Neno "samahani" lina nguvu ya ajabu

Moto wa volcano

JF-Expert Member
Jun 3, 2018
726
1,850
Neno samahani ni fupi lakini linauzito na nguvu ya ajabu linapotumika, samahani inaweza ikaokoa mahusiano yako, samahani inaweza ikalinda urafiki wako / undugu wako, samahani inaweza ikalinda ajira yako, samahani inatuliza machukizo makubwa, sisemi uwe zoba ila tambua hata wewe ni binadamu kuna wakati unakosea, unapoteleza jishushe kwa uliowakosea, kiburi na majivuno ni chukizo mbele za Mungu.
 
HAKUNA kitu!! Kuna mengine hayaishi kiwepeisi ivo!!

Embu fikiri mtu anamla mkeo then hao wasaliti just easy tu samahani
 
HAKUNA kitu!! Kuna mengine hayaishi kiwepeisi ivo!!

Embu fikiri mtu anamla mkeo then hao wasaliti just easy tu samahani
Kwanini mfano wako ume base kwenye kumla , kk elewa mada kwa mapana inafundisha mtu unapokosea kujishusha na kukubali makosa ni somo la unyenyekevu
 
Back
Top Bottom