Ni Laana kwa Afrika kufuta vibali vya Uchawi na Uganga Tanzania

Nakubaliana na yerico mimi ni kati ya watu wanaoamini uwepo wa uchaw na nguvu zake na binafs unanisaidia kwa wakat flani flani ila tatizo ni kuwa kwa kawaida wachaw hutumia majin sasa wakat flan mwanadamu akiwa na shida flan majin yanataka kitu flan yamsaidie sasa hapo ndio tatizo mwanadamu akiambiwa kiungo cha albino lazima apeleke. Kwa kifup hakuna namna ambayo majini au mizimu inaweza kukusaidia bure ni lazima ulipe kitu flan sasa kwenye malipo ndio inategemea utaambiwa nini na wakat flan yana kulazimisha kuwa yakishakutajia yanachotaka lazima ulete sasa kwa hal hiyo albino hawawez kupona ila pia mganga wa kweli hawez kuzuiliwa na serikal maana ana nguvu kuliko serikali

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Leo nimeelewa watu wengi sana humu Jf wana upeo mdogo sana wa kufikiri wapo waganga wa ukweli wanaosaidia jamii kwa kiasi kikubwa kama hao wanaotumiwa na ccm kupata vyeo na wanafikiwa na wapo waganga feki serikali inatakiwa kufanya utafiti kugundua waganga wenye faida kwa jamii waachwe na hao waganga feki ndo wanatakiwa kufutiwa vibali.
Shida ni kwamba hata mganga akiwa wa kweli vip hawez kuendana na mfumo wa maisha wa sasa na naomba nitoe mfano kidogo tu...kuna ndugu yangu aliwah kuwa na kesi ya mauaji akakaa sero mwaka na nusu sisi tukatafuta mganga akadai tumpe ngombe tulivyompa akatuma jin likaleta faili la kesi nyumbani tukalichoma moto baada ya mada akaachiwa maana hakuna faili.. Sasa lengo la kutoa huo mfano ni kwamba ukiruhusu sana uchaw hata serikal haiwez kufanya mambo yake sawasawa zaidi mfumo wa serikali utaingiliwa tu

ndo maana nimesema wapo waganga wa kienyeji wenye msaada mkubwa kwa jamii na wapo matapeli wale matapeli ndo wanatakiwa kufutiwa vibali .
 
Wewe Yericko Una Laana Kubwa Sana imo ndani yako Kamwe Huwezi Kuijua,maana Laana Hiyo Imekomaa Sana,bila Hata Aibu Kijana Mzima Unashabikia Uchawi? Hivi Unajua Kuwa Uchawi Ni Shetani Na Shetani Hana Huruma? Unadiriki Kusema Eti Dini Zimeletwa Na Wazungu Na Waarabu,wewe Humjui Mungu Na Wala Huna Hofu Ya Mungu,hakuna Mwanadamu Aliyeleta Dini,dini Zimeletwa Na Mungu Mwenyewe Kupitia Manabii Wake Kama Kina Musa,Elia,Yakobo,NA n.k,unaishabikia ccm Kuzunguka Na Wachawi Hujui Kuwa Viongozi Wote Wa ccm Pamoja Na Wafuasi Wao Wamelaaniwa? Kama Huamini Ipo Siku Utaamini,utakuja Kuona Kitakachowapata Mungu Huwa Hana Haraka Maana Si Mwanadamu,miaka Elfu Moja Kwa Mungu Ni Sawa Na Dk Moja,kwa Hiyo Wewe Ni Mjinga Ambaye Hujaishi Hata Sekunde,kwa Ujinga Ulionao Unawaita Watu Wasiokubaliana Na Ujinga Wako Kuwa Wana IQ Ndogo,upo Sawa Kabisa,wana IQ Ndogo Ya Kumjua Shetani ila wana IQ Kubwa Ya Kumjua Mungu,kaa Chini Ujitathimini Au Lah Maisha Yako Duniani Yatakuwa Mafupi Sana,wewe Ni Chukizo Mbele Za Mungu.

