Ni kweli kuwa Katiba Mpya ndio kila kitu?

Path Finder

Member
Jan 28, 2011
50
8
Karibu kila jambo linalotokea tunakimbilia kusema suluhu ni katiba mpya! Je ni kweli kwamba katiba mpya pekee inaweza kutukomboa na matatizo tuliyo nayo wa TZ?
 
Labda cha kujiuliza je ni kero gani zinazowafanya wananchi waTanzania kuona kuwa katiba mpya na endelevu ndio suluhisho la matatizo tuliyonayo? Binasfsi kero kuu ni kama zifuatazo (1) kushindwa kwa uongozi kuheshimu, kulinda na kuendeleza haki za binaadamu kutokana na sababu nyingi lakini kubwa ni maamuzi mabaya na yanayojali maslahi binafsi kuliko maslahi umma/taifa; dola kutumia malaka waliyopewa na wananchi kwa manufaa ya viongozi wa dola na jamii zao; rushwa iliyokithiri; ubadhirifu wa mali ya umma; viongozi kuwajibika kwa vyama vyao vya siasa, rafiki na jamii zao badala ya kuwajibika kuheshimu, kulinda na kuendeleza haki za binaadamu wote; umaskini uliokithiri kwa watanzania waliowengi; upendeleo wa wazi katika kugawa fursa ikijumlsiah mapato ya serikali, ajira, biashara/tenda na mengineyo; watumishi wa umma na wanasiasa kutokuwajibishwa kwa utendaji mbaya (2) kushindwa kwa wananchi kudai uwajibikaji kutoka kwa viongozi kwasababu nyingi ikijumlisha uwoga wa kushughulikiwa na viongozi wenye mamlaka makubwa yasiyo na mpaka; kutokujua haki zao na kwamba wao ndiyo waliowapa viongozi mamlaka; kukata tamaa kutokana na uwoga na matashio toka kwa viongozi na jamii zao. Kimsingi hizi sababu zote zinatokana na katiba mbovu tuliyonayo. Katiba mpya inatakiwa itatuwie haya matatizo niliyataja. Mfabno rushwa itatatuliwa kama katiba mpya itaweka mfumo mzuri wa taasisi za kuzuia rushwa kwa kuzifanya ziwe huru na zisiwajibile kwa Rais. Uetuzi wa Mkuu wa Taasisi hiyo usiwe mikononi mwa Rais. Pia mtendaji yeyote wa serikali au kisiasa alazimishwe kusimama pembeni pale anapohusishwa na rushwa na wakati uchunguzi unafanyika. Pili mtumishi yeyote wa umma na kisiasa akipataikana na rushwa anakosa sifa ya kushika nyadhifa yeyote hadi baada ya miaka 10 na kama kuna ushahidi amejirekebisha. Katiba mpya iweke taratibu ya kuchunguza viongozi wote wanaoteuliwa na pia katiba mpya ipunguze mamlaka ya rais ya kuteuwa viongozi wakuu wa serikali. Tukifanya hili tutapunguza uwezekanao wa kupata viongozi wabovu na wasio na maadili. Pili watumishi wa umma wengi wataogopoa na kujali maadili. Pia katiba mpya iweke mipaka kwa macontractor na wafanyabiashara wenye kutuhimiwa na kupataikana na makosa ya rushwa ili Wakihusishwa wakati wa uchunguzi wasipewe tenda na kampuni zao zisimamishwe wakipatikana na hatia wazuiwe kufanya biashara na serikali mpaka baada ya miaka 5 na pale tuu wakithibitishwa kujirekebisha. Katiba mpya ilinde haki ya wananchi kudai uwajibikaji wa utumishi bora toka kwa serikali na viongozi wa siasa na mwananchi yeyote awe na haki kupata suluhu pale haki inapovunjwa kwa mujibu wa sheria. Ubaguzi wa ain yeyote na upendeleo katika ajira, tenda na kadhalika ukomeshwe na vipengele ndani ya katiba ambapo mwananchi anweza kwenda mahakami kudai haki. Tume ya Haki za binaadamu ipew meno na uhuru kuchunguza ukiukwaji wa haki za binaadamu ikijumlsiha mauaji yanayofanywa na polisi. Rais asiteue mawaziri kutoka miongoni mwa wabunge kwani inaingilia utendaji wa wao katioka kuiwajibisha serikali. Haya yakitokea matatizo ya mawaziri kutokuwajibika yatapungua. Pia Rais ataliheshimu bunge maana hatakuwa na wafadhilina. Haki ya kupata taarifa kuhusu maamuzi ya serikali na matumizi ya fedha za umma ikikaziwa katika katiba mpya malipo na matumizi hewa yatajulikana na wahusika watuchukuliwa hatua kiurahisi. Sasa hivi mwananchi hawezi kudai taarifa za maamuzi ambayo yameidumbukiza nchi katika madeni makubwa. Kama tungekuwa na haki ya kupata taarifa kabala maamuzi hayajafanywa labda tungeweza kuiepusha nchi na dowans. Pia pale serikali inaposhindwa kuheshimu haki ya mwananchi kupata taarifa, katiba mpya impe mwananchi mamalka ya kuipeleka serikali mahakamani/ Ili mahakama itoe haki ni vyema katiba mpya iondoe mamlaka ya kuteuwa majaji na mwanansheria mikononi mwa Rais. Hii itawafanya wawe huru na kutokumuogopa Rais kwani hatakuwa ndiye pekee aliyewateua.Katiba mpya izuie uwezo wa waziri, wizara ama bodi za vyombo vya umma kujipangia mishahara ya watendaji wakuu ambapo wengi wametumia mianya hiyo kuwapangia mishahara mikubwa ndugu na marafiki zao ambao ni watendaji wa umma. . Mishahara hii mikubwa isiyolingana na utendaji ni uwizi wa wazi wa matumizi ya fedha za umma. Uteuzi wa wajumbe wa bodi za umma pia unahitaji kuangaliwa upya katika katiba mpya. Bodi za marafiki ama jamaa zinashia kufanya maamuzi mabovu kama yale yaliyohusisha uuzaji wa nyumba za umma na mabodi mabali mbali. Wananchi wakipewa fursa ya kupitisha majina ya viongozi wa taasisi za umma, mabodi etc watapunguza sana watu wasiofaa kupewa majukumuBinafsi ninaimani kuwa Katiba mpya ikiwa endelevu itatatua mengi ya matatizo yetu. Ila ni ukweli usiopingika kuwa na katiba mpya ni hatua ya kwanza ya pili ambayo nimuhimu sana ni kuhakikisha inatekelezwa. Ni muamko na hamasa ya kudai utekelezwaji wa katiba mpya miongoni mwa wananchi ndiyo utakaoleta mabadiliko Tanzania. Soma makala nyingine kujua zaidi tofauti kati ya katiba dumavu na ile endelevu. Hivi vigezo ni muhimu kutisaidia katika mjadala wa Katiba Gani tunayoitaka Tanzania
 
Back
Top Bottom