Ndivyo nilivyo .... Niko hivo....

Usijali Kasie. Visichana vya sasa wala! They should never bother you. Stick to the fashions that please and suit you. Kwani bibi zetu hawakupendwa na babu zetu japo walikuwa hawana make up? Tupo wanaume wengi tu we admire original beauty from God

Ooh yeah... usemacho ni kweli. After all I don't bother. ...
 
Habari za jumapili,

Mmh iko hivi...

Kasie ana mazoea yake na kawaida zake sasa usifikiri hata siku moja utatoka huko ulikotoka ukambadilisha Kasie muonekano wake au haiba yake.

Duniani hatulingani hata kidogo kama ambavyo tumeumbwa kwa namna tofauti tofauti ndivyo ambavyo haiba na mionekano yetu haiwezi kufanana.

Yaweza kutokea mtindo wa kisasa wa nywele au nguo au mavazi au nakshi ambazo wewe ukaona ni swaga kwa mschana au mdada yeyote basi usilazimishe nami niwe kama hao. Mfano sasa hivi kuna mtindo wa nywele bandia za kutoka Brazil ambazo mdada au mschana akivaa hizo nywele huonekana kama zake na zina bei hadi laki 9 na watu wananunua. Aiseeh kama hizo swaga hazipandi akilini mwangu hatoniona nimetinga. Vivyo hivyo kwenye vitu vya urembo kama rangi za mwili rangi za kucha au rangi za mdomo na nyusi.
Wako walioniita mshamba bin wakuja bin wazamani wengine wakasema mie ni shkamoo jazz band.... sawa ila nafanya navaa na kupaka kitu kwenye mwili wangu ambacho nimeridhika nacho na kwa asilimia kubwa kama si 97 huwa naambiwa nimependeza kutoka majirani, kanisani, sokoni hadi kazini.

Imenilazimu kuandika haya baada ya kukutana na mdada leo kanisani yuko eeh Kasie mbona unajizeesha kuvaa haya magauni ya kutarizi ya kizee? Halafu nywele mbona hiyo ni mitindo ya zamani? Nikamsalimu nikaingia kwenue gari na kurudi nyumbani maana ibada ilikuwa imeisha na sikutaka kupoteza upako wangu wa jumapili maana nilihisi ninhefunua mdomo kumjibu ningemtukana halafu ingekuwa mbaya zaidi.

Mchana baada ya kupata mlo wa mchana nyumbani nikaenda zangu mahali kuna mambo flani nilikuwa nafatilia nikakutana na mkaka tulisomaga nae chuo yuko ooh Kasie za siku mingi na makumbato mengi na busu za gafla za mashavu za kurudia rudia.... baada ya muhtahsari wa salamu akaniambia you still look good... hahaha tukaagana kila mtu anaendelea na yake.

Yawezekana huyo mkaka alinisifia ile ya mwanaume kawaida kimsifia mwanamke hata kama hajapendeza walau kuonekana ameongea na huyo mdada.

Sina shida na hilo ila nimejikuta Kasinde nafanya mambo kwa ajili yangu na si kwa ajili ya mtu au watu wanione.

Nikifanya mazoezi ni kwa ajili ya afya yangu na mie niwe fit kwa jinsi ninavyojipenda na si kwasababu flani anione. Ukiniambia tutoke out usitarajie ntaenda kununua nguo na kwenda saluni kwa ajili unione niko vizuri, ntakuja mtanashati kama sikuzote nnavokuwaga mtanashati.

Nikienda saluni kutengeneza nywele au kucha ni kuwa muda wangu wa kwenda kusuka au kutengeneza kucha umefika. Nikinunua nguo ni kwasababu nimeipenda na ntaivaa kwenye tukio lolote litalotekea au hata siku ya kawaida.

Hivo wee bidada (yupo humu) wiki ijayo ukiniona kanisani uwe ushapata jibu la maswali yako.

Poleni kwa maelezo marefu, ndivyo nilivyo hehehe.

Kasie.
Ur right dear .. Ishi uwezavyo huwez mridhisha kila mtu
 
we Dada kama Mimi usitarajie eti nitoke unavyotaka wewee!

Niko kama nilivyo kwa kweli!

Kwanza makorokoro mengi kwenye mwili wangu hapana

Sina huo muda wa kufurahisha hadhira zote!

Halafu ukiwa mzuri,ni mzuri tu!
 
Hongera.

Kama uko hivyo haufati mkumbo kama vidada vya siku hizi unafaa.

Siku hizi wadada wanatisha sana siyo siri;

Ngozi bandia

Nywele bandia,

Kucha bandia,


Yani maisha ya siku hizi ni zaidi ya movie.
hayo mambo yamenishinda hata filter siweki

ukiniona ndo nilivyo yaani
 
Sio tuu kuwa tofauti nao ni kuwa tuu unakuta nikijaribu kufanya hayo huwa nakosa ujasiri mbele za watu nahisi nikitabasamu wataona kama nimekunja uso nalia au kama nimelamba ndimi hivo kuipa shida akili yangu kuwaza anayenitazama anaona sawa au kituko aaah sasa adhabu yote hiyo ya nini?

Hata nikihusishwa kwenye shughuli ambazo nahitajika nipake rangi za mwili (make up) basi nikitoka hapo lazima yule mpambaji alalamike juu yangu maana wale nao hawatakagi kukosolewa. Anachoona yeye anaona yuko sahihi mie nikifika namwambia wanja na rangi ya mdomo nipe nipake mwenyewe.... hiyo foundation kila akipaka naangalia kisha namwambia hapo basi akisema bado nanyanyuka yaani sio nakuwa msumbufu makusudi ila nawaza kwanini naondolewa uhuru wangu wa kutabasamu?

Niko hivyo ana ndivyo Kasie alivyo.
just like me!
 
we Dada kama Mimi usitarajie eti nitoke unavyotaka wewee!

Niko kama nilivyo kwa kweli!

Kwanza makorokoro mengi kwenye mwili wangu hapana

Sina huo muda wa kufurahisha hadhira zote!

Halafu ukiwa mzuri,ni mzuri tu!
Sema hakyamungu...
 
Ingekuwa ni kufika bei ningeshaolewa siku mingi basi tuu nimeamua hivyo kama jinsi nilivyo niko hivyo. Na hii naisemaga sana humu ndivyo ilivyo.
Duu!!inalekea una msimamo kama mimi!!kwa hiyovsasa hatma yako ni nini mbeleni!!vipi ulishazaaga!!
 
Hongera.

Kama uko hivyo haufati mkumbo kama vidada vya siku hizi unafaa.

Siku hizi wadada wanatisha sana siyo siri;

Ngozi bandia

Nywele bandia,

Kucha bandia,


Yani maisha ya siku hizi ni zaidi ya movie.
Yaani kila kiru bandia, mwisho yeye mzima anakuwa bandia..!!!
 
Back
Top Bottom