Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Ili kuimarika kuna mapitio mengine ni muhimu kuyapitia ili yawe ukumbusho wa kukosa pale ukipata.

Ila kiukweli kabisa hakuna faraja kwenye ufukara.

Nakumbuka kuna kipindi nilipigika ikawa natembelea washkaji mida ya misosi kiasi cha kujua ratiba ya mlo wa masela wote.

Kuna msela wangu (Mungu amlaze mahala pema) ilikuwa ikifika jioni ananipigia simu kuniita tukapige story, kumbe alishajua hali yangu na ule wito ulikuwa ni msaada indirectly maana alihakikisha nakula ndio naondoka.

Na kila nikiondoka mkewe ananipa kikontena cha msosi ananiambia shem naona chakula cha leo umekipenda beba na hiki utakula baadae.

Hawakujua jinsi gani walikuwa wakinisevu.
Maisha ni mazuri mkikutana mnaoelewana
Tuishi kwa kusaidiana ndio maana ya maisha na usela wa kweli
 
Kuna muda niko Dar mwaka 2016-17.
Baada ya kufukuzwa kazi serikalini kipindi cha Magufuli na kufilisika na kukosa pa kushika, Nilibakiwa na suruali moja ikachanika bahati mbaya kwa msumari wa kwenye benchi nikashona kiraka kabisaa kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu.
Nilishatembea hadi Tandale ndani ndani kwa Mama mmoja hivi kwenda kula msosi wa buku na nilikula jioni hiyo tu hadi kesho tena jioni. Kodi ya nyumba iliisha nikaishia kulala chumba cha mlinzi.

Bahati nzuri baada ya mwaka nikalipwa pesa yangu kutoka PSSSF zaidi ya milion 8.

Siku hiyo niliheshimu pesa na kutoutamani tena umaskini. Nilifanya biashara zangu kwa bidding na maarifa. Thanks God sasa hivi nakula ninachokitaka na sio ninachokipata.

Money is sweet
You guy....My guy....
Been a long... Happy to see you here HA
 
Da maisha haya we Acha tu sitasahau nikiwa mdogo tumekuja dar kwa shemeji yangu mm na mdogo wangu
Bas bwana mdogo wangu akaanza kuumwa hakuna aliyekuwa anajali si sister wala shemeji
Si ndo nikalopoka mbona dogo hampeleki hosp?BIG MISTAKE
Shemej akanitimua kwake nikaondoka na mdogo wangu na kwenda kuishi nyumba aliyojenga mama nikiwa na mdogo wangu mgonjwa.
Tukaanza kukaa na cjui hela ya dawa nilipataga wap dogo akapona
Mfukoni nilibakiwa na Mia 5 tena mbovu nikawa naenda na dogo kula mihogo na tunapomaliza kula ndio tunatoa ile hela na wauzaji walikuwa wanatugombeza wanaturudishia ile hela kwa hiyo kesho tunabadilisha sehemu ya kula na cha ajabu tunarudishiwa tena hiyo jero:Mungu huyu
Sasa basi kwa sababu nyumba ya shemeji ilikuwa karibu na nyumba aliyojenga mama (tulipokimbilia)watoto wa sister wakawa wanakuja kushinda pale(majaribu hayo)
Ikabidi nishindwe kuacha kuwapa chakula wale watoto wa ndugu yangu nakumbuka nilitumiwaga elfu 30 na mama hivyo tukawa tunakula kwa kujibana na wale watoto wa dadangu(japo kwao kulikuwa na kila kitu)ila c unajua watoto
Yaani nilikabidhiwa jezi na mchezo wala siujui..ikabidi ninunue gunia la mkaa nianze kuuza na mdogo wangu(kumbuka wote ni watoto)ili tuweze kupambana na jiji la dsm
Mungu alileta mkomboz yule mzee wa bandari(mungu akurehemu)yaan yule kuku uliyetununulia pale bandari atukuwahi tena kula kuku mtamu kama yule(nadhan kuku kwa wakati ule kilikuwa kitu cha Thaman sana kwetu)
Now tumekuwa tunataman kurudisha fadhila kwako ila ndo hivyo kazi ya mungu
 
What's good, my good friend My Makiwendo. Tokea huku Zanzibar tuenjoy best.

Maisha sasa hivi mazuri I can afford kula na kulala hata kwenye fancy hotel na wanene kuna kipindi it was horrible situation.

Kwa sasa wananiita Bosi kazi, nishatemana na umaskini.

Sasa hivi namshukuru Mungu kwa wema wake kwangu nakula vinonoView attachment 2662420View attachment 2662421
See God now!!!!

Mungu anatutoa mbali, anatupeleka mbali....Glory to the Most high alone.

As long as your happy,I'm happy and GOD is Happy..
Enjoy life My friend Humble..Wewe ni mtu poa sana.... Na unastahili kila kilicho chema kwenye hii Dunia...

NB,Usiwe unapotea namna hii hapa jukwaani..Wewe una vitu vyako special sana sana...Hatuvipati popote hapa...Amini kwamba.
 
Kuna muda niko Dar mwaka 2016-17.
Baada ya kufukuzwa kazi serikalini kipindi cha Magufuli na kufilisika na kukosa pa kushika, Nilibakiwa na suruali moja ikachanika bahati mbaya kwa msumari wa kwenye benchi nikashona kiraka kabisaa kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu.
Nilishatembea hadi Tandale ndani ndani kwa Mama mmoja hivi kwenda kula msosi wa buku na nilikula jioni hiyo tu hadi kesho tena jioni. Kodi ya nyumba iliisha nikaishia kulala chumba cha mlinzi.

Bahati nzuri baada ya mwaka nikalipwa pesa yangu kutoka PSSSF zaidi ya milion 8.

Siku hiyo niliheshimu pesa na kutoutamani tena umaskini. Nilifanya biashara zangu kwa bidding na maarifa. Thanks God sasa hivi nakula ninachokitaka na sio ninachokipata.

Money is sweet
Mzee baba upo?
Msalimie CCNP Engineer
 
Hata mimi naamini hivyo. Hii dunia haikuwa mahala pake.

Yule jamaa alikuwa na roho ya kipekee. Hakusubiri kuombwa.

Hii story yangu ni cha mtoto, baada ya mauti yake waliibuka wengi mno. Kuna aliowapa hifadhi ya makazi, aliowapa mitaji na hata aliolipia ada za watoto wao.

Kuna binadamu Mungu aliwaumba waje kuwa mfano wa wema tu kwa binadamu halafu waondoke.
Nimesoma hii Comment yako machozi yamenilenga

Iko hivi Mkuu...Kuna watu ni Daraja,Baraka katika maisha ya watu wengine....Hata wewe pia...

Hujawahi kuona unaweza kuwa kwenye changamoto fulani halafu Mungu anamleta mtu wewe mwenyewe huelewi..Then huyo mtu atakusaidia kwenye hiyo changamoto.. ukivuka hapo anaondoka na siyo mmegombana... ni ukaribu tu unapungua..Maana yake ni nini? Kazi yake ameimaliza...Anatakiwa akafanye kingine kwa wengine na wengine tena...Hawa watu wanaitwa "Destiny Helper"
 
Back
Top Bottom