News Alert: Kima kipya cha mishahara

Hivi wametumia kigezo gani kupanga kima hicho cha chini?

Kigezo kilichotumika hapa ni kuwa "taja figure yeyote tu ili kuonyesha kuwa mishahara imepanda kwani hakuna atakayefuatilia kuona kama hili linatekelezeka." Hii mishahara hailipiki kwa hao waliotajwa na hakuna atakayedai maana ukipiga kelele unaaambiwa acha kazi na wewe utaachaje kazi wakati sehemu ya kudokoa vitu (ili kujiongezea kipato) ni hapo kibaruani.
Mnao hoji bajeti gani itawezesha kiwango hiki kulipwa bila shaka mnaikosa pointi, hii ni kwa ajili ya sekita binafsi. Kama Kada Mpinzani kwenye baa yako utaweka wahudumu 20 ni wewe mwajiri ndio utajua pesa ya kuwalipa inatoka wapi na si serikali.
 
hivi ni mwajiri gani atakayekuwa tayari kuendelea kuajiri watu ishirini kwa malipo ya namna hiyo. Mwajiri mwenye akili atahakikisha anapunguza wafanyakazi na zile fedha za kuwalipwa wale zinaingizwa kwenye nyongeza ya mishahara ya wale waliosalia. Matokeo yake ni kuwa nyongeza hii ya mishahara itasababisha ukosefu wa ajira (unemployment). Zaidi ya yote kwa wale walioachishwa kazi itakuwa vigumu kupata kazi kwenye nafasi zile zile kwa malipo haya mapya na matokeo yake itabidi wafanya kazi chini ya uwezo wao au ajira za chini ya ujuzi wao..
 
masuala kwa mheshimiwa waziri

1) kumetumika vigezo gani kuweka vima hivyo ambavyo vinatofautiana kwenye kila sekta? ( kima cha chini kinakwenda na uzalishaji wa sekta?)

2) wameangaliaje suala la kuongeza mishahara kwa ghafla na upunguzwaji wa wafanyakazi maofisini?

3) atahakikisha vipi viwango hivi vinatekelezwa?

4) ana mpango gani kwa mishahara ya wafanyakazi wa serikalini?
 
Hii kwenye management wanaita postponement of agitation bse washajua watz wako na jazba na mambo ya msingi ya nchi yao sasa wanaanza kutupotezea concentration.
Inabidi tuwe makini as suala la buzwagi,BOT na mengineyo ni mpaka kieleweke ata kama kima cha chini kitakuwa billion
 
Ndugu watanzania wenzangu naomba kwa kweli tuache itikadi pembeni kwa hili "tukubaliane" na serikali. Jamani kiwango cha mishahara ya Tanzania sio cha kumfanya mtu aishi kabisa. mi naona kumlipa mtumishi wa ndani 65,000 Tshs ni halali kabisa hata kama angekuwa anakula na kulala kwa mwajiri jamani 65,000 ni kitu gani? wengi humu hiyo hela ukienda nayo Rose Garden au kwingineko haimalizi siku. Jamani huu umasikini ndo unawafanya hata watu wetu washindwe kufikiria. After all Hakuna mtu anayefanya kazi kama House Helper just imagine..anakufulia nguo, anakupikia, anakuogeshea watoto, anadeki nyumba na mambo mengine lukuki na usisahau ndo wa kwanza kuamka na wa mwisho kulala, lakini ndo analipwa peanut! Kweli hii ni dhambi kubwa. In otherwords hawezi kwenda nyumbani kwa sababu yuko on call 24 hours!

Mwanakijiji, nadhani umeenda mbali kwamba watu wakipandishiwa mishahara ajira zitakosekana, sikusoma uchumi lakini nadhani hii theory yako si ya kweli. Jiulize wabeba box huko ulaya na kwingineko wangekuwa hawathaminiwi kwa kazi za kulibeba hilo box ingekuwaje? Labda hapa tungesema serikali iboreshe maslahi ya watumishi wake kusudi na wao waweze kuwalipa watumishi wao wengine. Not the otherway around.

