Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,214
- 42,087
Ukweli ni kwamba kuna matukio Rais wetu amekuwa akiingizwa mkenge ni pengine kwa makusudi au kwa bahati mbaya hasa na wasaidizi wake!
Mh Rais alipoingia madarakani alichagua wasaidizi kutoka kada mbali mbali kuanzia uchumi, siasa, diplomasia na kila kona!
Lakini pamoja na wasaidizi hao bado inaonekana ni watu wasio msaidia kabisa zaidi ya kumhujumu!
Kwanza walianza kwenye uteuzi wa boss wa TPDC wakachomeka mtu asiye na sifa baadae baada ya kelele Madam president akagutuka na kurekebisha. Swali: hawa wasaidizi walikuwa wapi kuzuia hili? Rais alikataa ushauri? Hashauriki na yeye?
Pili, hawa wasaidizi walijua kabisa Madam president anakwenda kufanya mahojiano na BBC chombo kinacho angaliwa dunia nzima. Kweli walishindwa kumuandalia kabisa possible questions na majibu?
Kama swala la Mbowe ilikuwa inajulikana wazi litaulizwa sasa mpaka Rais anatoa majibu kuwa wenzie Mbowe walishakiri makosa wakahukumiwa nani alimwambia? Ina maana wasaidizi wa Rais wote walikuwa hawajui kuwa case haijaanza kusikilizwa? Pengine Rais alifanya kusudi au hakutaka kusikiliza ushauri wao kwenye swala hilo?
Tatu, Madam president alikwenda kushiriki kwenye sherehe ya utiaji saini wa mkataba wa utengenezaji meli ambao baadae alikuja kugundua ni wa kifisadi na kipigaji bado maswali yanakuja hivi hawa wasaidizi wake wana msaada gani? Kwanini wana muingiza Rais kwenye mikenge? Kwanini Rais hakusaidiwa kufatilia hilo hadi anapiga makofi kwenye kusaini na baadae ndio ana stuka?
Nne jana kwenye hotuba ya miaka 60 ya uhuru watu walitarajia Mh Rais kugusia mambo muhimu ya kijamii na kiuchumi hasa mfumuko wa bei ya vitu na bidhaa mbalimbali na kutoa majibu na matumaini kwa watanzania lakini bahati mbaya ni kuwa waandaji hotuba wameona ni bora kumuhujumu tu kwa kuweka mambo ambayo siyo ya msingi kabisa na ambayo yalitakiwa kuzungumzwa siku ya uhuru maana ilikuwa historia. Hivi wasaidizi wa Rais kwenye uchumi, diplomasia, siasa na kijamii hawakuwa na la kuandika zaidi ya yale? Kweli kwanini tusiamini kuna watu wana mhujumu Rais baada ya kujua ni mpole?
Kwenye hotuba ya jana kuna makosa mengi hadi watu wanajiuliza ni nani aliyeandika hotuba ya jana na kumpa Rais?
Kiukweli ni wazi Rais wetu amekuwa mzito kufatilia baadhi ya mambo mengi hasa ya msingi hivyo wengi wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kufanya yao na kumchomekea.
Bado najiuliza hawa wasaidizi wa Rais ni wanini? Wana kazi gani za msingi?