SYLLOGIST!
JF-Expert Member
- Dec 28, 2007
- 7,259
- 6,903
Nakandamiza kibara yupo wapi?
Binafsi sifagilii chama chochote cha siasa Tanzania, kumekua na tuhuma hapa JF kwamba mtandao huu ni wa Chadema na maoni mengi yanayotolewa kwenye hii thread yananilazimisha kuanza kuamini hili.
Nakumbuka wiki kadhaa hapa kulikua na habari ya Bw. Msekwa kujenga shule ya sekondari huko kwao Ukerewe, mashambulizi aliyoyapata yalikua ni ya kutisha na kushangaza.Kuna tofauti gani kati ya kitendo chake na hiki cha Mh. Ndesamburo? Tusiwe biased waziwazi kiasi hiki jamani.
Ndasamburo ni mbunge wangu. Ila naweza kusema huyu mzee bwana anajitahidi. Ni tajiri anayejeribu kula na masikini. Nakumbuka aliwahi kununua Ambulance kwaajili ya Hospital ya mkoa (Mawenzi Hospital) kwa pesa zake mwenye. Nakumbuka huyu mzee aliwahi kutoa msaada wa compter nyingi tuu kwa shule moja ya sekondari huko moshi serikali ikashindwa kupeleka umeme.
Unajua kutokana na kujitoa kwake kutumia chake cha mfukoni ndio imefanya CCM washindwe kumtoka kabisa pale. Uliza watu wakuambie Shemeji yake Mkapa (Mama Minde) alivytumia pesa nyingi kuwarubuni watu wa Moshi mjini lakini bado tuu walimchagu Ndesa Pesa.
Ndio huyu mzee ni tajiri na huwa tunasema kuwa mtu h ashibi pesa lakini kwa kitendo chake cha kutoa pesa zake kuletea watu maendeleo hata kama nikumletea mtu mmoja maendeleo ni mfano wa kuigwa.
Kwani matajiri wangapi wanazo jamani na wanashindwa kusaidia?
JF Members and contributors to this thread if I were you I would ignore the comments of SYLLOGIST.He has already displayed his ignorance sufficiently .Let's concentrate on more important issues like the BOT scandal and not forgetting the mining industry .
Capitol Hill
Nandevu nyingi kama hizo utaenda tu kununua ekari tano na kugawa tu? ndio kurubuni kwenyewe-nilitaka kusema hongo lakini ilikuwa haingii-sasa nikisema labda alikuwa anatoa hongo kwa wapiga kura hao 1000 nitakuwa nimekosea?
Kwa kweli kama ni mfanyabiashara na alikuwa na azma nzuri tu basi hakuna taabu. Kwa mwandishi kudai ni MP amefanya hivyo(kuleta maendeleo) pia ni kudanganya kadamnasi. Au hii ndio sera ya CHADEMA? Jee ofisi ya MP ina bajeti? Tueleweshane
Huyu mzee hakuanza leo. Alivyopata ubunge mara ya kwanza alienda kwenye hospitali ya mkoa akabadilisha kuanzia vitanda, shuka, magodoro pamoja na ukarabati mwingine na kuwapa ambulance 2. Hivyo wapiga kura wake wanamwelewa vizuri tu.
Mbona unakurupuka hivyo tena? Kuuliza yuko wapi ina maana ngapi? Hiyo hoja iko wapi? Haya mie sio wa JF lakini nimo humuhumu na sing'atuki!SYLL unamuuliza mzee wa Kibara kwa nini ? Unataka kujua yupo wapi ukiwa na maana ipi ? Mimi si msemaji wake ila nimeshangaa hoja hii na swali lako kwa mwana JF huyu .
Mbona unakurupuka hivyo tena? Kuuliza yuko wapi ina maana ngapi? Hiyo hoja iko wapi? Haya mie sio wa JF lakini nimo humuhumu na sing'atuki!
Alikuwa na maana gani ya kuanzisha hi thready...halafu anagwaya?
Ngoja niangalie kama hii ni mwenendo wa humu manake mtu ukiwa mgeni basi kila mtu anakutupia madongo shabash.
Sasa lunyungu unataka kumtetea kama sio msemaji wake tena?