Na lazima tujua hawa mahouse helper toka vijijini wanokuja mjini wana familia zinazowategemea na ni watu kama wengine. Its a disgrace mtu kumlipa 10,000 kisa..eti anaishi na kula kwangu! Sina uwezo lakini ningekuwa advcate wa hawa watu...wananyonywa mnoo! na wasomi wa JF ndo hao wanasema kwamba wakipandishwa maslahi ajira zitakosekana! What a pity!

Serikali imefanya jambo jema (if it will ever be implemented anyway). Mambo kama haya ndo yanatufanya tuzidi kuwa masikini kwa sababu tunadharau kazi na zile kazi ngumu na za muhimu katika maisha yetu ndo hizo zinadharauliwa kama mwalimu, nesi, nk. Hatuwezi kuendelea bila kuwathamini hawa watu ndo walipa kodi na wanaoifanya nchi iendelee kuwa nchi kwa sababu wao wananyonywa hawasemi, elimu yao ni ya kati, hawana exposure ya ulaya na America kama wengi weu humu JF, hawana sehemu ya kulalamika wala kushtaki na ndilo group kuuubwa sana. Jamani hatuna budi kuanza kuwaunga mkono hawa watu. Uliye USA au Europe unamuona Karamagi na Balali kama mafisadi, lakini ukweli ni kwamba huyu mtumishi wa ndani ambaye unamlipa 10,000 na anategemewa na familia nzima kijijini, has nothing to do with Karamagi infact atakuelewa kama ukiwa na nia ya kumsaidia na yeye ajikomboe. Otherwise atajua ni wale wale wanaotaka kula so be it CCM, CUF, CHADEMA ni wale wale.

Umaskini ni kitu kibaya sana, unalemaza na unamfanya mtu ashindwe kufikira kabisa. No wonder viongozi wetu they take us for granted kwa sababu wanatujua.
 
KILIO cha wafanyakazi wa Sekta Binafsi ambacho kilikuwa kinataka waboreshewe Mishara sasa kimesikika na Serikali imeamua kutangaza mishara mipya ya kima cha chini iliyopanda kutoka shilingi 48,000 hadi 65000 kwa mfanyakazi w a ndani bila kujali kama ni kijijini au mjini na shili 350,000 wa migodini.

Serikali kupitia Wizara ya Ajira ,Kazi na Maendeleo ya vijana imefikia hatua hiyo baada ya Waziri John Chiligati kuunda Bodi zilizokuwa na wajumbe wawili kila pembe ,waajiri, wajiriwa na Serikali kufanya uchunguzi na kutoa matokeo yaliyotumika kupanga mishahara.

Akitangaza Mishara hiyo Mipya itakayoanza kulipwa Novemba Mosi Mwaka huu mbele ya Wandishi wa Habari Waziri Chiligati alisema kua anatumia kifungu namba 41 (1)cha sheria namba 7 ya mwaka 2004 ambacho kinampa mamlaka ya kutangaza mapendekezo ya Bodi aliyopokea ndani ya siku 60 tangu akabidhiwe mapendekezo hayo vingenevyo itabidi akajieleze Bungeni.

mapendekezo hayo aliyapokea 27 Septemba Mwaka huu takribani Siku 10, yaliyotplewa na bodi nane alizounda ambazo ni Sekta ya Majini, Bahari na nchi kavu,Majumabani na mahotelini, Kilimo, Madini,ulinzi binafsi,Biashara na viwanda, Afya na Usafiri,Mawasiliano, pia ameonya kwamba wajiri wasipandishe kodi katika vitegauchumi vyao ili kufidia gharama za mishara mipya watakayoanza kuwalipa wafanyakazi w ao.

Chiligati alisema katika uchunguzi bodi , zilibaini mapungufu yafuatayo ,karibu 15% ya wafanyakazi hawana mikata ya Ajira, sehemu nyingi za kazi hakuna mikataba ya hali bora ya kazi baina ya mwajiri na mfanyakazi, wafanyakazi w anafanyizwa kazi kwa saa nyingi bila kujali saa za kazi na ziada.

mazingira kiafya na usalama wa wafanyakazi katika baadhi ya sehemu nyingi za kazi hayaridhishi,
kuna baadhi ya waajiri hawajaandikisha wafanyakazi wao mifuko ya hifadhi ya Jamii,kama NSSF,PPF,n.k.

na wafanyakazi wanaoumia wakiwa kazini wanacheleweshewa au hawalipwi malipo ya fidia ya kuumia kazini (Workmen's Compensation)na baadhi hawalipwi.

