Ngawaiya adai vurugu zinachochewa na wafadhili wa nje

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
BAADHI ya vurugu za kisiasa zinazotokea hapa nchini zimedaiwa kuchochewa na wafadhili wa nje kwa kutoa fedha nyingi.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utawala Bora na Maendeleo Tanzania (CEGODETA), Thomas Ngawaiya aliwataka wafadhili hao kuheshimu uamuzi wa Watanzania vinginevyo wanaweza kusababisha machafuko.

“Uchaguzi mkuu umekwisha na Watanzania wameshafanya uamuzi, tunawaomba wafadhili wa nje hususani wa Ulaya na Marekani, waache kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu ikiwa ni pamoja na kutuchagulia viongozi,” alisema.

Alitoa mwito kwa Serikali kuangalia namna ya kuchukua hatua kwa wageni wanaotoa fedha kwa ajili ya vurugu za kisiasa na washirika wao ili kulinda heshima na amani ya nchi.

Pia aliwataka Watanzania kuwa makini kwa kukataa kushawishiwa na watu hao wenye nia ovu ili kudumisha amani, utulivu, umoja na mshikamano kwa maslahi ya Taifa na vizazi vijavyo.

Kuhusu Polisi, alilitaka Jeshi hilo kutumia mbinu za kisasa wakati wa kuzuia maandamano na kuepuka kutumia nguvu kupita kiasi hali ambayo inasababisha mauaji kwa watu wasiokuwa na hatia.

Aidha mwanasiasa huyo ameishauri Serikali kutolipa deni la Kampuni ya Dowans kwa sababu si deni halali na endapo litalipwa linaweza kufilisi nchi na wananchi wakakosa huduma muhimu.

“Tanzania ingejiondoa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Biashara kwani Mahakama hiyo mara kwa mara hutoa hukumu mbaya dhidi ya nchi yetu kama ilivyofanya kwenye suala la IPTL ambapo hadi leo tunalipa zaidi ya Sh bilioni nne kila mwezi,” alisema Ngawaiya.
 
Muda wenu unahesabika mtamsingizia kila mtu, lakini ukweli utasimama tumewachoka nyie mbuzi.
 
Eti hata ka-Ngawaiya nayo ni mkurugenzi wa utawala Bora Tanzani, my foot!!! Kumbe ndio maana kila kitu ni BORA UTAWALA HIVI??
 
Ukiona mtu mzima sawa yake Kikwete, CCM na mlamba buti Ngawaiya wote wanalia HADHARANI MBELE YA WATU KWA JINA LA WAFADHILI wa Ulaya na Marekani basi ujue tayari mtu kabanwa KORODANI na kubakia tu kuminyaminya macho na kutoa sauti nyembamba kwa uchungu mkali mno.

Wananchi tukaze zaidi buti hapa.
 
Bado kitambo kidogo mtasema mimi ndo nasababisha maandamo na migomo Bongo!!!!!!!!!!
Haya ni matokeo ya ccm kugawa mali za nchi kwa muda mrefu bila kuwajali wananchi wake. Umaskini unaongezeka huku watu wakiona jinsi ambavyo kundi dogo linatanua kwa jasho la walala hoi! If the systemiwill not change we must expect more than this. Mchawi ni watawala wa ccm tangu MWingi alipouza Liliondo waliofuata wakaendelea kuuza kila kitu hapo ndipo ccm ilipojimaliza. MCHAWI NI CCM NA SERIKALI YAKE HAKUNA MFADHILI WA NJE WALA WA NDANI
 
huu uhuru wa kuongea kila mtu lazima atoe tamko hata kama la kwenye njozi naona tunasingizia yasiyokuwepo
 
huu uhuru wa kuongea kila mtu lazima atoe tamko hata kama la kwenye njozi naona tunasingizia yasiyokuwepo
tatizo ni la mkuu wa nchi mwenyewe yupo kimya mno wala haongei sijui hata kuna nini ndiyo maana kila mtu anaongea lake na kwa mtindo huu alioanza nao inaonyesha mwanzo mbaya hz ishu za downs na migomo,maandamano alitakiwa atoe tamko sasa hatuelewi sijui anaogopa
 
Hao wafadhili ni akina nani? Wataje kama huwataji basi kaa kimya maana tumeshajua mbinu yenu ya zamani sana ya kushift the blame.
 
