Ndugu zangu ambao Hatujafunga mfungo wa Ramadhan/Kwaresma tunapaswa kuishi kwa Tahadhari kubwa sana

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
4,138
10,540
Nimesikitishwa sana na kitendo cha kijana Hassan kumchoma kisu mwenzake kisa kamuomba maji ya Kunywa.

Ndugu zetu mlioko katika mifungo, mbona mna makasiriko sana kipindi hiki cha mwezi wa toba?

Nashangaa sana kuona mtu akasirika kisa mwenzie anakula.. mnahukumu vipi wakati nyie si Waumbaji?

by the way, ambao mnajua hamjafunga, mchukue tahadhari sana maana wameanza kutuua kwa sababu zisizo na msingi

Ni hayo tu
 
Hao walikuwa na uadui mwingine hilo la kuomba maji ni kisingizio tu.
 
Nimesikitishwa sana na kitendo cha kijana Hassan kumchoma kisu mwenzake kisa kamuomba maji ya Kunywa.

Ndugu zetu mlioko katika mifungo, mbona mna makasiriko sana kipindi hiki cha mwezi wa toba?

Nashangaa sana kuona mtu akasirika kisa mwenzie anakula.. mnahukumu vipi wakati nyie si Waumbaji?

by the way, ambao mnajua hamjafunga, mchukue tahadhari sana maana wameanza kutuua kwa sababu zisizo na msingi

Ni hayo tu
Yaani ilikuwa...
Amir: Naomba maji
Hassan: Kisu cha shingo
 
Mimi nimesikitishwa na wewe, kwamba aliyefanya kosa ni Hassan, iweje uwajumuishe wafungaji wengine wote kwamba eti "wana makasiriko sana kipindi hiki cha toba?" Kosa afanye Hassan iweje uwahukumu wengine?

" .....wameanza kutuuua kwasababu zisizo na msingi", yaani huyu Hassan mmoja wamekuwa wengi hadi waje 'wakuue wewe??! Jifunze kutenganisha kosa lifanyalo na mtu mmoja isiwe ndio kosa lifanyalo na wengi. Huwatendei haki, labda kama una hoja nyingine iliyojifica.
 
Back
Top Bottom