Ni muda muafaka Afrika Mashariki kuwa taifa moja lenye Rais mmoja na Serikali moja

Hakuna tija yoyote vinchi maskini vilivyojaa migogoro ya kisiasa vikiungana.

Kwanza haiwezekani kufikia hatua hiyo ya serikali moja, maana vyeo vitapungua, na kwenye vinchi ushubwada kama hivi vyeo ndiyo kipaumbele namba 1.
Hakika mkuu ,uroho wa madaraka ,wizi ,umimi haiwezekani kabisa
 
Huwa nawazaga hivi kwa viongozi mliopo madarakani hakuna anaewaza kuitawala Afrika Mashariki yote na kulifanya likawa taifa moja?

Kwa sasa naiona hiyo ni fursa kwa viongozi wa Tanzania kujitafakari na kuchanga karata ili muweze pata fursa ya kufikia lengo hili, ila kama mtaendelea kuwaza kujenga madarasa, na kuunga juhudi za vyama, niwaambie tu kuna siku upepo utabadilika itatokea taifa mojawapo hapa Afrika Mashariki litajikuza kiuchumi, kiteknolojia, nk, na kuanza kuchukua mamlaka kinguvu ndani ya mataifa mengine, na tutapofikia huko tambueni kwamba mtakuwa mmechelewa.

Mimi naamini kuna viongozi kati yenu ndani ya Afrika Mashariki wanawaza kuzitawala nchi nyingine, na nchi mmoja wapo ni Rwanda huyu jamaa wa Rwanda endapo angepata na atapata nyezo na nafasi thabiti mtajikuta mnatawaliwa na kuunganishwa na kuwa nchi moja, na hili haliwezi fikika kirahisi, kama hutotumia akili na mahesabu makali kulitimiza.

nb: Viongozi wa Tanzania ni muda wenu sasa kujipanga ili hiyi nafasi ibaki kwenu.
Kama Tanzania imeshindwa kuwa Na Rais Mmoja na Serikali Moja..
Unafikir East Africa itaweza
 
Bila mkutano wa Berlin kuigawa Africa, leo hii Africa tungekuwa na vita visivyoisha, na jaribio lolote kuibadili mipaka ya Berlin au ya wakati wa Uhuru ni kuchochea vita Africa.

Licha ya kufanana rangi na wote wabantu lakini sisi waafrica tunatofauti sana za kitamadani, only in Tanzania ndio tuna jamii moja isiyo na ukabila (sababu ya Kiswahili na Siri anayoijua Nyerere) nje ya Tanzania mataifa yote yana ubaguzi wa kikabila, kiukoo au kidini na muda wote wako tayari kupigana vita.

Mreta mada utakuwa huijui Somalia, Somali imevunjia kwa sababu za kiukoo tu, sasa imagine watakubali vipi kutawaliwa na watu wachoyo kama Wakenya ambao nao pia wana Ukabila, achia hapo kuna Rwanda na Burundi, Congo, huko Sudan kuna watu hawajui nani ni Rais.

kabla hatujawaza mambo mazito kama hayo kila mtu afix ya ndani kwake
 
nb: Viongozi wa Tanzania ni muda wenu sasa kujipanga ili hiyi nafasi ibaki kwenu.
Acha mzaha bro. Hawa hawa walio madarakani kwa wizi wa kura wataweza kutoboa huko? Wakenya, Wasomali... siyo wapole kama Watanzania, kutazuka vita ya kudumu
 
Mleta mada hapo mtaani kwenu tafuta watoto wadogo kabisa unaona hawana hatia Kati ya 5 hadi 10, wape sinia LA wali na waambie wale kwa Amani na utulivu, wakiweza kuwa wastaarabu basi aina ya muungano kama wa EAC ni rahisi, wasipoweza ujue Bado binadamu hasa waafrika tunahotaji kustaarabika sana
 
Huwa nawazaga hivi kwa viongozi mliopo madarakani hakuna anaewaza kuitawala Afrika Mashariki yote na kulifanya likawa taifa moja?

Kwa sasa naiona hiyo ni fursa kwa viongozi wa Tanzania kujitafakari na kuchanga karata ili muweze pata fursa ya kufikia lengo hili, ila kama mtaendelea kuwaza kujenga madarasa, na kuunga juhudi za vyama, niwaambie tu kuna siku upepo utabadilika itatokea taifa mojawapo hapa Afrika Mashariki litajikuza kiuchumi, kiteknolojia, nk, na kuanza kuchukua mamlaka kinguvu ndani ya mataifa mengine, na tutapofikia huko tambueni kwamba mtakuwa mmechelewa.

Mimi naamini kuna viongozi kati yenu ndani ya Afrika Mashariki wanawaza kuzitawala nchi nyingine, na nchi mmoja wapo ni Rwanda huyu jamaa wa Rwanda endapo angepata na atapata nyezo na nafasi thabiti mtajikuta mnatawaliwa na kuunganishwa na kuwa nchi moja, na hili haliwezi fikika kirahisi, kama hutotumia akili na mahesabu makali kulitimiza.

nb: Viongozi wa Tanzania ni muda wenu sasa kujipanga ili hiyi nafasi ibaki kwenu.
Wazo baya kuwahi kutokea.
Mataifa mengi Afrika Mashariki ni njaa kali kiasi wanakimbilia Tanzania kusaka doo.
Pia mataifa mengi ya Afrika mashariki hayajastaarabika.
Hiyo Rwanda usiihesabie kuwa na nguvu maana mipaka yake tu inamshinda sembuse aje kuuweka chini ukanda mzima??
 
Back
Top Bottom