Mungu alileta Dini ? :beer:
 
ndo maana nimesema wapo waganga wa kienyeji wenye msaada mkubwa kwa jamii na wapo matapeli wale matapeli ndo wanatakiwa kufutiwa vibali .
Msaasa upi sasa..Wabongo akili zenu za nyumbu....Mganga kaleta file likachomwa ili muuaji apone.Ila si kuwajibika kwa kosa alilofanya,na kuwa mfano wengine wasiuawe?Shetani siku zote ndivyo alivyo...na waendekeza uchawi jamii yao yote hulaanika na kuwa masikini.Akina Zitto,JK, Sitta,Mudhihi na wengine wa maeneo maarufu kwa uchawi na yaliyouza wengine km wanyama wangesema ukweli .Life style yao na kukumbatia uchawi ndipo kulikowafanya masikini na si ubaguzi .Shetani anatafuta sababu nyingine za kurudi ktk maisha ya kawaida ya watz na kupewa uhalali zaidi.
 
Hata kama unautukuza uAfrika lazima ujue hawa watu wameshindwa kutumia huo uchawi wao vizuri, nikweli huu ulikuwa ni miongoni mwa utamaduni wetu lakini ujue katika kipindi kile uchawi ulitumika kwa baadhi ya makabira katika kupambana na mkoloni, kulinda ngome n.k lakini si kuuana kikatili kama ilivyo sasa.

Uchawi na ushirikina umekuwa ni tatizo kwa sasa, maana mtu anaye amini ushirikina hashindwi kumuua hata mama yake mzazi, pia waganga wenyewe waongo watupu, tena wana toa masharti ya ki hila hila ili kazi ionekane ngumu, hakuna mganga dunia hii ni matapeli kama matapeli wengine ndio maana serikali ikaliona hili la kuwafutia vibali. jiulize kuna mtu anaweza kukupa dawa zifuatazo:
  • kufaulu mtihani
  • kupata hela wakati yeye hana anategemea mteja ndio umpe.
  • kumtuliza mpenzi wakati yeye ndoa aliyonayo niya 7 na inaning'inia.
  • kukupa cheo wakati hata darasa la saba hukumaliza.
  • n.k
Kwa hili jiongeze kaka.

Mambo mengine hayafai hata kuchangia, mtu anayeshabikia uganga wa kienyeji na uchawi katika karne hii ni wakumuepuka, kuna mambo mengi yaliyofanywa na mababu zetu ambayo ukitafakari unajiuliza walikuwa wanafiki nini, Kwa msimamo wa huyo jamaa waganga wa kienyeji wakielekeza Albino wauawe tuunge mkono, mabinti wakikeketwa tuunge mkono. Amesahau moja kwamba mababu zetu walitembea nusu uchi na sisi turudie huko kwa sababu huo ndiyo Uafrika wetu. Kwa sababu ya matendo ya kichawi, kishirikina na uganga wa kienyeji watu kutoka mabara mengine bara la Afrika huliita bara la giza, huyu jamaa alipashwa kuzaliwa katika karne ya tatu au nne.
 
Sikutegemea kama unaweza kuwa huru na mwenye uelewa mpana kiasi hiki.
Umeandika ukweli lakini ni ukweli mchungu usiomezeka kwa wenye uelewa mdogo na walioleweshwa uongo wa mapokeo.

Binafsi nilipokuwa mdogo niliamini sana katika vitabu vitakatifu na uwepo wa Mungu.Lakini nilipogundua kuwa Mungu hayupo na hana msaada wowote kwa binadamu na wengi wanaojiita watumishi wake wamejaa ujanjauanja na watumiaji wakubwa wa ushirikina na uchawi ili kuvuta wateja kiasi cha wao kwa wao kugombana,kutukanana na kukashifiana niliamua kutoka ndani ya ufungwa huo na kubaki huru.

