Ni CCM national congress au music concert?

Fareed

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
328
135
Naona live kwenye TBC sasa hivi mkutano mkuu wa CCM (national congress) ukiendelea Dodoma. Sehemu kubwa ya mkutano umechukuliwa na burudani za muziki wa ToT, TMK, Dokii, Flora Mbasha, vijana wa chuo na kadhalika. Wasanii kama kina Dokii wakisha perform wanapanda high table na kuruhusiwa kuwakumbatia kina marais na kuomba pesa. Naona hata Kikwete na Mzee Mkapa wametoa pochi na kugawa pesa kwa kina Dokii.
Kikwete meno nje, yuko excited kama mtoto akiona pipi na ametoa macho kusherekea muziki wa Bongo fleva. Nyimbo ni za kumsifia Kikwete tuuu. Mkapa anaonekana yuko bored balaa.
Kweli Rais tunaye!
 
Sasa kasimama Kiongozi wa Upinzani wa TLP Augustine Mrema anamtetea Kikwete kwa "uongozi uliotukuka" na kuomba Watanzania wasimtose kwani anapambana sana na ufisadi na aendelee tena na second term. "CCM mnatisha, mlitugaragaza 2000 na 2005," alisema Mrema huku akicheza wimbo wa ToT wa "CCM Nambari One."
 
Kweli watu kama wakina mrema wameishiwaaa! HIVI WATANZANIA KATUROGA NANI? MBONA HATUBADILIKI...Yaani we waone hao wanvyochekelea..kesho utawakuta hao hao wanalia gharama ya maisha.....HIVI TUMELOGWAAAAAAAAAAAAAAAAAAA?

CHADEMA WANAUMEEEEEE PEKEE
 
Sasa kasimama Kiongozi wa Upinzani wa TLP Augustine Mrema anamtetea Kikwete kwa "uongozi uliotukuka" na kuomba Watanzania wasimtose kwani anapambana sana na ufisadi na aendelee tena na second term. "CCM mnatisha, mlitugaragaza 2000 na 2005," alisema Mrema huku akicheza wimbo wa ToT wa "CCM Nambari One."
Naomba kwenye post zako usimseme Mrema maana hata yeye anajua hana rafiki kwa wapinzani wa serikali hii ndio sababu kaamua awe sisi m b. Ni kibaraka aliyetumwa kuhakikisha upinzani hausogei mbele. Baada ya kugundulika sasa kajiweka wazi. UWT @work.
Binafsi huwa sitaki hata kumsikiliza. Nikisikia anaanza nazima TV nakwenda zangu au nabadilisha channel.
 
...hawana jipya la kuwaambia wamachama wao na wananchi so the have to depend on the poor artists for two cent cheap popularity!
 
Sasa kasimama Kiongozi wa Upinzani wa TLP Augustine Mrema anamtetea Kikwete kwa "uongozi uliotukuka" na kuomba Watanzania wasimtose kwani anapambana sana na ufisadi na aendelee tena na second term. "CCM mnatisha, mlitugaragaza 2000 na 2005," alisema Mrema huku akicheza wimbo wa ToT wa "CCM Nambari One."

Lipumba kasema nini naye auhakupewa nafasi?Mbona chadema hawakualikwa?
 
Teh teh teh! Mrema bwana! Anaongea utafikiri kapandwa na mashetani. Unbelievable! Naona CCM wamemshangilia sana.
 
Its so disgusting...The late Baba wa Taifa once said the guy wasn't fit enough for presidency post.....So bad why he never said when he'll be fit for this post..........but i guess it wasn't a right time and yet still its not a right time.......This ship is sinking........
 
Lipumba kasema nini naye auhakupewa nafasi?Mbona chadema hawakualikwa?

Lipumba hakupewa nafasi ya kuongea. CCM wanajua asingeweza kuwapa sifa za kijinga kama Mrema na kiongozi wa UPDP aliyemfananisha JK na Yesu. Hapo amekosekana tu John Cheyo wa UDP kutimiza listi ya viongozi wa upinzani walionunuliwa na kampeni ya Kikwete. Chadema nadhani wamefanya busara kukacha kikao hiki cha upuuzi.
Pamoja na ujinga mwingi alio ongea Mrema, kanifurahisha alivyosema JK alimtosa waziri mkuu wake na kuvunja baraza la mawaziri kutokana na kashfa ya ufisadi wa Richmond. Lowassa na Mkapa walionekana kununa sana na kuwa na hofu ya kuumbuliwa Mrema alivyo zungumzia ufisadi serikalini.
Mrema practically begged CCM wamwachie jimbo la ubunge la Vunjo. Wakijua kuwa Mrema kafulia, wana CCM wakampa mwanasiasa huyo pesa kama mwanamuziki wa taarabu. Mrema akapokea pesa hizo na kuweka mfukoni.
 
Sasa kasimama Kiongozi wa Upinzani wa TLP Augustine Mrema anamtetea Kikwete kwa "uongozi uliotukuka" na kuomba Watanzania wasimtose kwani anapambana sana na ufisadi na aendelee tena na second term. "CCM mnatisha, mlitugaragaza 2000 na 2005," alisema Mrema huku akicheza wimbo wa ToT wa "CCM Nambari One."

jamaa njaa inamsumbua na hana jipya mtu wao.
 
Mrema ni aibu hata kumzungumzia. Wale waliomuona akibwabwaja pale Dodoma watakubaliana nami kuwa huyu ni chizi
 
Back
Top Bottom