Ngawaiya- Please KAA KIMYA! Huoni haya kuelezea matatizo yetu kwa kusingizia nyumba ya jirani! Kauli za namna hii nilizisikia kwako miaka ile ya sabini wakati unahamia Dar kutoka Iringa. Lo! Mpaka leo unazo!

Mustakabadhi wa taifa uko mikononi mwetu SIO kwa jirani! Ni mbayumbayu tu anayeweza kuendeshwa na taifa lingine! Zile hekima za JKNyerere alizokuwa anahubiria kuhusu kutofungamana na yeyote (non-alignment) hazikuweza kupenya hata kachembe ka bongo yako. Aibu Thomas.

Kwa taarifa yako, mataifa ya Ulaya na Magharibi wanaifaidi Tanzania iliyo tulivu na yenye viongozi wa YES SIR kuliko Tanzania yenye vuguvugu la mapinduzi, lenye watu wanaohoji kulikoni!
 
Ngawaiya angetuambia hao watu wanaofadhiliwa na wanafadhiliwa na wakina nani, na wameleta vurugu wapi ili tuweze kumuelewa. la sivyo ajue watanzania wa leo si wa miaka yake na kama alishindwa kuwatetea bas akae kimya wengi wapo nasi tutakuwa nyuma yao.
 
BAADHI ya vurugu za kisiasa zinazotokea hapa nchini zimedaiwa kuchochewa na wafadhili wa nje kwa kutoa fedha nyingi.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utawala Bora na Maendeleo Tanzania (CEGODETA), Thomas Ngawaiya aliwataka wafadhili hao kuheshimu uamuzi wa Watanzania vinginevyo wanaweza kusababisha machafuko.

"Uchaguzi mkuu umekwisha na Watanzania wameshafanya uamuzi, tunawaomba wafadhili wa nje hususani wa Ulaya na Marekani, waache kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu ikiwa ni pamoja na kutuchagulia viongozi," alisema.

Alitoa mwito kwa Serikali kuangalia namna ya kuchukua hatua kwa wageni wanaotoa fedha kwa ajili ya vurugu za kisiasa na washirika wao ili kulinda heshima na amani ya nchi.

Pia aliwataka Watanzania kuwa makini kwa kukataa kushawishiwa na watu hao wenye nia ovu ili kudumisha amani, utulivu, umoja na mshikamano kwa maslahi ya Taifa na vizazi vijavyo.

Kuhusu Polisi, alilitaka Jeshi hilo kutumia mbinu za kisasa wakati wa kuzuia maandamano na kuepuka kutumia nguvu kupita kiasi hali ambayo inasababisha mauaji kwa watu wasiokuwa na hatia.

Aidha mwanasiasa huyo ameishauri Serikali kutolipa deni la Kampuni ya Dowans kwa sababu si deni halali na endapo litalipwa linaweza kufilisi nchi na wananchi wakakosa huduma muhimu.

"Tanzania ingejiondoa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Biashara kwani Mahakama hiyo mara kwa mara hutoa hukumu mbaya dhidi ya nchi yetu kama ilivyofanya kwenye suala la IPTL ambapo hadi leo tunalipa zaidi ya Sh bilioni nne kila mwezi," alisema Ngawaiya.

Kwenye red
Yeye hajapata mgao? Kwa nini analalama wakati hizo fedha za wafadhili ndizo zinazomweka mjini vinginevyo angekuwa kijijini kuendeleza kilimo cha mibuni
 
Back
Top Bottom