NguvuKazi suluhisho la kuondoa Umasikini na kujenga Uchumi!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Sheria ya Nguvu Kazi ni Muhimu Irejeshwe
Mwandishi Wetu
Daily News; Sunday,December 28, 2008 @20:00

maendeleo.JPG
1. Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Baraza la Biashara la Taifa(TNBC), Philemon Luhanjo (katikati) akibadilisha mawazo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF), Esther Mkwizu (Kulia) na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dunstan Mrutu hivi karibuni
Nguvu kazi ni fursa pekee, ambayo hutoa nafasi kwa nchi ama maeneo mbalimbali ambayo yapo nyuma kimaendeleo .Kwa kuliangalia hilo Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), linasisitiza kurejeshwa kwa sheria hiyo.

“Sheria ya nguvu kazi ni muhimu irejeshwe kwa kuwa nguvu kazi nyingi haitumiki ipasavyo, kwani wengi wanakuwa wanapoteza nguvu hizo kwenye mchezo wa Pool,”anasema Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), Dunstan Mrutu.Anasema hayo wakati akifanya mazungumzo na waandishi wa habari na kutoa majumuisho ya mdahalo wa baraza hilo.

Mdahalo huo ulikuwa wa uwezeshaji kiuchumi, uliojumuisha wakuu wa mikoa.Mrutu anasema kuwa Watanzania wengi, hawafanyi kazi katika muda unaotakiwa, kwani wanafanya kazi kwa muda mfupi.

“Utafiti unaonyesha kuwa Watanzania wanafanya kazi kwa saa chache sana ukilinganisha na watu wa mataifa mengine Afrika na nje ya Afrika. Hili ni tatizo kubwa katika kuharakisha maendeleo ya kiuchumi,” anasema Mrutu na kusisitiza umuhimu wa kurejesha sheria hiyo.

Anasema sheria hiyo ikirejeshwa, inaweza kusaidia nguvu kazi nyingi inayopotea, kwa kucheza mchezo wa pool ikarudi na kuamua kufanya kazi za uzalishaji mali na hivyo kujiletea maendeleo.

Anasema sheria hiyo iainishe kuwa asiyefanya kazi asile, kwani kwa kutumia sheria hiyo itawafanya watu kuwajibika, wakitambua kuwa wasipofanya hivyo watakuwa wamekiuka sheria ambayo adhabu zake pia ziwekwe bayana.

Anasema kuwa dhana ya kutegemea kuwezeshwa ni potofu na hivyo ni muhimu kubadilisha mtazamo huo na kuwafanya Watanzania kutumia nguvu zao katika kufanya kazi za kimaendeleo na si kuanzisha vijiwe vya kupiga domo na kuendeleza michezo ya pool, kuanzia asubuhi bila kujali muda wa kufanya kazi za uzalishaji.

Mrutu anasema sheria hiyo ifungue pia fursa ya Elimu ya Ujasirialimali, kwani ni muhimu sana kwa kuwajengea uwezo wa kufahamu umuhimu na changamoto zilizopo katika kujiwezesha kiuchumi, badala ya kusubiri kuwezeshwa.

Hata hivyo, Mrutu akiwa kama kiongozi katika kuziwezesha sekta binafsi katika kuweka mazingira bora ya kibiashara, hakusita kuishauri serikali kuwa katika mstari wa mbele katika kuwawezesha wananchi wake.

Aidha katika mdahalo huo, Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Taifa, anasema kuwa kuinua hali ya maisha ya Watanzania, ndilo jambo la msingi la Serikali tangu Uhuru mpaka sasa.

Rais Kikwete anasema kufanikisha malengo hayo, imekuwa ndiyo msingi wa sera na hatu mbalimbali zilizochukuliwa na kwa nyakati mbalimbali na kiini cha sera na hatua zote zilizochukuliwa ni kuwawezesha kiuchumi wananchi.