Waziri Chiligati akiwa ameongozana na viongozi wa vyama mbalimbali vya wafanyakazi na waajiri akiwemo katibu wa shirikisho la wafanyakazi TUKTA,Nestory Ngulla, alisema;

"mapendekezo ya kima cha chini cha mshahara yaliyoletwa na Bodi za kisekta na ambayo karibu yote nimeyakubali ,ispokuwa mapendekezo ya sekta ya huduma za usafiri na mawasiliano , kila sekta itakuwa na kima chake cha chini cha mshahara kwa kuzinagatia hali ya uzalishaji" .

"kima cha chini cha mshahara kitatumika kwa wafanyakazi wote katika sekta husika bila kujali kama ni wafanyakazi wa mjini au vijijini kwa hiyo’

Wafanyakazi wa Kilimo wataanza kulipwa kima cha chini cha mshara shilingi 65000 kutoka 48000 na wafanyakazi wa Sekta ya Majini;Baharini na Ziwani katika Meli kubwa za kimataifa watatumia mkataba wa ILO wa Mwaka 2006.

lakini wale wa Meli za mizigo na abiria watalipwa 225,000 Meli za uvuvi wa Ndani shilingi 196000,Makuli na wajenzi wa meli 30,000.
Sekta nyingine ni ya wafanyakazi wa majumbani na mahotelini ambapo wa majumbani wamegawanywa katika makundi matatu wapo w anaowafanyia kazi wafanyabiashara wakubwa na mabalozi watakuwa wanalipwa kima cha chini cha mashahara 90,000 wale w anaowafanyia maafisa wanaolipiwa huduma hii na waajiri wao watalipwa 80,000 na wengineo watakuwa wanalipwa 65,000.

hata hivyo w aziri akizungumzia Sekta hii ya ndani alisema kuwa watumishi wa ndani wanaoishi na kupata huduma ya chakula ,malazi na nyinginezo kutoka kwa mwajiri atakatwa asilimia 68 ya mshahara wake kwa ajili ya malazi ambapo chakula 56% na 12% matumizi mengine.

kwa wale wa mahotelini watakuwa w analipwa kima cha chini shilingi 150,000 hoteli za kitalii na Maahoteli ya kati 100,000 na hoteli ndogondogo , mabaa ,nyumba za wageni na migahawa shilingi 80,000.

katika Sekita ya madini upande wa migodi mikubwa watakuwa wanalipwa shilingi 35,000 kima cha chini lakini waajiri wanaoshughulika na chumvi au chokaa wataingia kwenye kundi la viwanda vidogo kwa kuwa uwezo w ao ni mdogo ukilinganishwa na wa migodi ya madini yenye thamani kubwa.

Sekta ya Ulinzi binafsi Serikali imesema kuwa katika uchunguzi wake imegundua kuwa makampuni mengi yanawalipa wafanyakazi wao pesa kidogo au kuwacheleweshea mshahara wakati w amewapa silaha hali inayowafanya wajiingize kwenye vitendo vya ujambazim kutokana na hali hiyo wamiliki wa makampuni hayo wameonywa kama watashindwa kuwalipa kima kipya wafunge makampuni yao mapema.

kutokana na hali hiyo makampuni ya wakubwa na makampuni ya kigeni itakuwa shilingi 105,000 na makampuni mengeineyo 80,000 Sekta nyine ni biashara na viwanda ambapo ni pamoja na mabenki kima cha chini kitakuwa shilingi 150,000 na viwanda vidogo na biashara ndogo itakuwa shilingi 80,000.

sekta nyingine ni Afya amabapo imegawanywa katika makundi mawili kuna ,Hospitali kubwa na maduka mshara kima cha chini kitakuwa 120,000 kwa hospitali ndogo na zahanati kitakuwa 80,000.

