Ni Lini haki itaonekana kutendeka hasa katika uchaguzi mkuu

Mussa Mussa

Senior Member
Jan 10, 2012
138
42
Ndugu zangu mimi bado naendelea kujiuliza kama kuna siku tutakuja kuwa na uchaguzi ambao utakuwa wa uhuru na haki ikaonekana kutendeka. Ninaposema haki ionekane kutendeka ninamaana mshindi anayetangazwa na tume ya uchaguzi basi awe ndiyo chaguo la watu ki ukweli na si kuchakachuliwa. Utakumbuka mheshimiwa Rais (sipendi kumuita Dr. kwa kuwa alipewa mezani) alimtangaza mwenyekiti mpya wa NEC mapema mwezi huu Mh.Jaji mstaafu Damian Lubuva na kwa hali isiyokuwa ya kawaida mwenyewe alikiri wazi kuwa hatoleta mabadiliko yeyote kwenye taasisi hii. Hii ni wazi kwamba kwa yeyote anayefikiri vizuri mshindi wa uchaguzi wa mwaka 2015 amekwisha patikana yaani ni Mgombea wa CCM kwa sifa zozote atakazo kuwa nazo ziwe zinakubalika au hazikubaliki. Kungekuwa na uhuru wa kweli katika chaguzi hizi basi kauli ya Lubuva ilikuwa ni sababu tosha ya kustaafu kazi aliyopewa hata kama hajaitumikia hata kwa masaa 3 toka anapewa wadhifa huo mpaka kutoa kauli hiyo. Mabadiliko yataletwa na wewe uliyfanikiwa kuisoma habari hii ukichanganya na zako. Nakutakia kila la heri katika ujenzi wa taifa. The hard way the only way. Please your comment is my success. All the best.
 
Elimu ndiyo itakayowakomboa Watanzania...bila ya mtu kujishughuisha kutaka kujua sehemu zingine wanafanyaje kuhusiana na wagombea waliopo, basi atamchagua yule aliempa chumvi na Tshirt!.
Elimu pekee ndiyo suluhisho..chanfia hili kwa kumsomesha mtoto wako au wa nduguyo!
 
Back
Top Bottom