi 😳😳🤔🤔,
Akafika akajibana kwenye ukuta wa jengo moja uliobomolewa kwa mabomu huku upande wa nyuma ya ule ukuta kuna risasi zinarushwa na IDF kuelekea upande aliopo na kwingineko.

Mwanahabari na uchu wake walau wa kupata kapicha ka tukio akachomoa kichwa na kamera yake mkononi tayari kuchukua picha za askali wa Israel wanaorusha risasi 🤦🤦,

Kosa kubwa risasi mbili zikazama mwilini haraka sana licha ya kuwa na kofi nyeusi iliyoandikwa (press) kwa umbali wa hatua kadhaa anaonekana na kamera akienda chini nyuma ya ule ukuta na msaidizi waliyekuwa naye akipiga kelele kuomba usaidizi (maana yeye hakuchomoa kichwa).

Kijana mmoja jasiri anatokea upande wa nyuma ya kamera iliyorekodi tukio na kwenda kumvuta Shireen kutoka eneo la tukio na kumuwahisha kwenye huduma za Afya ila alifariki wakati akiendelea na matibabu hiyo ilikuwa kabla ya vita kamili ya October 7 (Video).

Kuuwawa kwa Camera man Samer Abdu Daqqa.

Huyu katika shughuli zake za kila siku hapo gaza wakati huu wa vita alikutanishwa na milipuko ya Israel yakamjeruhi na kupelekwa hospitalini, huko huko hospitalini wakati amepata unafuu walau wa kutembea akakutanishwa na bomu lingine akamaliziwa.

Naye Wael Al-Dahdouh.

Bomu lilimkuta na familia yake likaua familia nzima mke na watoto akasalia yeye kama yeye na majeraha akiwa na mkoti umeandikwa press...

Siyo kwamba Aljazeera pekee yake inapoteza wanahabari (maana hadi hivi leo zaidi ya wanahabari 90 wameuwawa hapo gaza) ila wao wamezidia na hadi jengo lao la kurushia matangazo limebomolewa.

Wito.

Ni muda sasa wanahabari kukaa mbali na vita kwani bomu, risasi na makombola hayana akili wala uwezo wa kutambua huyu au eneo hili kuna mwandishi wa habari tusilipuke au kuuwa

Wanahabari wasihusike kwenye eneo la makabiliano ya risasi huku wakifuata miongozo ya askali na siyo kujiongoza wenyewe,

Kumbuka uhai ni zawadi tuliyopewa kibinafsi na siku ukiuacha unauacha kibinafsi, so utunze kwa gharama yeyote na siyo kisa kazi unaamua kujiweka rehani....

Done..
 
Shireen_Abu_Akleh_(4).jpg

mwanahabari Shireen Abu Akleh
 
Naye Wael Al-Dahdouh.

Bomu lilimkuta na familia yake likaua familia nzima mke na watoto akasalia yeye kama yeye na majeraha akiwa na mkoti umeandikwa press...
Huyu Nakumbuka alikuwa upande wa Hamas bila kupepesa macho. Ni kinyume na maadili ya uandidhi wa habari kuwa upande mojawapo wa vita. Alionywa mapema lakini hakusikia. Matokeo yake IDF ikamhesabu kama mmoja wa Hamas
 
Huyu Nakumbuka alikuwa upande wa Hamas bila kupepesa macho. Ni kinyume na maadili ya uandidhi wa habari kuwa upande mojawapo wa vita. Alionywa mapema lakini hakusikia. Matokeo yake IDF ikamhesabu kama mmoja wa Hamas
Kapoteza familia huyu, aisee
 
Back
Top Bottom