Ngono yazidi kutawala Dar!

Hemed Maronda

Senior Member
Oct 27, 2010
138
43
Ni jambo la kusikitisha kidogo lakini ndiyo ukweli wenyewe.
Leo asubuhi nimetoka Bagamoyo kuelekea Jijini,nikiwa kwenye shughuli zangu za kawaida za kibiashara,baada ya kuona nimeshindwa kumaliza shughuli zangu kwa leo nikaamua kulala. Jambo nililokutana nalo ndilo limenilazimu kuleta uzi huu angalau na wenzangu muchangie.
Nimezunguka Mbagala - Zakhieem ili nipate Guest House nipumzike,cha ajabu nilichokutana nacho! Nimetembelea Guest House 10 zote nakuta vibao pale nje vinanielekeza kuwa Vyumba Vipo lakini nikiingia ndani na kuwaona Wahudumu naambiwa kuwa hakuna Chumba kwa Mgeni anaetaka kulala,ila kuna vyumba kwa wale wanaohitaji huduma ya muda mfupi ama "short time" mwanzo sikuamini nilichokuwa naambiwa ila kila nikiondoka kutoka Guest moja mpaka nyingine bado majibu niliyokuwa nayapata ni hayohayo. Nilizidi kuwa mdadisi nifahamu nini kilichojiri mpaka kupelekea hali hii? Bahati nzuri wakati naifikia Guest House ya 11 nikamkuta dada mmoja ambae ni Mhudumu kwenye Guest hiyo,nikamuuliza kulikoni nimekosa chumba cha kulala kwenye Guest 10 pamoja na hiyo ambayo nilikuwapo? Yule dada hakuwa na hiyana akaanza kunipa maelekezo kwa nini kuna hali kama hiyo,alichonieleza kuwa toka pale DAR LIVE ilipofunguliwa pale Mbagala - Zakhiem mauzo ya Guest zote ambazo ziko karibu na Dar Live yameongezeka tena hasa hasa siku za Jumamosi na Jumapili,tena si kwa wateja wa kulala bali wateja wa "short time" ambao kwa chumba kimoja tu wanaweza kutumia mpaka watu 10 kwa siku na kila matumizi ya mara moja gharama ni Tshs 5,000/= sasa wamiliki wa Guest wanaona ni heri siku za wikiendi wafanye biashara za muda mfupi kuliko kumpa chumba mtu wa kulala,jambo ambalo siyo sahihi ni kinyume na madhumuni ya kutolewa Leseni za biashara hiyo,pia tujiulize kuna ngono salama inayoendelea huko ndani?
Nawasilisha wadau tujadili.
 
Ngono ni starehe isiyobagua kwa maskini na tajiri..............So sad lakini ndiyo hivyo tena
 
ulikuwa hujui, na wewe karibu raia milioni 40 wanandgu dar wewe guest ulifata nini, na istoshe, guest ni sehemu chafu, magodoro, mito, mashuka wewe ulitaka upige usingizi juu ya utoko wa watu? tafakari, hii ni dunia nzima,

san sana uendage louge, au hotel, bei ni kwenye 30alfu tu. kaka. achana na madanguro,
 
Ngono ni starehe isiyobagua kwa maskini na tajiri..............So sad lakini ndiyo hivyo tena
Ila Mkuu Platozoom hatukatai basi watengewe eneo maalum kama kwenye Madanguro na si kugeuza Nyumba za kulala Wageni kuwa Madanguro? Hivi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke inafahamu kuwa inaibiwa? Maana hao watu wa short time wahaandikishwi kwenye Rejesta ya Wageni ambayo inatumika kukokotoa Kodi wanazotakiwa kulipa wamiliki wa Guest House kwa Halmashauri husika.
 
Ndiyo maana watu kama siye tunasafiri na mataulo yetu
 
Pole mkubwa.

Wlichotakiwa kufanya ni kujenga sehemu kubwa kiasi kwamba wanaotaka kujinafasi kwa muda mfupi waweze na wanaotaka kulala waweze.

Kumkatalia mtu chumba kwa sababu anataka kulala na hali chumba kipo ni kuvunja mwiko wa biashara, kabla hata ya kuingia kwenye sheria huko.

Hivi ingekuwaje kama makondakta wa mabasi wangekuwa wanatuuliza mlangoni "wewe unakwenda wapi?" Ukimwambia unaenda Karioakoo anakupiga chini, anapakia wa kushukia njiani tu. Tungeelewana hapo?

Mamlaka husika inabidi zimulike hili. Watu wenye kazi zao wapelekwe wamevaa kiraia, waombe chumba, wakataliwe kwa majibu hayo ya kihuni, hapo hapo mtu anakamatwa na Guest House inapigwa bonge la faini. Wakifanya hivi mara nne tano watu wote wataogopa kuleta upuuzi huu.

Mfanyabiashara hakatai biashara yake. Labda hajajipanga vizuri huyo.
 
gest ya elfu tano??
Anyway, pole.
Mkuu hapana Guest House ambayo nimeshawahi kulala pale inaitwa Minazi na niliwahi lipia Chumba Tshs 20,000/= ila siku ambayo nilipata chumba mapema haikuwa siku ya Wikiendi nimeona mabadiriko siku ya leo baada ya kuambiwa leo biashara kubwa ni Short Time ambayo ndiyo inayowalipa sana!
 
Pole mkubwa.

Wlichotakiwa kufanya ni kujenga sehemu kubwa kiasi kwamba wanaotaka kujinafasi kwa muda mfupi waweze na wanaotaka kulala waweze.

Kumkatalia mtu chumba kwa sababu anataka kulala na hali chumba kipo ni kuvunja mwiko wa biashara, kabla hata ya kuingia kwenye sheria huko.

Hivi ingekuwaje kama makondakta wa mabasi wangekuwa wanatuuliza mlangoni "wewe unakwenda wapi?" Ukimwambia unaenda Karioakoo anakupiga chini, anapakia wa kushukia njiani tu. Tungeelewana hapo?

Mamlaka husika inabidi zimulike hili. Watu wenye kazi zao wapelekwe wamevaa kiraia, waombe chumba, wakataliwe kwa majibu hayo ya kihuni, hapo hapo mtu anakamatwa na Guest House inapigwa bonge la faini. Wakifanya hivi mara nne tano watu wote wataogopa kuleta upuuzi huu.

Mfanyabiashara hakatai biashara yake. Labda hajajipanga vizuri huyo.
Mkuu umenena sawa! Maana haki za watu zinapotea bure bila sababu kwa tamaaya Watu wachache wanaopenda kujinufaisha binafsi kwa kubadiri matumizi sahihi ya Guest House wakati wahusika wapo wanaosimamia sheria za nyumba za wageni
 
Kwanini umefikiria ngono tu? Wengine labda huwa wanaenda kufanya mazungumzo tu na kutoka.
 
Back
Top Bottom