Ndege zote zinazotua uwanja wa ndege wa Mwanza zimezuiwa leo

ARV

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
4,983
6,986
Umeme wa TANESCO umekatika, Generator ya Mwanza Airport mbovu. Ndege zote zinazotua kuanzia saa moja usiku zimefutwa. Hii nchi ngumu kuishi.

===============

Urgent - Due to an electricity outage at the Mwanza airport all airlines have been forced to cancel flights departing after sunset. Your reservation XXXXXX has been moved to flight FN0131 on 02AUG. We are sorry for the inconvenience but this is beyond Fastjets control. For further info please contact yor nearest fastjet office or call 255784108900
 
Hivi huu upuuzi unaofanywa na Tanesco utaisha lini jamani?mbona tunapata manyanyaso kwenye nchi yetu na pesa ya umeme tunalipa? Imenikera sana hii
 
Tunaanza na wa chini kwenda juu hadi tutapata anayehusika tu...

Ukweli ni kuwa mfumo wa uzalishaji wa umeme uko hoi sasa lakini si wizara wala hao tanesco wanaosema ukweli. Haijulikani ni madeni ya kuendesha hayo mamitambo ya iptl au hao wanaotuuzia gesi yetu wenyewe.
 
Na bado hakuna wa kuwajibisha wala kuwajibishwa...

Hakunaga mzee.
Wako busy kukata umeme watu wasione Lowassa anahamia CDM.
Halafu na ujinga wao huo huo wanakata umeme kwenye vyanzo vya mapato na sekta zinazochochea utalii.
 
Nakumbuka toka miaka ya 1984 habari ya kutua ndege usiku mwanza imekuwa ndoto ,hivi mpaka Leo mamlaka husika imeshindwa kutatua tatizo?kweli viongozi wapo likizo ya muda usiojulikana
 
Tunaboresha kiunombinu jamani.Tulieni tuli na sasa hivi tupo juu ya nguzo inchi nzima kama taa za barabarni hatubaguani wake kwa waume,wazee kwa vijana,babamkwe kwa mkwilima ndo maendeleo.Ilani ya kampuni yetu ni kwamba ni lazima tuning'inie kwenye nguzo na kukata kata taarifa muhimu za runinga muda wowote.
 
Hivi huu upuuzi unaofanywa na Tanesco utaisha lini jamani?mbona tunapata manyanyaso kwenye nchi yetu na pesa ya umeme tunalipa? Imenikera sana hii

pigia kura ukawa,hapa piga porojo kuwaridhisha ccm lakini ktk kura ni siri yako pigia kura ukawa,usijibu post hii,nenda ukajibu kwa vitendo october 25 ktk sanduku la kura na Mungu akubariki
 
Back
Top Bottom