Vitalis Msungwite
JF-Expert Member
- May 11, 2014
- 3,269
- 7,775
Tarehe 23 wakati wa ufunguzi wa mikutano ya kisiasa pale Mwanza mheshimiwa mwenyekiti alipwaya Sana. Alionesha ni kwa namna gani anashindwa kutumikia mabwana wawili. Uso wake ulionesha anatamani uanaharakati lakini makubaliano na mama yanamkaba. Alikua anapata shida maana akisifia serikali makamanda hawamuelewi na akimkandia mama hatamuelewa hivyo akabaki kuongea pole pole na Kwa umakini mkubwa kiasi kwamba dakika Moja maneno 10 tu.
Alipowasili makamu mwenyekiti angalau alionesha mwanga Kwa chama kuwa kielekee njia ipi. Ingawa aliweka chumvi Sana kwenye hotuba yake lakini ndio maisha ya siasa. Hata mwenyekiti alibadirika kidogo hiyo siku.
Kutokana na Mbowe kuwa katikati ya pande mbili no Bora kwenye uchaguzi wa mwaka huu asigombee Tena. Hii itamfanya astaafu siasa Kwa heshima kuliko kuja kubezwa mbeleni ma makamanda. Tundu lissu ana amsha amsha na harakati za maana na convincing power ya kutosha ila Kwa mwenyekiti nafikiri hata umri umemtupa mkono apumzike.