Neno La Leo: Mchwa Anapokaribia Kufa Huota Mbawa

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,


Kuna tuliomsoma mwanafasihi Shaaban Robert. Kuna mahali kwenye kitabu chake ‘ Nchi Ya Kusadikika’ Shabaan Robert anamwelezea mchwa anayekaribia kufa.


Kwamba huota mbawa. Hukiacha kichuguu . Yumkini ataruka juu sana. Atakwenda mbali. Lakini, huko angani hufika mahali, mbawa hupukutika. Mchwa ataanguka chini. Mbali na kichuguu.


Hapo, mchwa hukabiriwa na hatari kubwa. Hawezi kuruka tena, na yu mbali na kichuguu. Na kichuguu ni taasisi. Hivyo, mchwa anaweza kuliwa na kinyonga, au hata chura. Na akinusurika na wawili hao, aweza kukanyagwa na unyayo wa mwanadamu, au hata tairi la baiskeli. Mchwa atakufa.


Naam, mengine tuyafanyayo hupelekea maanguko yetu. Hata kama mwanzoni huonekana kutupaisha juu angani.


” Nafikiri, ndio maana naishi”- Anasema mwanafalsafa Rene Descartes.


Na maarifa ya Sayansi yanatusaidia kuyabaini mahusiano kati ya dunia tunayoishi na mazingira yanayotuzunguka. Hiyo ni falsafa ya kivitendo. Ndio iliyo bora kuliko ile dhanifu- Speculative.


Iweje basi tumekuwa ni watu wa kuishi kwa dhania na hata kusambaza uvumi?


Ngoja nijiandae kwa safari yangu ya Iringa kesho alfajiri.

Usiku mwema.
Maggid
Msamvu, Morogoro.
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
 
Nakutakia safari njema,salimia huko Iringa. Lakini hii stori ya mchwa,nadhani unawazungumzia jamaa wa magamba. Sasa sijui huyo mchwa ni Sitta ama Mwakyembe?!
 
mchwa ni wale wote mnaokurupuka na kutangaza vifo vya binadamu wenzenu as if mmekuwa makatibu muhutasi wa mwenyezi mungu, acheni maneno ya udhushi hasa kwenye ishu za vifo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom