Nguvu ya Umma yamtisha Wassira; akana kutaka kufuta CHADEMA!

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katika kile kinachoonekana kutuliza wananchi na upepo mbaya nchini kutokana na kauli yake ya kutishia kufuta CDM, jana waziri wa nchi ofisi ya Rais Stephen Wassira amekana kauli yake na kusema hana nia wala mpango wa kufuta CDM.

Amesema kauli yake aliyotoa alinukuliwa vibaya kwani ililenga vyama vyote na sio CDM pekee. Wassira amesema alichokuwa analenga ni umuhimu wa vyama vyote kufuata sheria lakini ameshtushwa na jinsi alivyoshambuliwa nchi nzima kwa kuhusisha matamshi yake na hujuma dhidi ya CDM.

Source: Mtanzania Jumapili
 
Huyu mzee anamatatizo ya ubongo mimi binafsi huwa napata shida sana coincide wa ccm wanavyo kimbia vivuli vyao mara wapokosea. Nilini wataamka na wasimamie minimal ya kauli zao?tofauti na hivyo jamii inatakiwa kuwadharau na kususia mikutano yao

Na wanasusiwa kweli kweli sasa hivi huko vijijini.
 
Kama ni kufuta vyama kutokana na kuvunja sheria then kwanini CCM bado ipo mpaka sasa?
 
Siyo kwamba amenukuliwa vibaya bali hana UBAVU wa kikifuta CDM
 
5dba16fa-27f8-1df8.jpg

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Katika kile kinachoonekana kutuliza wananchi na upepo mbaya nchini kutokana na kauli yake ya kutishia kufuta CDM, jana waziri wa nchi ofisi ya Rais Stephen Wassira amekana kauli yake na kusema hana nia wala mpango wa kufuta CDM.

Amesema kauli yake aliyotoa alinukuliwa vibaya kwani ililenga vyama vyote na sio CDM pekee. Wassira amesema alichokuwa analenga ni umuhimu wa vyama vyote kufuata sheria lakini ameshtushwa na jinsi alivyoshambuliwa nchi nzima kwa kuhusisha matamshi yake na hujuma dhidi ya CDM.

Source: Mtanzania Jumapili
Wassira anatakiwa asome hotuba ya Mubarak aliyoitoa mara tuu pale nguvu ya umma ilipoanza kushika kasi kwenye mitaa ya cairo. Alisema atawakamata wote wanaoandamana na kuwashikisha adabu na aliamuru jeshi lizime maandamano hayo mara moja.
Leo hii mubarak yuko wapi?
Kamwe usidharau nguvu ya umma, binadamu akichoka hata umtishe vipi utaondoka tu.
 
Mbona mnamuandama baba wa watu......tehe tehe teh teh....! Ni kwamba aliyaongea hayo wakati akiwa amelala.....!

Kibanga Msese
 
Bila kumkwaza mtu yoyote ningeshauri wana-JF tujikite kwenye hoja badala ya kujadili physical appearance ya mtu. Hata kama hukubaliani na Wassira sidhani kama ni vema kujadili sura/umbo lake. Hakuna mtu miongoni mwetu aliyemwambia Mungu amuumbe alivyo, na leo hii unaweza kupata ajali na sura/umbo lako likabadilika kabisa.

Ni vema tukajenga ustaarab wa kuhemu wengine regardless ya maumbo yao.
 
Huyu mzee anamatatizo ya ubongo mimi binafsi huwa napata shida sana coincide wa ccm wanavyo kimbia vivuli vyao mara wapokosea. Nilini wataamka na wasimamie minimal ya kauli zao?tofauti na hivyo jamii inatakiwa kuwadharau na kususia mikutano yao

Utakuta hata ahadi walizotoa baadae wanazikana na kusema tuliwanukuu vibaya.
 
Ni kuhusu kuwa Chadema kinaweza kufutwa
*Yasema anajenga uhasama kuliko uhusiano
*Yasisitiza hQakitakubali kufutwa, kitachukua hatua
*Wassira asema tamko lake halikulenaga Chadema

MWENYEKITI wa Baraza la Taifa la Vijana la Chama cha Demokrasi na Maendeleo (BAVICHA), John Heche amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uratibu na Uhusiano, Steven Wassira kuwa ni kiongozi anayejenga uhasama zaidi kuliko uhusiano. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Heche alisema Wassira alinukuliwa na vyombo vya habari hivi karibuni wilayani Bunda akitoa kauli ya vitisho ya kutaka CHADEMA kifutwe.