Watu wanakupinga kwa kutumia vigezo vya dini ambazo kimsingi licha ya kutumika kututoa kwenye msitari na kutuharibia uafrika wetu bado zimetumika kutunyonya, kututia umasikini,kuuwa watu wasio na hatia,kubaka na kulawiti watoto. Ushoga leo ni halali,Watu wanavalishwa mabomu na wanajilipua ili waende akhera.

Wewe hujasupport mauaji ya albino katika post yako ila unaiomba serikali ifikirie kwa kina kutafuta best solution kwa sababu swala hili ni complex na lina mizizi yake iliyojificha katika jamii. Serikali kufuta vibali vya waganga wa jadi wakati yenyewe,viongozi wake,viongozi wa dini na jamii hawawezikuacha kuwatumia waganga hawa kufanikisha mambo yao ni uanafiki. Hivyo suluhisho ni kutafuta namna ambayo inaweza kuwasaidia waganga na wachawi kuacha kutumia viungo vya albino kama wanavyofanya sasa na kutafuta mbadala wake. Inawezekana.

Mimi huwa sio mchangiaji sana ila kwa jinsi mada yako ilivyonigusa nimewiwa kuchangia ila ni msomaji na mfatiliaji mzuri.

:wave::wave::wave:

Thanx.
 
Naamini katika uafrika wangu, naamini katika tamaduni zangu, najivunia kuwa muafrika. Ninachukia ubeberu na ukoloni mamboleo.

Nasikitika kuwa sisi wapinzani wa ubepari huwa hatueleweki kwa jamii. Kwa kuwa wanaotuzunguka wamefunikwa na kudumazwa kabisa na ubepari na ubeberu.Wanatamani kuwaza kwa pamoja, kitu kimoja kwa wakati mmoja.

Kwaujumla wanawaza kwa fomula ambazo ni standard zilizowekwa na kikundi fulani na kuwaaminisha ni sahihi. Kikundi hicho chenye mawazo dharimu ni wapinzani wakubwa wa Uafrika na mambo ya Afrika. Wameuaminisha mambo mengi ulimwengu uyaone ni bora, ya usasa na cilivilazation. Wakitizama mila zetu na kuziita za kishenzi.

Mimi ni huamini katika mrengo wa kushoto. Uchawi na Uganga ndio uafrika wetu.

Huwezi kufutilia mbali vibali waganga wa kienyeji ama wachawi kwa kigezo cha mauaji ya Albino, uganga ama uchawi ndio uafrika wenyewe. Hata Ulaya kuna wachawi na waganga wao wa kienyeji na ndio uzungu wao.

Wachawi ndio wanaolinda taifa lolote lile duniani, Wachawi ndio walioleta uhuru Tanganyika na Zanzibar, Wachawi ndio wanaolinda Ikulu ya Marekani. Uchawi hutumika vitani, Uchawi hutumika kwenye siasa, na wale wakumbukao vita vya Uganda nikuwa Uchawi ulisaidia sana, ilifika hatua wachawi wetu walifeli, hasa brigedi ya ujenzi wa daraja la mto kagera, ndipo tulipokwenda kukodi wachawi Msumbiji, walipofika tu daraja lilijengwa kw masaa 12 tu huku maadui waliokuwa ng'ambo ya mto uli wakipigwa usingizi wa pono, na walipozinduka walikuta majeshi yetu yashavuka daraja.

Mfano mwingine mzuri ni Chama cha Mapinduzi uchaguzi 2010 ilikusanya wachawi 200 nchi nzima wakazunguka na mgombea wao huku wakiloga kila walipokanyaga ili watu wamchague mgombea wa ccm. Sasa kama ccm iliweza kuwakodi na wakafanikiwa wanashindwaje leo kuwaita wachawi wote ili wawaombe wabadili masharti ya dawa hiyo isitumie viongo vya albino?

