Carlos Valderrama
JF-Expert Member
- Dec 27, 2014
- 664
- 240
- Thread starter
- #21
Huu ndiyo ukweli ambao wafuasi wa Chadema hawataki kuukubali.
Wana JF.
Kama wachambuzi wengi makini wa siasa walivyotabiri, CHADEMA imeshindwa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba2015. Ingawa kushindwa huko kwa CHADEMA kumechangiwa na mambo mengi, lakini kubwa zaidi ni makosa yaliyofanywa na mwenyekiti wake mh. Freeman Mbowe kushinikiza chama kimsimamishe mgombea asiyekubalika.
Ingawa baadhi ya watu wakiangalia juu juu wanaona mgombea aliyeletwa na Mbowe ameleta manufaa, lakini ukiangalia hesabu kwa makini utaona kuwa mgombea huyo hajakinufaisha chama na badala yake amekiletea chama hicho migogoro na kukitenganisha na agenda yake kuu ya ufisadi.Mwaka 2005 mgombea wa CHADEMA mh. Freeman Mbowe alipata asilimia 5.88 ya kura za urais. Mwaka 2010 mgombea Dr. Slaa alipata asilimia 27.05.
Hii ni tofauti ya asilimia 21.17 au ongezeko la asilimia 360 ikilinganishwa na 2005.Vilevile, mwaka 2005 Chadema ilipata majimbo 5. Mwaka 2010 ilipata majimbo 23. Ongezeko hili la majimbo 18 ni sawa na asilimia 360.Mafanikio haya waliyapata CHADEMA bila kuhitaji msaada wa mgombea wa kuazima toka CCM. Kama waliweza wenyewe kufika hapa, ni sahihi kuamini kuwa wangeweza kwenda mbali zaidi.katika uchaguzi wa mwaka huu,CHADEMA wamepata asilimia 39.97. Hii ni tofauti ya asilimia 12.92 ikilinganishwa na matokeo ya chadema ya mwaka 2010.
Hapa utaona kuwa ongezeko aliloleta mgombea "wa kuazima toka CCM" ni dogo kuliko ongezeko aliloleta Slaa la asilimia 21.17.Kwenye ubunge, mwaka huu CHADEMA imepata majimbo 39. Hili ni ongezeko la majimbo 16 ambayo ni sawa na ongezeko la aslimia 69.6. Hapa utaona kuwa mgombea "wa kuazima toka CCM" ameshindwa kuongeza kiasi cha majimbo kama alichoongeza Slaa mwaka 2010.
Ikumbukwe kuwa mgombea wa mwaka huu aliungwa mkono na vyama vinne vya upinzani tofauti na miaka iliyopita ambayo mgombea wa CHADEMA alikuwa anasimama peke yake. Kuungwa mkono huku kulimfanya pia mgombea huyo awe na wabunge wengi wa majimbo (47) wanaompigia kampeni Bara na Visiwani. Dr. Slaa alikuwa na wabunge watano (5) tu waliompigia kampeni.-Pamoja na kuungwa mkono huko lakini bado mgombea hajafanikiwa kuleta mafanikio zaidi ya mwaka 2010.Hitimisho:Woga wa Mbowe umeiponza CHADEMA bure. CHADEMA ilishaanza kujiimarisha kitaasisi na sasa sura ya kitaasisi imebomolewa na kujengwa sura ya kutegemea jina la mtu mmoja.
Kauli za Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA kuwa hawawezi kushinda uchaguzi bila kuchukua kigogo toka CCM itawatafuna siku za usoni na kuwakatisha tamaa wafuasi wao kwenye chaguzi zijazo iwapo hawatapata kigogo wa CCM wa kugombea kupitia CHADEMA.CHADEMA ina jukumu kubwa la kutafuta mtu wa kufidia nafasi ya Dr. Slaa.
Kihesabu hakuna mtu aliyevuna mafanikio makubwa kwa CHADEMA kama Dr. Slaa. Lowassa ameshafikia kilele chake, haongezeki tena nguvu. Kama ameshindwa kufikia level ya Dr. Slaa katika uchaguzi huu, basi hataifikia tena.Uchaguzi huu ni fundisho kwa vyama kuthamini mafanikio ya hatua kwa hatua inayojipatia yenyewe kwa kuheshimu misingi yake kuliko kukimbilia tamaa za kuenda ikulu kwa kubomoa misingi iliyojengwa kwa miaka mingi.
Cc; Zemarcopolo.
Usiwaangalie CUF tu waangalie na NCCR Mageuzi pamoja na NLD wamenufaika vipi na Lowassa?Cuf leo wamepata wambunge wengi kuliko 2010
Usiwaangalie CUF tu waangalie na NCCR Mageuzi pamoja na NLD wamenufaika vipi na Lowassa?
