Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Cuf limesikitishwa na hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kujidhalilisha na kujishushia hadhi kwa kushiriki katika hujuma za Dola dhidi ya CUF.
Mbali na kasoro kadhaa, hata kama ingekuwa kufukuzwa Wabunge hao wa CUF kulikuwa ni halali na kumefanywa na chombo halali cha Chama, basi Kanuni walizojiwekea wenyewe Tume katika uteuzi wa watu wa kujaza nafasi hizo huo unafuata mpangilio wa majina kama ulivyokuwa umewasilishwa na Chama husika wakati wa uteuzi wa wagombea wa ubunge wa viti maalum wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.
CUF ilipeleka orodha yake ambayo haihusishi majina yaliyotangazwa. Hivyo ndiyo kusema hata kama hicho kinachoitwa kufukuzwa uanachama Wabunge hao kingekuwa halali (jambo ambalo si halali), basi kwa Kanuni za Tume yenyewe, watu wa kujaza nafasi hizo wasingekuwa hao waliotangazwa.
Kwa maelezo haya, Baraza Kuu linaweka bayana kuwa kitendo kilichofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kimezidi kuidhalilisha na kuishushia hadhi Tume hiyo na kwamba kwa kushiriki kwake katika hujuma hizi chafu ni ushahidi mwengine kwamba Tanzania hatuna Tume huru ya Uchaguzi.