Najua uchawi upo na unafanya kazi, nzuri na mbaya pia. Belief in witchcraft is almost universal, and it has its essence in the development of man and knowledge.

Naomba watu tusome tena kazi za kitaaluma za Prof. Ray Abraham wa Cambridge University kuhusu witchcraft in Nyamwezi and Sukumaland; mwingine ni Prof. Sufiani Bukurura aliyewahi kufundisha sheria Chuo Kikuu cha Mzumbe, pia Prof. Simon Mesaki wa UDSM sociology department... Tusome pia kitabu kimoja cha Prof John, (sikumbuki ubini), Witchcraft in Europe...

Watu hawa wamefanya utafiti wa kina sana kuhusiana na masuala ya uchawi na uganga wa kienyeji, na perspectives zake, mbaya na nzuri. Ukienda Boston Massachusetts na hasa Salem, nenda kwenye museum utaona stories za uchawi, mauaji ya vikongwe, vilema na hata albino. Huku kwetu, leo, na hata kale, hili la mauaji ya albino ni baya na ovu, lakini essence yake ina kina kirefu sana katika mythology ya makabila husika.

Hupigi tu marufuku uganga wa kienyeji kwa vitisho vya mamlaka na sheria, kwa sababu hii, hutasaidia chochote...

Utaua hata elimu nyingine ambayo ni adhimu kwa maisha ya binadamu. Mfano, watu hatujafanya research ya kutosha kuhusu contribution ya African medicine katika pharmacology ya Africa. Sasa hivi, dawa nyingi za kiafrica zimepotea na hatutazipata tena. Wachina wao wanatafiti traditional medicines zao, sisi dawa zetu tunazipiga vita tena bila kuwa na maarifa. Ni ma fallacies tupu ya generalization.

Kwaujumla uchawi ndio dini zetu za kweli kuliko hizi dini za ukristu na uislamu tulizoletewa kwenye majahazi ambazo leo hata hao wazungu hawaziabudu.

Serikali yetu ishughulikie kwa kina suala la mauaji ya albino, sio kupiga tu marufuku uganga wa kienyeji... Suala hili ni complex kuliko linavyoonekana

Njia bora nikuwaambia wachawi wabadili teknolojia ya hii dawa inayohitaji albino, wabaki na dawa, majini na madubwana yanayohitaji damu za wanadamu wote tu.

mmmmmh, nitashangaa kama bado hujakamatwa
 
Asante sana mkuu kwa tariff hii
 
Nasikia uinggereza wao wana ajira maalumu kwa mchawi na wachawi hufanya interviiew na aliye mchawi zaidi hupewa kazi katika moja ya bustani zinazotunza mambo ya uchawi. Basi ili tusifute hivi vibali tuwe na ajira ya mchawi na mganga mkuu wa jadi. Hawa watasaidia kujua wachawi na waganga feki na watapendekeza katua kali za kuwachukulia. Watawezesha kubaini ni yupi anatumia viuongo vya albino na anakamatwa. Hii itamaliza tatizo
 
Wachawi na waganga wote inatakiwa wauwawe hata maandiko yamesema maana wao ndio chanzo cha maovu yote kwenye Jamii. Mwizi kibaka jambazi aibi bila msaada wa mganga, waganga ndio utoa limbwata kwa makahaba kupora waume za watu Ili familia ziteseke, wamiliki wa mabus usababisha ajali kwa maagizo ya waganga Ili watoe kafara kwa mashetani, wachawi urudishwa nyuma na kuleta mikwazo ya maendeleo kwenye Jamii kwa kuwajengea hofu.Ndio wameharibu akili za watu kuamini ndumba badala ya akili zao.
Waganga wanafarakanisha familia, wanaua walemavu,nk
Kwa ujumla hili kundi halina umuhimu kabisa kwenye Jamii.
Ulaya waliwaua wachawi na waganga wote wakapata kizazi kipya chenye fikra za maendeleo.
 
Back
Top Bottom