Ni kosa lipi alilofanya jk linalomgharimu hadi sasa?

mpuuzi

Member
May 29, 2010
99
17
Mimi hadi sasa siamini kama Muungwana ni kiongozi mbovu kama wengi wanavyoamini. Ila ninachojua alivyoanza kazi hakuwa mwangalifu na ndio maana anatumia nguvu nyingi sasa ku rectify mambo na bado jahazi linayumba sana.

Wana JF, tunaweza kusema waziwazi kuwa kosa kubwa sana la Muungwana lilikuwa wapi? Na endapo akirekebisha hilo nchi haitayumba?

Wapo wengine wanaodai kuwa alikosea kwenye baraza lake la kwanza la mawaziri alipoweka mawaziri 60 ambao hawakuwa na tija.....

Wengine wanasema alikosea kuweka maswahiba wake kiasi ambacho alishindwa kuwakemea pindi wafanyapo madudu...

Wapo wanaosema kuwa ziara zake nyingi mwazoni kabisa mwa utawala wake zilimkosesha direction

tusaidiane jamani, tumsaidie Rais wetu huenda na yeye hajui alikosea wapi!
 
Kosa lake kubwa ni kugombea uraisi, nafasi ambayo hana uwezo nayo na litakuwa kubwa zaidi akigombea tena mwaka huu!
 
Alipotia timu tu, RICHMOND ikaanza kurindima. Utawala wake wa miaka mitano ya kwanza umekuwa defined na richmond scandal ambayo hadi leo haijawahi kuwa addressed conclussively. Kuamua kuwashitaki kina Liyumba na kuwafunga was OK. Lakini RICHMOND kuiweka chini ya kapeti haitoshi. RICHMOND ITAENDELEA KUMTESA HATA BAADA YA OCTOBA 2010. RICHMOND IS NOT YET DEAD.
 
Mimi hadi sasa siamini kama Muungwana ni kiongozi mbovu kama wengi wanavyoamini. Ila ninachojua alivyoanza kazi hakuwa mwangalifu na ndio maana anatumia nguvu nyingi sasa ku rectify mambo na bado jahazi linayumba sana.

Wana JF, tunaweza kusema waziwazi kuwa kosa kubwa sana la Muungwana lilikuwa wapi? Na endapo akirekebisha hilo nchi haitayumba?

Wapo wengine wanaodai kuwa alikosea kwenye baraza lake la kwanza la mawaziri alipoweka mawaziri 60 ambao hawakuwa na tija.....

Wengine wanasema alikosea kuweka maswahiba wake kiasi ambacho alishindwa kuwakemea pindi wafanyapo madudu...

Wapo wanaosema kuwa ziara zake nyingi mwazoni kabisa mwa utawala wake zilimkosesha direction

tusaidiane jamani, tumsaidie Rais wetu huenda na yeye hajui alikosea wapi!
we mpuuzi!
unauliza swali wakati una majibu tayari!?
 
Kosa la kimsingi alilolifanya ambalo mtawala yeyote asiye makini litamsumbua na kuingiza wanamtandao kwenye baraza lake la mwanzo wengi wao wakiwa ni mizigo ya utawala uliopita.Matokeo yake baada ya Richmond wote walilazimika kuanguka na kuanza moja na watu wasio wake.Atalikumbuka sana kosa hilo mwaka huu maana ndio utakuwa mtaji wa kampeni kwa wapinzani wao.
 
Mimi hadi sasa siamini kama Muungwana ni kiongozi mbovu kama wengi wanavyoamini. Ila ninachojua alivyoanza kazi hakuwa mwangalifu na ndio maana anatumia nguvu nyingi sasa ku rectify mambo na bado jahazi linayumba sana.

Wana JF, tunaweza kusema waziwazi kuwa kosa kubwa sana la Muungwana lilikuwa wapi? Na endapo akirekebisha hilo nchi haitayumba?

Wapo wengine wanaodai kuwa alikosea kwenye baraza lake la kwanza la mawaziri alipoweka mawaziri 60 ambao hawakuwa na tija.....

Wengine wanasema alikosea kuweka maswahiba wake kiasi ambacho alishindwa kuwakemea pindi wafanyapo madudu...

Wapo wanaosema kuwa ziara zake nyingi mwazoni kabisa mwa utawala wake zilimkosesha direction

tusaidiane jamani, tumsaidie Rais wetu huenda na yeye hajui alikosea wapi!
hapo kwenye bold kamuulize Mrema ambaye amejitolea kufa na rais ambaye hata akikosea yeye anasema hana hatia.

makosa aliyoyafanya JK mpaka sasa ni kukutuma wewe kuja hapa kusaka majibu ya maswali atakayoulizwa kwenye kampeni.

Usiwe na shaka tutakutana naye jukwaani atujibu maswali yetu. na TUTAMPIMA
 
Join Date
Sat May 2010
Posts
19
Thanks : 6
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power
0

Wakuu watu kama hawa watakuja sana humu!! Tunajua wanaingia sana humu maana wanajua kuna majibu ya baadhi ya makosa yao. Huyu katumwa na mjumbe hauwawi... We mpuuzi nenda karudishe majibu kuwa, kosa la muungwana ni kutaka uraisi ilhali akijua hana uwezo wa kuongoza!! Mkwere huyo ameajawa na mizaha mizaha tu... Nenda bana!!:angry:
 
kama Nyambala alivyosema, kosa lake ni kugombea nafasi nzito kuliko uwezo wake kiakili, kiuadilifu na kimwenendo. nafasi ile ni yajuu sana kwake.
kosa lingine ni kufanya uteuzi wa kijinga, wakujizungushia wajinga katika nafasi za juu za kitaifa, Kingunge, Kapuya, Malima, Masha, Sophia Simba, Kawambwa Shukuru, MsollA, etc.
kuweka walafi wenzie kama Karamagi, Lowassa , kwenye nafasi za juu zautawala.
 
Mkulo waziri wa fedha ambaye kwa muda wote aliokalia ofisi hajui status ya uchumi wa taifa....
 
Kosa lake kubwa ni kuweka viongozi waloukuwa waoga, sizungumzii uoga wa JK kudili na mifisadi iliyo kubuhu nazungumzia uoga wa viongozi wasiokuwa na mapendo ya ukweli na nchi yao.Kuunda sera mbovu za kumzuia mtanzania mwenye bidii kwa kuogopa challenge la wimbi la vijana wakesho kuja kuleta changamoto za kweli baadae, wao wanafikiria kupachika mitoto yao hata kama ni mi mbumbumbu huu ni uoga. Mfano balozi nyingi zimefuta utaratibu wa kupata passport za kitanzania ugenini na masharti chungu mtele yasio kuwa na kichwa wala miguu.

Kutokua na sera za kuwaanda vijana wakitanzania nyumbani kupambana au kuweza kujua maadili ya kazi, sidhani kama wawekezaji wageni wangelilia wakenya kama watanzania wengi wangekua na heshima na kazi bila kuleta ujanja ujanja wa kishamba ambao unaliumiza shirika au kulemeza target za shirika.

Kushindwa kumuweka mtu sahihi kurekebisha uchumi unaotoa picha ya uongo kutokana na rushwa kubwa iliyoko tanzania matokeo yake inflation seems is beyond control kisa tabia za watanzania wengi kujifunza kuishi kutokana na mazingira ya rushwa ikiwa mtindo. Mbaya zaidi wale wasiokuwa na nafasi za kuiba kuishia kupata tabu za maisha. Ujambazi uliokithiri ni ishara ya tabu za maisha tanzania.

Kushindwa kuelewa yeye mwenyewe Tz anataka iendelee wapi au aiache vipi na kizazi kijacho kimkumbuke vipi na legacy zipi apart from laxing free speech to a limit.

Kushindwa kujua kumzuia mtanzania mwenye nia ni sababu za kudoroza maendeleo iwe upinzani, mtu, mwanafunzi, mwalimu, mfanyabiashara na wengine wote, kuruhusu dini ziwe na sauti za ajabu katika siasa zetu, kukosa mipangilio ya kesho na kutojua solution za matatizo yao.

Wapo watanzania wengi wanao ipenda nchi yao na ubunge, umeneja sijui na upuuzi mwingine wenye channel za ufisadi azipo akilini mwao. Watu wanataka warudi waseme openly what is wrong and what ought to be done openly hili watanzania wanufaike bila ya uoga wa polisi au hata hao wageni mnao waalika baadae uenda wakageuka maadui kwa wasema kweli kwa kuwa tunataka kuwanyan'ganya tonge na lirudi kwa watanzania.

Uzalendo ni kujijua wewe ni nani, na ni nani anahaki kubwa ya faida ya tanzania. Foreigners wasipewe kipa umbele mbele ya wazawa, hila inabidi kuwaanda wazawa wawe tayari kuwa na fikra za maendeleo na kuchukua nafasi za kuleta maendeleo. Tunaposoma vijana wakitanzania ni second best kwenye nafasi za kazi au mashirika ya kazi kutangaza ajira kwa vijana wakitanzania waliopo nje something is not right there. Kwani hao waliopo numbani ndio wanao staili hizi nafasi kwanza. Either training wanayo pewa ni mbovu, training si degree au cheti tu bali hata descipline kazini. Yote hayo yatakuwa hadithi mpaka JK ajue kuweka watu wanao elewa kazi na si marafiki hili malalamiko yanapofika wanakuwa fired without hesitations, wasiweke watu kwa fadhila bali kwa merit.

Na kama kazi inamshinda ni bora aiwache akae aangalie mechi zake za mpira awapishe wenye uwezo na uelevu what needs to be done.
 
Join Date
Sat May 2010
Posts
19
Thanks : 6
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power
0

Wakuu watu kama hawa watakuja sana humu!! Tunajua wanaingia sana humu maana wanajua kuna majibu ya baadhi ya makosa yao. Huyu katumwa na mjumbe hauwawi... We mpuuzi nenda karudishe majibu kuwa, kosa la muungwana ni kutaka uraisi ilhali akijua hana uwezo wa kuongoza!! Mkwere huyo ameajawa na mizaha mizaha tu... Nenda bana!!:angry:
Jamaa kweli mpuuzi, anauliza wakati majibu tayari anayo! si bure ametumwa!
 
Kutokana na kutokuwa na uwezo wa ku-hold nafasi kubwa ya uraisi amekuwa anatumia nguvu nyingi sehemu ambayo haistahili. Nguvu nyingi kwenye tatizo la wafanyakazi walipa kodi na usanii mwingi kwa mafisadi wanamtandao. Matumizi makubwa sana kwenye ziara za kitalii nje ya nchi na fedha kiduchu kwenye huduma za jamii.
 
Ukitaka usikosee, usifanye lolote. JK kafanya anavyoweza. Mambo yanakwenda ingawa si yote, kwa viwango,vipimo na vionjo vyetu. Baadhi yetu tulikuwa na "Marais" wetu ambao hawakuwa. Kwetu sisi JK si lolote si chochote! Kakosea sana, kagombea nafasi haimudu. Hatusemi kashindwa lipi kwa saana kiiivo!
 
KOSA KUBWA -
1 - Ku-underestimate presidency ilhali hakuielewa mechanism inayoendesha hiyo kitu. Presidency is an institution not a person, na anashindwa kwa sababu amekuwa akijaribu kuipersonalize na si kuendelea kui-institutionalize na ku-uphold values zake.

2 - Uswahiba na utawala ni maji na petrol, havichangamani. Amejitahidi kuchanganye na sasa ameamua kuwaingiza hata watoto wao as if Tanzania is a Kingdom.
ON Uswahiba na urafiki
ukisoma Bible when King solomon died, mwanaye alitawala, akawakaribisha maswahiba na washikaji kama washauri wake (just like JK) the end result was that the United Israel Kingdom split. Judah and Benjamin on one side and other 10 groups on the other.
It might even cost huo muungano wao ambao sisiemu wanajivunia kila kukicha. and it is very near.
 
Ukitaka usikosee, usifanye lolote. JK kafanya anavyoweza. Mambo yanakwenda ingawa si yote, kwa viwango,vipimo na vionjo vyetu. Baadhi yetu tulikuwa na "Marais" wetu ambao hawakuwa. Kwetu sisi JK si lolote si chochote! Kakosea sana, kagombea nafasi haimudu. Hatusemi kashindwa lipi kwa saana kiiivo!

kashindwa kuleta maisha bora kama alivyoahidi, ameshindwa kuboresha hali ya maisha ya Walimu kama alivyoahidi, kaisha kuchekacheka tu
 
Jk hana kosa. aliutaka uraisi tangu 95 lakini bahati mbaya hakujua majukumu ya raisi.
Alidhani akiwa rais atapata nafasi ya 'kuwatoa' kimaisha na kuwaongezea umaarufu maswahiba zake.
Asiyejua alitendalo hana makosa.
 
kashindwa kuleta maisha bora kama alivyoahidi, ameshindwa kuboresha hali ya maisha ya Walimu kama alivyoahidi, kaisha kuchekacheka tu

Maisha bora yapo ingawa sio kwa viwango vinavyolingana kwa wote. Leo hii hapa Dar magari hayana pa kupita, nyumba zinachipuka kama uyoga, vyuo vikuu vimejaa Watoto wetu, ukienda pale MlimaniCity hapatoshi masaa yote,.......
 
Back
Top Bottom