New gold zone found in Tanzania

Asante Nyerere kwa kututunzia rasilimali hizo. Ungeamua kuwa FISADI ungeweza kujinufaisha pekee yako. Ninawalaumu viongozi wetu wa sasa kwa kufanya rasilimali za watanzania ni mali ya wageni na wala nchi. Kugundulika kwa dhahabu hii hakuna faida kwa watanzania. Je Watanzania wanafaidika nini na machimbo ya dhahabu yanayochimbwa sasa?.
Basi tushirikiane kuilinda rasilimali hizi ili ziwe na manufaa kwa watanzania wote.
 
Hao wanafanya exploration, na hiyo ni stage ya mwanzoni katika mtiririko mzima wa kutafuta body imekaa wapi.

Unaweza kupata soil anomaly mahala fulani lakini isiwe true representative ya mahala hapo. Kuna kitu kinakuwa insitu na vingine ni transported.

Ni mapema mno ku-comment na kuanza kuwaangalia mafisadi hapo. Ila ki-ukweli ni kwamba jamaa wanastahili sifa kwa kuweza kupata matokeo hayo.
This is good news to us and to the nation. Tahadhari watanzania wenzangu tusianze kutoana macho kama wenzetu wa pemba waliosema wanataka kuchimba mafuta hata kama hayapo kitakachopatikana ni hicho.
 
Tunashindwa kupambanua hoja ndogo tu kama ya Dr MWakyembe kusajili kampuni ya kufua umeme na kisha yeye kuwa katika kamati ya kuchunguza Kampuni hewa ya Richmond kuwa haileti Conflict of Interest;
Kwa sababu kwanza unachunguza kampuni isyokuwepo.
Pili hakuna hoja ya msingi inayodhihirisha wazi kwamba kulikuwa na uonevu, uongo, husuda na upishi wa ushahidi katika shughuli nzima ya uchunguzi uliopelekea bunge, Wabunge na wananchi kujiuliza maswali yasiyo na majibu.
hakuna mtu aliyejitokeza na kudai yeye ni mmiliki wa Richmond au kuonyesha uchungu juu ya Richmond ukiacha gazeti la Mtanzania na mtu anayejulikana kama Rostam Aziz.

Hili dogo kabisa linatufanya kwa kudhamiria tukune vichwa kwa ugumu wake, ni kweli sisi WaTZ tutaweza andika mkataba wa maana wa kuchimba madini??

Iwapo viongozi ni sehemu yetu sisi wananchi sioni kwa nini wasitokee viongozi wanaoshindwa kujua zuri na baya la kuingiza ndani ya mkataba.
Tatizo siyo wageni kuja kuchimba dhahabu au uwepo wa dhahabu nchini Tanzania, tatizo ni wembamba wa upeo wetu wa kutambua mali na jalala au kugeuza jalala kuwa mali.

Mikataba mibovu si aibu ya viongozi wetu pekee yao ni aibu ya taifa zima, kwa sababu sasa hivi kuandika mkataba wa kishetani au kutetea mkataba wa kishetani kwa nguvu zetu zote huku povu likitoka vinywani mwetu ni sehemu ya utamaduni wetu Watanzania ni jambo linalokuwa na kawaida na linalo shabihiana na maisha yetu ya kila siku kama lugha ya Kiswahili, kila Mtanzania anaiongea.
 
Ni mapema mno kuongelea suala la mkataba. kwa soil results ni vigumu kujua kama watapata kiasi cha kutosha kufungua mgodi au la. waki-drill na kufanya resource estimation ndipo tutajua kuna mali ama la.

Nakubaliana na wewe Mkuu, Lakini Nyota njema huonekana asubuhi. Ukweli ni kwamba Tanzania iko very rich in Mineral Resources na kuna maeneo mengi sana ambayo bado hayajafanyiwa exploration. Hivyo basi ni vizuri tukaweka mazingina mazuri kabla ya kufikia kwenye hizo stage za Resource Drilling na Resource Estimation. Ukiangalia mfano mzuri ni Buzwagi, Deposit ilipatikana siku nyingi sana ikiwa chini ya Anglo America lakini tumekuja kuingia mkenge miaka ya hivi karibuni.
 
Back
Top Bottom