Ni manufaa gani yanayoletwa na big brother?

jobseeker

Member
Feb 25, 2012
70
7
Bara la Afrika lina janga kubwa linalolitesa kwa miaka mingi mno nalo ni la ugonjwa wa ukimwi.
sina haja kabisa ya kusema ni chanzo kipi kinachochangia kuenea kwa gonjwa hili baya kwani
kila muafrika sio tu anajua bali kwa njia moja au nyengine ameguswa na gonjwa hili.

Kinachonitatiza mimi ni kuwepo na hii big brother africa ( ambayo jumba lenyewe liko south africa ambako
gonjwa la ukimwi limekithiri) na kila kukicha kinachoonyeshwa kwenye site mbali mbali ni wanawake waliomo
katika hilo jumba wakiwa uchi wa mnyama na pia watu waki sex. Yaani imefika mwaka huu kuna fee maalum
ili uweze kuona parts ambazo hazikurushwa hewani, parts hizo zaidi ni wakati wakikoga na wakiingiliana.

Suali langu ni kuwa hivi kweli watayarishaji wa kipindi hiki wanajua ni kiasi gani wanachangia kuhamasisha casual sex?
Hivi program hii ina manufaa na elimu yeyote kwa jamii yetu? Kweli waafrika tunaiga mengi kutoka nje ya bara letu lakini
hili kweli ni lazima?
 
  • Thanks
Reactions: mij
bora ya wewe umelitambua japo tatizo lakini wengi wetu bado wanashabikia hii kitu na kukenulia meno (kuchekea) kana kwamba ni somo la kilimo cha kufa na kupona. Wazungu wanafurahia haya mambo kwa maana wenyewe hawawazi sana juu ya nile nini au nivae nini wakati hapa kwetu tunaona hakuna lingine la kujifunza zaidi ya hayo. Tuna matatizo mengi sana lakini ukombozi wa kifikra ni muhimu zaidi
 
Itabidi tumuulize prezzo amepata elimu gani kutokana na hiyo program ya BBA.
 
Last edited by a moderator:
Bara la Afrika lina janga kubwa linalolitesa kwa miaka mingi mno nalo ni la ugonjwa wa ukimwi. sina haja kabisa ya kusema ni chanzo kipi kinachochangia kuenea kwa gonjwa hili baya kwani kila muafrika sio tu anajua bali kwa njia moja au nyengine ameguswa na gonjwa hili. Kinachonitatiza mimi ni kuwepo na hii big brother africa ( ambayo jumba lenyewe liko south africa ambako gonjwa la ukimwi limekithiri) na kila kukicha kinachoonyeshwa kwenye site mbali mbali ni wanawake waliomo katika hilo jumba wakiwa uchi wa mnyama na pia watu waki sex. Yaani imefika mwaka huu kuna fee maalum ili uweze kuona parts ambazo hazikurushwa hewani, parts hizo zaidi ni wakati wakikoga na wakiingiliana. Suali langu ni kuwa hivi kweli watayarishaji wa kipindi hiki wanajua ni kiasi gani wanachangia kuhamasisha casual sex? Hivi program hii ina manufaa na elimu yeyote kwa jamii yetu? Kweli waafrika tunaiga mengi kutoka nje ya bara letu lakini hili kweli ni lazima?
siku zote huwa naona ni upuuzi kupoteza muda wangu kuangalia Big brother, kwanza wengi wa washiriki huwa wanaigiza hawaishi maisha yao halisi.
 
faida ya big brother ni vijana wetu WAJINGA-WAJINGA kuiga na kujifunza tabia CHAFU, huku wenye show wakimeki bingo.
 
Faida ipo kwa wanaoshiriki BBA kwani watalipwa pesa nyingi sana endapo watashinda,kwa watazamaji wanafaidika kama entertainment,...hujalazimishwa kuangalia na tena kuangalia kwenyewe kuna garama,it's better ukatune tv channels zingine ambazo zinarusha programme mambo unayoyataka..unapoangalia football,mieleka,basketball kwani we mtazamaji unapata faida gani?
 
Kiukweli kwa mtazamo wangu chanya hii haina elimu yoyote kwa jamii zaidi ya kuhamasisha zinaa kwa jamii ya kiafrika ambayo ina matatizo lukuki na hivyo kufanya matatizo yaongezeke cku hadi cku.kweli 2mekuwa wapuuzi kiasi kwamba 2najichinja wenyewe kwa tamaa ya kupata utajiri wa haramu na hii inatokana na kuyaacha maadili ya dini ze2 na ya kiafrika na tatizo kubwa sasa ni utandawazi ambao 2naona ni ukombozi kwa mtazamo chanya lkn ni janga kwa mtazamo wangu
 
Back
Top Bottom