Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo katika kata 37 za Tanzania bara zilizopo katika halmashauri 27 nchini, ikieleza kuwa uchaguzi huo utafanyika Oktoba 13, 2018.
Akitangaza uchaguzi huo leo Alhamisi Septemba 13, 2018, mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema fomu za uteuzi wa wagombea katika uchaguzi huo zitatolewa kati ya Septemba 15 hadi 21, 2018.
Amesema uteuzi wa wagombea utafanyika Septemba 21, 2018 na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 12.
Amebainisha kuwa uchaguzi huo unafanyika baada ya NEC kupokea taarifa ya uwepo wa nafasi wazi za udiwani.
Wakati huo huo, NEC imewateua madiwani watatu wa Viti Maalum kujaza nafasi zilizo wazi.
Jaji Kaijage amewataja madiwani hao kuwa ni Halima Kisenga (CCM) katika halmashauir ya wilaya ya Kigamboni.
Emmy Shemweta kupitia CCM katika halmashauri ya Wilaya ya Lushoto na Nuru Mwalimu Chuma (CUF) katika halmashauri ya manispaa ya Ilala.