Wana JF.
Kama wachambuzi wengi makini wa siasa walivyotabiri, CHADEMA imeshindwa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba2015. Ingawa kushindwa huko kwa CHADEMA kumechangiwa na mambo mengi, lakini kubwa zaidi ni makosa yaliyofanywa na mwenyekiti wake mh. Freeman Mbowe kushinikiza chama kimsimamishe mgombea asiyekubalika.
Ingawa baadhi ya watu wakiangalia juu juu wanaona mgombea aliyeletwa na Mbowe ameleta manufaa, lakini ukiangalia hesabu kwa makini utaona kuwa mgombea huyo hajakinufaisha chama na badala yake amekiletea chama hicho migogoro na kukitenganisha na agenda yake kuu ya ufisadi.
Mwaka 2005 mgombea wa CHADEMA mh. Freeman Mbowe alipata asilimia 5.88 ya kura za urais. Mwaka 2010 mgombea Dr. Slaa alipata asilimia 27.05.
Hii ni tofauti ya asilimia 21.17 au ongezeko la asilimia 360 ikilinganishwa na 2005.Vilevile, mwaka 2005 Chadema ilipata majimbo 5. Mwaka 2010 ilipata majimbo 23. Ongezeko hili la majimbo 18 ni sawa na asilimia 360.Mafanikio haya waliyapata CHADEMA bila kuhitaji msaada wa mgombea wa kuazima toka CCM.
Kama waliweza wenyewe kufika hapa, ni sahihi kuamini kuwa wangeweza kwenda mbali zaidi, katika uchaguzi wa mwaka huu, CHADEMA wamepata asilimia 39.97. Hii ni tofauti ya asilimia 12.92 ikilinganishwa na matokeo ya chadema ya mwaka 2010.
Hapa utaona kuwa ongezeko aliloleta mgombea "wa kuazima toka CCM" ni dogo kuliko ongezeko aliloleta Slaa la asilimia 21.17.
Kwenye ubunge, mwaka huu CHADEMA imepata majimbo 35. Hili ni ongezeko la majimbo 16 ambayo ni sawa na ongezeko la aslimia 69.6. Hapa utaona kuwa mgombea "wa kuazima toka CCM" ameshindwa kuongeza kiasi cha majimbo kama alichoongeza Slaa mwaka 2010.
Ikumbukwe kuwa mgombea wa mwaka huu aliungwa mkono na vyama vinne vya upinzani tofauti na miaka iliyopita ambayo mgombea wa CHADEMA alikuwa anasimama peke yake. Kuungwa mkono huku kulimfanya pia mgombea huyo awe na wabunge wengi wa majimbo (47) wanaompigia kampeni Bara na Visiwani.
Dr. Slaa alikuwa na wabunge watano (5) tu waliompigia kampeni.-Pamoja na kuungwa mkono huko lakini bado mgombea hajafanikiwa kuleta mafanikio zaidi ya mwaka 2010.
Hitimisho:Woga wa Mbowe umeiponza CHADEMA bure.
CHADEMA ilishaanza kujiimarisha kitaasisi na sasa sura ya kitaasisi imebomolewa na kujengwa sura ya kutegemea jina la mtu mmoja.
Kauli za Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA kuwa hawawezi kushinda uchaguzi bila kuchukua kigogo toka CCM itawatafuna siku za usoni na kuwakatisha tamaa wafuasi wao kwenye chaguzi zijazo iwapo hawatapata kigogo wa CCM wa kugombea kupitia CHADEMA.CHADEMA ina jukumu kubwa la kutafuta mtu wa kufidia nafasi ya Dr. Slaa.
Kihesabu hakuna mtu aliyevuna mafanikio makubwa kwa CHADEMA kama Dr. Slaa. Lowassa ameshafikia kilele chake, haongezeki tena nguvu. Kama ameshindwa kufikia level ya Dr. Slaa katika uchaguzi huu, basi hataifikia tena.
Uchaguzi huu ni fundisho kwa vyama kuthamini mafanikio ya hatua kwa hatua inayojipatia yenyewe kwa kuheshimu misingi yake kuliko kukimbilia tamaa za kuenda ikulu kwa kubomoa misingi iliyojengwa kwa miaka mingi.
Cc; Zemarcopolo.
mafanikio ya chadema na ukawa yameonekana dhahiri ,kwa mfano CUF wamefanikiwakuongeza idadi wabunge ,chadma imefnikwa kuongeza idadi ya kura za raisi na meya majiji matano.
Shehe ponda vipi mambo yake?ccm wamekataa kuwapa haki yao ya kiwanja cha shule future ya waislamu vipiunaweza fafanua hili.
Swissme