Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
na wewe prove kama hawana ugomvi binafsi
Majibu yako haya hapa chini. Hii ni makala moja mnayoilalamikia, na mdau kaamua kuprove ukweli wa hoja za Ngurumo.
Hebu tuangalia mambo mengi aliyosema Ngurumo kama yana uongo, tutajua:
"Chuki ya wazi dhidi ya CCM inasababishwa na maisha magumu waliyonayo wananchi. Udhaifu wa serikali ndio umekiua CCM, maana kimegeuka chama cha viongozi waongo, wasioaminika." TRUE KABISA!
"Ile jeuri ya wanachama na mashabiki wa CCM kutembea kifua mbele wakiwa wamevaa mashati na fulana na kijani na njano mitaani, imenyauka." TRUE KABISA, mfano ni baba yangu mzazi, japo ccm siku hizi hata Tshirt ya kijani ukimnunulia havai!
"Hii ndiyo sababu inayowafanya CCM kuandaa mikutano ya hadhara kwa gharama kubwa mno, ikuhusisha kubeba wananchi kwenye malori na mabasi kutoka sehemu za mbali na kuwaleta mahali pa mkutano, tena baada ya kuwaahidi au kuwagawia pesa au fadhila nyinginezo." TRUE KABISA! imekuwa jadi! hadi kuhudhuria kwenye mikutano ya shina, tawi au kata wanadai posho!
"Sasa hivi hata watoto wadogo wanasalimiana kwa kunyosha vidole viwili, ishara ya ushindi inayotumiwa CHADEMA" hili halina ubishi, nenda hata mtaania ukutane na uangalie watoto wanaocheza uangalia wangapi utasikia wakisema kidumu, ila utasikia salam ya peoplez!
"Sasa hivi hata watoto wadogo wanasalimiana kwa kunyosha vidole viwili, ishara ya ushindi inayotumiwa CHADEMA" hili halina ubishi, nenda mtaani maeneo wanakocheza watoto uone kama utasikia hata mmoja wao akitamka kidumu chama … na uangalie kama utasikia salaam au alama ya peoplez!
"Shule za sekondari na vyuo vya elimu ya kati na ya juu vimejaa wanafunzi wasiokipenda CCM. Katika mazingira haya, CCM kinazidi kukosa mvuto, na wanachama wa CCM wanazidi kupungua." Hili hata kwenye report yao ya kujivua gamba, waliweka kama kiashiria cha kushuka hadhi mbele ya umma!
"Ni miaka sita ya shida na umaskini unaosababisha chuki ya wananchi dhidi ya Rais Kikwete. Hatujasahau kwamba mwaka 2005 Kikwete aliomba kura akiahidi maisha bora kwa kila Mtanzania. Yako wapi? " TRUE KABISA maana hata ile kauli mbiu yao ya ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya bila fikra mpya na dira mpya, nayo imekufa kibudu kama ahadi ya maisha bora yenyewe! sasa kwa hili Ngurumo karudia tu mambo ambayo yako wazi, hata anaetumia masaburi kufikiri, na mtumwa wa kuchumia tumbo atayaona!
Ukweli uliowazi ni kuwa ccm imekuwa a disappointment! Imewalet watz down siku ilipoamua kuwatelekeza wakulima na wafanya kazi na kukumbatia matajiri! Hata mwalimu alisema siku ikiacha misingi ya kuanzishwa kwake, basi itakufa! Ndio maana wao wenyewe wanakiri hadhi ya ccm imeporomoka na wakaja na usanii wa kujivua gamba, ambalo sasa limegoma!
Sasa na wewe prove kwamba wana ugomvi binafsi.