Alisema kutokana na kauli hiyo wanachama wa chama hicho kamwe hatawakubali kurudi nyuma na watachukua hatua kali zaidi kama kweli kuna mpango wa kufutwa.

"Hizi ni dalili za kuweweseka…namshangaa mzee Wassira na ukongwe wake wa siasa kutoa kauli kama hii, hakika nawaambieni CHADEMA haitarudi nyuma na vitisho vyake.

"Nina uhakika kauli ya Wassira haina uwezo wa kukifungia chama chetu…tutachukua hatua zote za kujilinda, hiki ni chama kikuu cha upinzani. Maneno haya yanaonyesha wazi waziri huyu amenaza kuweweseka kwa sababu anatambua tunataka kushika dola.

"Mzee Wassira, kama hataki kustaafu vizuri na kwa amani, basi asubiri tu mwaka 2015 vijana wa CHADEMA tunakuja kumstaafisha," alisema Heche.

Alisema pamoja chama hicho kuendelea kubanwa na vyombo vya dola kamwe hakitarudi nyuma kutetea haki za wananchi.

Akizungumza na Mtanzania Jumapili kwa simu jana, Waziri Wassira alikanusha kuwa anataka Chadema ifutwe.

Wassira alisema alichofanya ni kuwa alikuwa akijibu swali la wananchi waliohoji mwenendo wa Chadema na mstakabali wa amani ya nchi.

Alisema yeye aliwajibu kuwa ikiwa Chama kinakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa kwa kuhatarisha amani hakina budi kifutwe.

"Namshangaa sana huyo Heche … kwanza ni kijana mdogo anatakiwa ajue siasa ni kama mchezo wa mpira wa miguu lazima awepo msimamizi(referee).

"Kwa hiyo ukifanya madhambi unapewa onyo kwa kadi ya njano na ukizidisha inabidi ulimwe kadi nyekundu na huu ni ukweli kwa chama chochote kikionekana kwenda kinyume na sheria ya vyama vya siasa.

"Kwa hiyo mimi sikulenga moja kwa moja kuituhumu Chadema ifutwe ila nilikuwa najaribu kuwaelimisha wananchi walioniuliza swali hilo na ukweli juu Sheria ya Vyama vya Siasa," alisema Wassira.

Wakati huohuo, Heche akizungumia msimamo wa chama chake juu ya kutokuwa na imani na tume iliyoundwa kuchunguza mauaji ya kijana Ally Zona yaliyotokea mkoani Morogoro, Heche alisema kamwe hakitakubaliana nayo.
Alisema kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi wa mwili wa marehemu Zona, chanzo cha kifo chake ni jeraha lililotokana na kupigwa na kitu kilichokuwa katika mwendo wa kupaa (risasi au bomu la machozi). 2
heche.jpg

Mzee wazira ana busara sana vingenevyo angeshakifutilia mbali chadema busara na uvumilivu wa serikali ndo vinaiacha chadema kwa nchi nyingine chama cha chadema kingefutiliwa mbali na kupigwa marufuku
 
Wakuu msimshangae kuona Mh Wasira akikataa hoja yake, "LABDA ALISEMA AKIWA USINGIZINI" baada ya kuamka amesahau
 
Wassira anatakiwa asome hotuba ya Mubarak aliyoitoa mara tuu pale nguvu ya umma ilipoanza kushika kasi kwenye mitaa ya cairo. Alisema atawakamata wote wanaoandamana na kuwashikisha adabu na aliamuru jeshi lizime maandamano hayo mara moja.
Leo hii mubarak yuko wapi?
Kamwe usidharau nguvu ya umma, binadamu akichoka hata umtishe vipi utaondoka tu.
Naona anaumwa ugonjwa wa kusahausahau ndiyo maana keshasahau kilichotokea majuzi pale Moro ambapo licha ya kuua na kujeruhi wananchi walijitokeza kwa maelfu kuupata ujumbe wa ukombozi. Hakuna nguvu
chini ya jua inayoweza kuzuia nguvu za umma katika harakati za
ukombozi. Binafsi nawaonea huruma CCM kwa kufanya kazi ya
kuitangaza CHADEMA na kukiua chama chao bila malipo. Matumizi yao
ya Jeshi la polisi kuwanyanyasa wananchi kama walivyokuwa wakifanya makaburu yameipandisha chati CHADEMA, ila wakumbuke kwamba watawajibika kulipia kila nukta ya uhaini waliolitendea taifa hili.
 
Back
Top Bottom