Sekta nyinge ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu ni usafiri na mawasiliano ambapo kuna vyombo vya habari na daladala zinazowahusu wandishi na makondakta katika s ekta hii wafanyakazi wa huduma za anga kima cha chini watakuwa wanalipwa 350,000, wasafirishaji wa mizigo (Clearing and Forwarding) kima cha chini ni 230,000.

kwa wafanyakazi wanaofanya katika mitandao mbalimbali ya mawasiliano ya simu (Telcom)shilingi 300,000 wengine niusafiri wa nchi kavu (Makondakta) kima c ha chini kitakuwa shili.20,0000.

katika vyombo vya habari waziri Chiligati alisema Vipo vya aina mbili vya kibiashara ambavyo kima cha kumlipa Mwandishi kitakuwa Shilingi 250,000 na kwa vile vya kidini ambavyo huwa vinatoa matangazo ya Dini kima cha chini kitakuwa 150,000, hata hivyo Chiligati amesema kima hiki hakimzuii mwajili kupandisha mshahara isipokuwa kinambana asilipe chini ya hapo.

kwa upande w a vibarua ambao hawajaajiriwa wsaajiri wametakiwa kugawanya mashahara wa kima cha chini katika siku 30 hiyo ndio itakuwa malipo ya kibarua kwa kutwa aidha kaWaziri Chiligati alisema kuwa nyongeza hii ya mishahara isiwe chanzo cha waajiri kupandisha bei ya bidhaa kwani kwa kufanya hivyo ni kuwaumiza w afanyakazi wao.

"Kwa mjibu wa tangazo (Wage Order) litakalotolewa katika gazeti la Serikali (GN)Viwango vipya vitaanza kutumika kuanzia Mwezi Novemba mwaka huu, tangazo hilo mara litakapotolewa kila mwajiri anatakiwa kulipa viwango vipya ,kinyume chake ni kukiuka kifungu namba 41(1)cha sheria na 7ya Mwaka 2004 na kwahiyo hatua kalizitachukuliwa dhidi ya mmwajiri yeyote atakatelipa mishahara chini ya viwango vilivyowekwa kwa mjibu w a sheria"alisema waziri.


Naye Hellen Ngoromera anaripoti kuwa

Akizungumza baadaye kuhusu tamko hilo la serikali, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA), Nestory Ngulla, alisema TUCTA imeyapokea maamuzi hayo.

Awali kabla ya tamko hilo la serikali, Shirikisho hilo la wafanyakazi liliitaka serikali kuongeza mshahara wa kima cha chini na kuwa sh. 315,000.

Pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa pamoja na tamko hilo, TUCTA itatafakari na kuona ni namna gani itafanya kuhusiana na suala hilo.

“Tumeyapokea haya… ingawa kiwango hicho cha mishahara kilichotangazwa hakijafikia kiwango tulichokitaka TUCTA inaona kuwa huo ni mwanzo mzuri

Hiyo siyo kazi ndogo, kiwango cha mishahara kilikuwa chini mno, toka sh. 35,000 hadi sh. 65,000, kwa kuwa mshahara mpya unatakiwa kuanza kulipwa Novemba mosi nasi kama shirikisho tutatumia nafasi kuanzia leo(jana) kuona tunafanyaje,”. Alisema Katibu Mkuu huyo.

Sakata la TUCTA kuidai serikali kima cha chini cha mishahara lilianza miezi michache iliyopita jambo lililosababisha shirikisho hilo kufanya mgomo ikiwa serikali haitatekeleza ahadi yao.

Hatua hiyo ililifanya shirikisho hilo kuipa serikali mwezi mmoja kushughulikia suala lao. Hata hivyo baadaye serikali ililifanyia kazi suala hilo na kuunda kamati ndogo kufuatilia suala hilo ambalo ndilo lilikamilisha kazi yake na kuifanya serikali kutolea majibu suala hilo jana.
 
Safi sana

Acha kutuzingua wewee, unafukua mada za mwaka arobaini na saba unachangia kama current issues. Nimekucheki umechangia na mada ya toka 2009 kuhusu mwakyembe wakati unajua wazi hayupo nchini hivi sasa
 
Acha kutuzingua wewee, unafukua mada za mwaka arobaini na saba unachangia kama current issues. Nimekucheki umechangia na mada ya toka 2009 kuhusu mwakyembe wakati unajua wazi hayupo nchini hivi sasa

Hahahahaha! Jamaa ni MSENGEnyaji huyu!
 
Back
Top Bottom