Ndoa inaweza kukuletea maadui ama marafiki wengi sana;jiandae kwa hili

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,150
Sasa nakufikirisha hivi vitu vikusaidie, inawezekana kabisa hujafikia umri wa kuoa au kuolewa, lakini ninakuambia weka maombi yako ya akiba, (sijui kwa upande wako, lakini mara nyingine huwa nawaombea watoto wangu maombi ya akiba, kwa ajili ya ndoa zao kama Yesu atakuwa hajarudi, kwa sababu najua maana yake ni nini).
Ni vizuri upate maombi ya namna hii mara kwa mara - ujiombee mwenyewe, ukipata watu wa kukuombea shukuru Mungu, lakini hata kama hujapata watu wa kukuombea, ninakuambia kazana kujiwekea maombi ya akiba. Hiyo ni njia panda. Mahali pa kuoa au kuolewa ni njia panda. Ukichagua njia ambayo haiko sawasawa, maisha yako yatakuwa magumu sana.
Sasa ukiangalia kwenye kitabu cha Hesabu.12:1-2 inatuonesha wazi kabisa ya kwamba, harusi ya Musa ilileta ugomvi katikati yake na ndugu zake, hasa dada yake na Haruni. Kilichowasumbua ni kwamba alikwenda kuoa mwanamke Mkushi; au amekwenda kuoa mahali ambako hawakutarajia, kwa hiyo wakakasirika. Halafu naamini Musa aliwaambia Mungu amesema naye juu ya kuoa mke huyu, wale watu wakasema, ‘Mungu anasema na Musa tu peke yake, haiwezekani’ - ugomvi ukaingia.
Unajua ugomvi uliingia kiasi ambacho Mungu akasikia yale maneno na hayakumfurahisha, akawaita kwenye hema. Ikabidi ajieleze wazi uhusiano wake na Musa.
Kitabu cha Hesabu 12:6-8 kinasema; “Kisha akawaambia, Sikilizeni basi maneno basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?” Alivyomaliza kusema namna hiyo dada yake Musa akapata ukoma!
Ugomvi umetokea wapi? Musa alipooa! Kwa kuwa ameoa msichana ambaye dada yake hakumtaka. Mungu alimtaka, lakini dada yake hakumtaka. Dada mtu akaanza kumsema kaka yake, Mungu akampa adhabu! Dada mtu alipopewa adhabu ile na kaka mtu akapata shida, Israeli nzima ikapata shida, hawakusafiri walisimama wote, hawakuendelea na safari. Ugomvi ulitokea wapi? Ulitokea mtu mmoja alipooa!
Nimeona ndoa zingine kijana anaoa lakini uhusiano wake na baba yake na mama yake unakatika wakati huo huo. Vijana wengine wanakuwa hawako waangalifu hapo, na ndio maana mambo yakiwa magumu, na wazazi wanawabishia juu ya kuoa au kuolewa kwao hawataki kwenda kuzungumza na wazazi wao; wanapiga ‘short cut’, wazazi wao wanakuja kuambiwa tu saa na tarehe ya harusi!
Biblia inasema, “waheshimu baba na mama yako, hii ni amri ya kwanza yenye ahadi ili upewe siku nyingi katika nchi upewayo na Mungu wako” (Waefeso 6:1). Na kwa sababu hiyo vijana wengi sana wakiishakorofishana wazazi wao hawaendelei katika ndoa muda mrefu wakiwa na amani.
Sasa sisemi kwamba wamkubali tu huyo msichana au huyo kijana, ni zaidi ya hapo unajua. Suala ninalozungumzia hapa ni la wao kukupa kibali, na wakafurahi. Unaweza ukasema, hawaelewi kitu au hawajaokoka, kwa hiyo hawahitaji kuelezwa kitu. Hapana!
Ndio maana unahitaji kuomba. Kwa sababu unajua suala la kutaka kuleta msichana au kijana ndani, sio la kwako peke yako, linawahusu wazazi wako na ndugu zako kwa sababu unawaingiza kwenye familia nyingine. Hata kama unataka kuoa au unataka kuolewa, ni mambo ya kifamilia maana ni koo mbili zinakutanishwa na kuunganishwa.
Wakati mwingine unaunganisha kabila mbili au unaunganisha kabila tatu, (wengine hawaelewi kitu ninachosema, kwa mfano; “Mimi ni mnyakyusa, mke wangu ni msukuma, watoto wangu ni kabila gani”? Wanakabila mbili, ni mchanganyiko wa wanyakyusa na wasukuma, maana ningetaka kujipendelea ningesema ni wanyakyusa.
Lakini ndani wanaunyakyusa na wanausukuma halafu waolewe na mtu wa kabila lingine ambalo sio mnyakyusa wala sio msukuma, ni makabila mangapi yanaungana hapo, matatu! Sasa fikiria na anayeoa kwangu na yeye awe ametoka kwenye mchanganyiko wa namna hiyo.
Unaunganisha hapo makabila matatu, manne, matano, sasa wewe unataka wazazi wako wasiifuatilie ndoa hiyo kwa karibu. Kwa nini? Ukipata shida utarudi kwa wazazi wako, sasa kwa nini wakati wa maamuzi wasikusaidie!
Na mimi ninakuambia iko njia ya kutokea, ikiwa utapata tatizo la namna hii; wewe kukaa kwenye maombi kwa namna ambavyo, kama ni Mungu kweli aliyekupa huyo msichana au aliyekupa huyo kijana, basi ataweka kibali hicho hicho ndani ya wazazi wako, ili na wao wamkubali.
Saa nyingine unaweza ukapata marafiki wengine wazuri, lakini wakati mwingine marafiki wengine wanakuwa ni wabaya. Maana ukishaolewa marafiki wa mume wako ni marafiki zako, ukishaoa marafiki wa msichana ni marafiki zako. Vijana siku hizi wanaotaka kuoa au kuolewa wakitaka kujua ukoje, hawakuangalii wewe wanaangalia marafiki zako. Marafiki ulionao ndio wanaoonyesha picha uliyonayo ndani yako.
Rafiki wa kweli hafuati pesa ulizonazo, anafuata tabia uliyo nayo, wale marafiki wanaokufuata kwa sababu unacho kitu cha kuwapa hao sio marafiki, wanakufuata kwa sababu unachokitu, siku ukiishiwa huwaoni. Lakini wale marafiki unakuwa nao wakati wa shida na wakati wa raha, ni marafiki ambao malengo yenu na tabia zenu, kufikiri kwenu kusema kwenu zinafanana. Hao ndio marafiki ambao wanakuwa marafiki zako wa kweli; siku ukiwa na shida ni marafiki zako, unahela ni marafiki zako, umefilisika ni marafiki zako, hao ndio marafiki zako!
Sasa kama mtu anataka kukuangalia ulivyo, anaangalia marafiki zako. Sasa, akiangalia marafiki zako, hata kama unasema, ‘Bwana asifiwe’, hata kama unapiga pambio mpaka jasho la damu linatoka, lakini wanaangalia marafiki zako ulionao, na wakati mwingine ni wabaya kuliko wale wa kule duniani, wanajua na huyu msichana au huyu mvulana kuna mahali ‘ana short’.
Kwa wengine inakuwa vigumu kuliona kwa namna hii, lakini ni lazima ufahamu ukiwa kama kijana, lazima uwe mwangalifu juu ya marafiki ulionao. Vijana wengine wanabaki kushangaa kwa nini wasichana wanahangaika wanasema hatuoni vijana wa kuwaoa, wakati vijana wapo, lakini nani ataolewa na vijana ambao wameokoka lakini hawana msimamo? Nani anataka kijana wa namna hiyo ambaye anashinda vijiweni sawasawa na hao vijana wengine wa duniani?
Mwanaume akitaka kuoa lazima ajifunze kuwajibika. Hawezi akawa na marafiki ambao hawawajibiki kimaisha – na akataka aone na aendelee na urafiki nao. Akiwa karibu na hao marafiki, itakuwa ni vigumu kuwa na ndoa yenye amani. Angalia tu marafiki alionao, unashangaa kwamba anaendelea kusema bado ameokoka. Unashangaa wale marafiki alionao, hawafananii, hawawezi hata kumtia moyo kuomba, hawawezi kumtia moyo kusoma neno, vitu wanavyozungumza ni vitu vya ajabu.
Unajua, hata wakati mmoja hawana maneno ya kutiana moyo ya kuwa na maendeleo binafsi, lakini ndio anaoshinda nao toka asubuhi mpaka jioni, halafu anataka kuoa msichana ambaye ameokoka, anayeshinda kwa Mungu , anayekaa kwenye maombi, anayetaka kuona cha Mungu kinasimama katika maisha yake, ndiye anataka kwenda kwake ili amuoe;- hii siyo sawa! Ndoa yao itakuwa na matatizo tu kwa muda mrefu.
Maana usije ukapata shida ukiingia kwenye ndoa na kijana wa namna hiyo. Wewe uliona kabisa marafiki zake walivyo, unaolewa na ndipo unaposema, ‘mimi sitaki hao marafiki zako’! Imeanza wapi? Atakuambia vizuri kabisa “ulinikuta nao”, kwa nini hukusema mapema kabla hatujaoana ya kuwa huwataki?
Msichana anaolewa na ndipo kijana anamwambia hao marafiki zako nisiwaone hapa, lakini alikuwa anawakuta chumbani kwako wakati alipokuwa anakuja kukutembelea na hakusema kitu, na wakati mambo yakiwa magumu katikati yenu alikuwa anawatumia wao kukubembeleza ukubali kuolewa naye, sasa umekwishaolewa hawataki. Anaanza kuwasema ya kuwa tabia zao sio nzuri. Hili jambo si zuri; alitakiwa aseme mapema juu ya kutoridhika kwake na rafiki zake.
Unapotaka kuoa au kuolewa, usifikirie tu picha ya yule mtu wakumuoa au kuolewa naye, ni vizuri kuangalia na aina ya marafiki zake wa karibu – je unaweza kuchukuliana nao?.
 
Mbarikiwe kwa kusoma na kuyafanyia kazi akuna maana ya kusoma kama mwananchi ukaishia hapa soma neno shika neno tenda neno
 
nukundi kitutkitu ngewikia kuro ulakuso mamndenyi inu tupu !!nukumburie enda kanyyi mwisho maka
 
Asante kwa somo zuri kamanda.Hakika litawafaa sana vijana wetu
 
Back
Top Bottom