Ndo nimeajiriwa kwa huu mshahara, nipeni mbinu za kufanya nitoboe ndani ya huu mwaka

Soma kitabu kinaitwa mabala the farmer kile kipande cha mabala tu peke yake kisha tafakari kwa kukusaidia hiyo sehemu unasema mabala 1961 alimaliza shule akapata kazi baada ya kupata kazi mwamba akajua kula bata tu hakuwaza kujenga, kununua mashamba wala nini yeye bata batani si hana tegemezi ila mwaka 1975 mabala akaoa kwakua alikuwa yeye na mkewe hawana watoto wala nini bata likaendelea si ana ajira bwana ila mwaka 1979 mabala na mkewe wakapata mtoto,

Baada ya kupata mtoto maisha yakabadilika vitu bei juu kipato hakikidhi mahitaji na mbala kazoea bata akastuka anaitaji kutunza pesa na kujenga ila kipato kigumu pamoja na mkewe kujituma ujasilimali maisha yakawa bado magumu, kumbuka alikaa miaaka zaidi ya 15 anakula bata akumbuki jipanga maishq ya badae anakumbuka mda umeenda sana

Hali ilikuwa mbaya pale mtoto wao mabala anataka kuanza darasa la kwanza mabala hana hata mia mbovu

MY TAKE
Unapoanza ajira kuajiriwa maana yake safari ya kuijenga famila yako mdio imeanza siyo mda wa kupoteza kukesha kwenye makumbi na starehe au nyumba za wageni ukistarehe, kama ulishindwa kufanya huo ujinga kipindi upo masomoni basi jipe miaka saba au kumi ya kujenga misingi ya maisha yako na familia yako ndio uanze tena otherwise unapotea

So weka mipango yako kipi kipaumbele chako kabla ujawa na familia je usafiri au makazi, au umiliki wa aridhi

Kama unakopesheka narudia kama unakopesheka na hauna familia
Nenda kakope anza na kipaumbele chako namba moja kama gari kopa pesa utakayo nunua gari na aridhi kama ni makazi kopa pesa utakayo anza ujenzi ma kuishia kwenye hatua ya upauaji na kanunue aridhi

Kwanini kwenye kila kukopa nasema usiache aridhi na maana aridhi inapanda thamani kwaiyo kwenye aridhi u akuwa kama umetunza pesa na usikimbilie kununua aridhi katikati ya mji tafuta nje ya mji eneo ambalo unajua baada ya miaka mitatu uhitaji wa aridhi utakuwa mkubwa so unaweza kuuza pesa ukafanya jambo jengine

Turudi kwenye point nasema kopa nunua gari na aridhi na maana a aisha ya kibongo huwezi tunza pesa ukanunua gari kwa mshahara wa milioni ambao shida na raha unautizama

Kwaiyo unapokopa ukanunua gari let say mkopo wa miaka mitatu, unachukua na aridhi mkopo ukiisha tayali una aridhi, unakopa tena miaka mitatu, unainua boma la nyumba, na kununua aridhi, unakaa mika mitatu mkopo ukiisha kazini unakuwa na miaka sita ila una gari na boma la nyumba na viwanja viwili hapo sasa ndio unasema natoka mazima hata kama umeoa una mtoto hapo ndio mda wa karata yako ya mwisho

Uza viwanja vyote, uza gari yako hiyo uliyokaa nayo miaka sita nenda kapaue nyumba yako weka grill za madirisha na milango rudi kukopa sasa mkopa wa kikomo ule mrefu unachukua pesa nyingi chukua huo mkopo fanya finishing nyumba yako, hamia pesa inayobaki tafuta gari nyingine, na aridhi tena nje ya mji tulia anza furahia maisha na familia

Kumbuka hapo una miaka sita kazini una nyumba yako usafiri wako familia yako, na mshahara lazima utakuwa umebadilika na ujaishi kwa mateso kazini kwani ulikopa ukiwa na malengo so baada ya hapo anza kubeti sasa kwenye ujasilimali mtaji ukipotea unatulia unakopa tena u abet biashara nyingine hivyo hivyo unajitafuta

ZINGATIA
USIKOPEE PESA NDEFU ETI ANZA BIASHARA KWANI WATANZANIA KITU PEKEE TUNACHOONA NI RAHISI KUKIFANYA NA INAWEZEKANA NI BIASHARA STOP THAT WEWE MWAJILIWA PATA MAKAZI USAFIRI ANZA KUBET NA BIASHA KWANI HUWEZI SIMAMIA BIASHARA KWA UCHUNGU KAMA MTU AMBAYE BIASHARA NDIO AJIRA YAKE SO WENGI WATUMISHI WENGI WAMEPOTEA HAPO LEO STRESS ZINAWATESA
Shukran sana mkuu ....nakufata pm🙏
 
🙏....Please Naomba specific analysis
Yan nasave % ngap, nainvest % ngap.
Na kama nainvest nainvest kwenye nini inayohitaji minimum supervision?
Ili kupata analysis nzuri kuna info kuhusu matumizi yako ya msingi ambayo ni must ni kiasi gani then from there utajua unabakia na kiasi gani or asilimia ngapi for saving, naweza sema save 80% kumbe 20% haitoshi expenses zako za msingi.

Unaweza kuwekeza kwa kununua hisa, weka fixed deposit kama uko busy na huhitaji supervision. Otherwise angalia potential kwenye eneo unalotaka kufangua biashara then utaamua iwe ni biashara gani
 
Wataalam wa Darisalaam nawasalim,

Ndo nmereport kazin apa na takehome ya 1M. Nipeni mbinu za kufanya ili kufikia mwisho wa mwaka huu nisiwe Tena mtegemezi wa mshahara.

Nipeni mbinu za kiasi gani Cha kusave, kuspend na kuinvest ili kijana wenu nisiwe napiga marktime.

Na kama nainvest nipeni ushauri noinvest katika biashara gani ambayo Haina risk sana kwa sisi tunafanya kazi za kuajiriwa.
Nipeni pia mbinu za kuhandle vizinga kutoka kwa wanawake,ndugu,jamaa na marafiki.

Natanguliza shukran.🙏
.....kutoboa ndani mwaka huu ? Hapa sijaelewa....why meakacmmoja tu ? Weka malengo muda mfupi na mrefu endelea kuishi kwa malengo.....watu wana zaidi huo na mwala 20 sasa bado hakijaeleweka kivile....hiyo ni safariii
 
Wataalam wa Darisalaam nawasalim,

Ndo nmereport kazin apa na takehome ya 1M. Nipeni mbinu za kufanya ili kufikia mwisho wa mwaka huu nisiwe Tena mtegemezi wa mshahara.

Nipeni mbinu za kiasi gani Cha kusave, kuspend na kuinvest ili kijana wenu nisiwe napiga marktime.

Na kama nainvest nipeni ushauri noinvest katika biashara gani ambayo Haina risk sana kwa sisi tunafanya kazi za kuajiriwa.
Nipeni pia mbinu za kuhandle vizinga kutoka kwa wanawake,ndugu,jamaa na marafiki.

Natanguliza shukran.🙏
Huwezi toboa ndani ya mwaka labda sikio, Oa tunza wazazi wavute wadogo zako vaa vizuri pendeza tukutane Kidimbwi tupande juu ya meza tukicheza miso misondo.
 
M30 basic, M1 takehome
Muongo.

Kwa hiyo 2,500,000/- basic inaleta net ya 1,000,000/-??
Kwa makato yepi?
Kuna ma HR na Payroll Accountants humu ujue.
Screenshot_20240129-070331.jpg
 
Back
Top Bottom