Ni kawaida kwa wahuni kumzushia jambo mtu mwema

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,522
22,015
Mhuni wa kiume atamzushia kuwa kamla mdada mwenye kujiheshimu ili kuharibu heshima yake.
Hali kadhalika mdada mhuni atazusha vivyo hivyo kwa mkaka mwenye kujiheshimu.

Kuna mhuni atakuzushia kwamba umeiba kwa mwajiri wako ili akuharibie kibarua chako, kuna wahuni watakuzushia kwamba una makundi ya kigaidi na unataka kupindua serikali. Watazusha ili wakugombanishe kisiasa.

Ikiwa watu wanaweza kuzusha uongo katika jina la Mungu, kwa nini huwa unastuka wanaposema uongo kuhusu wewe?

Ikiwa watu walimzushia Yesu kuwa ni mlevi na mwenye pepo, kwa nini upoteze akili unapozushiwa uongo?

Yusufu alizushiwa uongo kwamba alimbaka mke wa bosi wake, Yusufu alitulia japo alipelekwa gerezani lakini Mungu alimthibitisha kwa kumtoa gerezani na kumpa ukuu.

Sio lazima kupigana jino na kucha ili kutakasa jina lako . Tulia, kisasi ni cha Mungu.

Ubarikiwe.
 
Mhuni wa kiume atamzushia kuwa kamla mdada mwenye kujiheshimu ili kuharibu heshima yake. Hali kadhalika mdada mhuni atazusha vivyo hivyo kwa mkaka mwenye kujiheshimu...
Je, unajua kitu kinachoitwa Black Propaganda? Au Characters Assassination and Smear Campaigns??
Watu wa 'Dawati la Propaganda' ndio kazi yao hii, usifikiri watu wote wanaowazushia watu wenzao mambo ya uongo ni wahuni.No.
 
Mhuni wa kiume atamzushia kuwa kamla mdada mwenye kujiheshimu ili kuharibu heshima yake. Hali kadhalika mdada mhuni atazusha vivyo hivyo kwa mkaka mwenye kujiheshimu....
nyakati hizi katika maeneo mengi uovu umejificha katikati ya wema....

wema unatumika sana kuwaliza watu kwa uovu...
 
Je, unajua kitu kinachoitwa Black Propaganda? Au Characters Assassination and Smear Campaigns??
Watu wa 'Dawati la Propaganda' ndio kazi yao hii, usifikiri watu wote wanaowazushia watu wenzao mambo ya uongo ni wahuni.No.
Kwa hiyo kanusho la mama kuwa na machawa sio mpango wa wahuni?
 
Back
Top Bottom