Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Kama umesoma Mwananchi Jumapili ya leo ukurasa wa 4 JK anaonekana akisalimiana na watoto wadogo chini ya miaka kumi hivi kwenye kampeni zake. Watoto hao wadogo hawajafikisha umri wa kupiga kura na siyo sahihi hata kidogo kuwatumikisha watoto wadogo kwenye shughuli yoyote ile hususani hii yenye mtaji wa kisiasa kwa mgombea.
Sheria ya ajira inayokataza watoto kutumikishwa kazi JK ameikiuka kikamilifu na bado anataka awe au aendelee kuwa Raisi wetu na huku anazibeza sheria za Nchi ambazo yeye mwenyewe alizisaini..............Kuhudhuria shughuli za kampeni hizi kwa watoto ambao wazazi wao wanajua wapo shuleni wakisoma kumbe siku hiyo wamechukiuliwa mkuku-mkuku kwenda kujaziliza kadamnasi ya watu baada ya viongozi wa CCM kuona mgombea wananchi wamemkataa na ukiukwaji wa maadili wa hali ya juu.
Watoto hao angalau basi walipaswa kuandamana na wazazi wao vinginevyo NEC imkaripie huyu bosi wa CCM proper