Ndoa sasa zimekosa thamani kwa hali hii

muudy

Senior Member
May 25, 2013
156
22
Habari zenu wanajf?? karibuni tujadili hili maana mwenyew napatwa na mashaka kidogo had nafikia kusema bora uwe upo upo tu kuliko kuingia kwenye ndoa!!

ok turudi kwenye mada yenyewe ni hivi kama kawaida yangu huwa nikiendaga dukani kununua T-shirt au suruali hupenda kumpelekea fundi wangu hapa hapa tu mtaani kuzitengeneza zi fitt na body
Sasa cku nikiwa nipo na fundi namsubiria huku tunapiga story mbili tatu huyu fundi akaniambia anateswa sana na mapenzi nikamuuliza kwa sababu gani? akaniambia tatizo ni kuwa mpenzi wake anam cheat na anatembea na jamaa wa hapa hapa tu mtaani akanitajia na jina la huyo jamaa
Sasa nikamuambia si ungemuoa huyo binti kama umempenda akaniambia kuwa ni mke wa mtu na mumewe yupo ila mtu wa mishe mishe may b ata akiingia ndani usiku kwa hiyo huyo mwanamke ana uhuru wa kutosha tu
Sasa mwenyewe nikajiuliza hivi kumbe ww umeoa lakini unatembea na mke wa watu ila unaumia mke wa watu unayetembea nae akitembea na jamaa mwengine
Hapo ndio nime realize kuwa sasa hakuna heshima tena kwenye ndoa hasa kimtazamo wangu nahisi wanawake wamezidi kuchepuka
Vp kwa mtazamo wenu mnahisi ni wepi wachepukaji zaidi kaina ya Waume na Wake??

My take: Kwa hali hii bora niwe nipo nipo kwanza kwani hata akiibiwa mtu tu naona kama naibiwa mm
Ahsanteni....!!
 
Ndoa hazifanani. Cha muhimu jenga yako katika kuheshimiana, uaminifu na mapenzi ya dhati. Tangu nimeolewa yapata miaka sita sasa sijawahi kuchepuka na mume wangu huwa ni mtu wa safari kwa sana. Nampenda na namuamini na naamini nilivyo hivi na yeye yuko hivyo hivyo yaani mwaminifu. Pia namtanguliza Mungu katika yote.
 
"Hakuna ndoa isiyo na matatizo" sentensi hii ina maneno matano, lakini ukianza kuichambua unaweza kuandika kitabu cha kurasa zaidi ya buku. Ukitaka furaha yako ya maisha iishe, oa au olewa.
 
Umesema wanawake wamezidi kuchepuka. Hivi hao wanawake wanachepuka na kina nani? Uchepukaji hauna jinsia
 
uwe makini mkuu isije ikawa na wewe upo kwenye chain bila kifahamu.
 
"Hakuna ndoa isiyo na matatizo" sentensi hii ina maneno matano, lakini ukianza kuichambua unaweza kuandika kitabu cha kurasa zaidi ya buku. Ukitaka furaha yako ya maisha iishe, oa au olewa.

Mkuu mbona umemaliza kwa kututisha?.."Ukitaka furaha yako ya maisha iishe, oa au olewa"..
Wataka kusema ndoa humaliza na kuondoa furaha kabisa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom