Ni halali Diamond na Harmonize kuwarushia watu fedha?

Mh.🤔🤔🤔 Afadhari ya hao wanagawa fedha bila ubaguzi kwa kuzirusha na yule anayegawa fedha kwa ubaguzi kwa kusimamisha msafara wake....! (Just a joke)
Ila naamini kila mtu ana uhuru wa kutumia fedha yake namna anavyoona inafaa cha msingi avunji sheria. Kwa upande wa wasanii ni kuleta hamasa katika show zao.
 
Nimeona clip za video zikiwaonesha Diamond akiwa Kahama na Harmonise akiwa Mtwara, wakirusha fedha na wanachi wakizigombania. Nauliza tu imekaaje kwenye sheria zetu za fedha?
Hela zao


Kwanini huulizi zile za zinazotokana na Kodi zako kwenye maziara ya Jiwe na Mwanae
 
daahh... nimecheka sana hizi comnt, hakuna hata mmoja anaesema diamond achukuliwe hatua au anavunja sheria, nikajiuliza kwanini!? kumbe ni kua kuna vifutu wawili wao kutwa kugawa fedha na SAA nyingine wakigawa kama zawadi tena kwa upendeleo kitu ambacho kinawaumiza watu, basi wanaona bora diamond anaegawa kwa kila mtu bila kujali😂😂
 
Wanarusha pesa,zinagombaniwa zinachanwa. Tusubiri kauli ya serikali wenye fedha zao. Mtu anadhani fedha ni mali yake, Kumbe yake ni ile thamani tu.
 
Mimi mwenyewe juzi masubwe nilidaka 50elfu kizembe zembe namshukuru diamond kwa ujio wake
 
Back
Top Bottom