Ni bora wahitimu wa Darasa la Saba hasa wa shule za serikali wawe wanasoma kozi ya Kiingereza kwa maandalizi mazuri ya sekondari

Kurutu wa Mungu

JF-Expert Member
Oct 23, 2017
366
571
Wana JF, miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa kwa wazazi hususani wanaokaa mijini kuwapeleka wahitimu wa darasa la saba kusoma masomo ya sekondari kama maandalizi maarufu kama Pre form one.

Kwa upande wangu naona kama nikuwapotezea mda vijana, maana wakishafungua shule kuanza kidato cha kwanza walimu huwa wanaanzia kufundisha utangulizi (introduction) kwa kila somo nakujikuta wakirudia kile kile walichojifunza huko mitaani, huku tatizo kubwa kwao likiwa ni kuandika, kusoma na kuongea lugha ya Kiingereza.

Ni bora wangekuwa wanatumia vizuri muda wanaokaa nyumbani kujifunza Kiingereza, juzi nimekutana na vijana wanne wanatoka huko wanakosoma Pre form one, nimesikitika ata kujitambulisha kwa Kiingereza hawajui, nikawauliza maswali madogo juu ya kile walichosoma ata kutamka hayo maneno yaliwashinda, nikaona kuna umuhimu wazazi na wadau wanaowafundisha hawa vijana kuanza kujikita kuwasadia katika lugha ya kiingereza ili kuwapa mwanga pindi watakapoanza masomo ya sekondari wasiwe wagumu na wazito katika kuelewa na inaweza kuwa chachu kwao kuanza kupenda kufanya mazoezi ya kuongea Kiingereza wawapo mashuleni.
 
Hii shida ya kielimu hakuna anayetaka kuitatua.
Ni heri sasa tuamue kufundisha kiingereza huko shule ya msingi kwa masomo yote.

Yaani mtoto atoke kuongea kiswahili tena kile cha kilugha then ghafla aongee kiingereza.
Ni changamoto iliyofumbiwa macho
 
Hii shida ya kielimu hakuna anayetaka kuitatua.
Ni heri sasa tuamue kufundisha kiingereza huko shule ya msingi kwa masomo yote.

Yaani mtoto atoke kuongea kiswahili tena kile cha kilugha then ghafla aongee kiingereza.
Ni changamoto iliyofumbiwa macho
Hili janga tunaweza kulitatua tukiweka siasa pembeni maana lugha ya kiswahili kufundishia shule za msingi linatumika kisiasa zaidi
 
Kati ya wanaomaliza darasa la saba ni wangapi kati ya hao ndio husoma hizo kozi baada ya kuhitimu ndio useme eti wanarudia waliyosoma mtaani?
 
Back
Top Bottom