Katika harakati za kumuinua Mtanzania, serikali ilianzisha Africanization, Azimio la Arusha, Ujama Vijijini, Elimu ya Kujitegemea, Madaraka Mikoani, kuanzishwa kwa Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO), kuanzishwa kwa Vyama vya Ushirika na mambo mengi yaliyoanzishwa na kutekelezwa.

Amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana au kuletwa na sera na hatua mbalimbali zilizochukuliwa, yalitofautiana, lakini huwezi kutilia shaka au kuhoji dhamira yake ya kuwawezesha wananchi kiuchumi, kukiwa na nia ya kuhakikisha kuwa panakuwapo na mkakati wa kuwawezesha wananchi wenyewe kumiliki na kuendesha uchumi wa nchi yao .

Rais Kikwete anasema mwaka 2004, Serikali ilitunga sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na Novemba 2004 Sheria ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ilitungwa na Oktoba 2005 Baraza la Taifa la Uwezeshaji kiuchumi likaundwa.

Hata hivyo, anasema kuwa baraza hilo liliundwa katikati ya kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, kwa hiyo halikuweza kufanya shughuli yoyote ya maana mpaka Serikali mpya ilipoundwa.

Aidha, anasema katika kutekeleza sera hiyo, imetamkwa kuwa serikali itaendelea kuimarisha mifuko mbalimbali ya mikopo na kuboresha mazingira ya wananchi, kwa kutumia fursa zilizopo kujiendeleza kiuchumi.

Serikali inafanya hivyo, kupitia programu mbalimbali za mikopo na ujengaji uwezo. Katika kipindi hiki, serikali imekuwa ikiendelea kutekeleza sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Hivi kucheza Pool kuna athari gani na ubunifu na ufanisi?

Tanzania tunatumia masaa 12 kuzalisha kitu ambacho tunaweza kutumia masaa 4, kisha tunaona kutumia masaa 12 ni ufanisi? Mbona tunaongozwa na watu wenye akili za kiduwanzi na kijima namna hii?

Wastani wa mtu kuwa productive ni chini ya masaa 6, kama huko makazini hakuna anayepima uchapakazi kuna maana gani kuanza misako Rose garden kukamata wale wanaocheza pool na snooker kama si bao, drafti na domino?

Hivi kweli Mrutu anataka kutuambia Tanzania ambayo mhitimu wa UDASA hana kazi, leo itaanzisha sheria ya kusaka wasiofanya kazi? kazi gani? Je ni kulazimisha watu wawe wakulima au vibarua? kama hawataki, inawawasha nini serikali?

Kama serikali na mashirika yanashindwa kujiendesha kwa ufanisi kwa nini wasianze kuangalia miundo yao na uongozi na si kulaumu kina Invisible na Shy kwenda Rose Garden kula mchemsho?

Ikiwa wacheza Pool ni Machinga au waliojiajiri bado watakamatwa na askari wa TAMISEMI na kupelekwa Kibugumo?

Mbona hazungumzii uhujumu, ufisadi na uzembe wa viongozi kudumaza uchumi wa nchi?
 
Rev. Kishoka,
Kama sikosei ile sheria ya nguvu kazi si ndio iliyokuja kukusanya vijana mjini kama wazururaji?.. Je, mnakumbuka adha ya sheria ile au mimi ndo nimechanganya!..Utaweza vipi kurudisha sheria ile ikiwa hakuna ajira, wananchi wenyewe hawawezeshwi ktk kukopeshwa zana za kilimo, iwe ufugaji, uvuvi, ama kilimo chenyewe. Viwanda tupo at the low level ambayo haijawahi kutokea ukilinganisha na Population inayoweza kufanya kazi. Kifupi unemployment is at the highest level sasa hivi kuliko wkati wowote baada ya mashirika mengi kupunguza ama kufukuza watu kazi. Je,
Kuna mbinu gani serikali imejiandaa yenyewe kuhakikisha nafasi za ajira zimeongezwa na muhimu zaidi makosa yale hayatarudiwa!
 
Back
Top Bottom