Ni kwanini Lowassa na Sitta hawakuchangia hoja ya muswada wa katiba?

RUMANYIKA

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
315
74
Wadau wa Jf hivi kwanini? Mbunge wa monduli na wa urambo mashariki huwa hawajadiri au kuchangia hoja zinazo wahusu wtz moja kwa moja. Suala kama la jairo, wizara ya uchukuzi,wizara ya nishati na madini kuhusu dharura, sheria ya ununuzi wa vitu vilivyotumika kwa dharura na Hili kubwa kuliko la muswada wa katiba. Tumeona sitta ametaka asionekane mnafki amejidai kwenda india kumjulia hali swaiba wake na ndugu lowassa akiwa bungeni akisikiliza vilaza wenzie wanavyo bwabwaja bila aibu. Je kutochangia kwa hawa wabunge ni kuepuka migongano na wananchi kwa kuwa wana malengo ya muda mrefu kisiasa?
 
kuchangia mswada kama huu kunaweza ku boomerang ndio maana wenye akili hawakuzungumza
 
Lowasa kuhusishwa na ufisadi cyo kama hana akili.anajua uhuni w ccm thts why kauchuna
 
Kwa Sitta sijui kwa nini hakushiriki, ila EL ni kuwa tayari chombo chake kiteule (Bi. Kiroboto) kilikuwa kinawajibika ipasavyo kuibaka demokrasia.
 
Hawataki kuharibu CV zao kwa kuchangia maamuzi mepesi,inaonekana tayari wameona kuna mkono wa mkubwa nao haakubaliani na mkubwa ni sawa na funika kombe mwanaharamu apite
 
Nasikitika mzee samwel sitta umekaa kimya kabisa kuhusu suala la katiba huku ulijipambanua kuwa uko kwa maslahi ya taifa la mtanzania, na utatetea ukweli bila kumuogopa yeyote yule pale unapoona masuala ya kitaifa yanaenda ndivyo sivyo! Kwanza ulijidhalilisha kuwemo bungune kujadili mswada ambao unapingwa na watanzania walio wengi! Tunaomba tamko lako maana katiba ni bora zaidi kuliko dowans.
 
Back
Top Bottom