Ndege iliyopotea kama ingekuwa ni ya Tanzania?

Mchochezi

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
10,432
6,639
Najaribu kuvuta picha, nini kingetokea kama ndege iliyopotea ingekuwa ni ya Tanzania, kuna baadhi ya matukio yangetokea kama vile: 1. Serikali ingetoa mapumziko nchi nzima 2. Zingeundwa tume kama 700 hivi kutafuta chanzo cha kupotea kwa ndege, na tume nyingine 900 kutafuta ndege ilipo. Endelea na wewe kutuambia unahisi nini kingejiri hapa Bongo...
 
waziri wa miundombinu na wasaidizi wake wangejiuzuru na rais angehutubia taifa na kuziita familia za waanga ikulu kula chakula!!!
 
Watu mnavituko, nimecheka sana, tume 700!
Wahanga wangeitwa ikulu kushiriki msosi..... aisee

Mie hata sijui nini kingetokea kwakweli, labda watu wangekuwa wamelundikana tu pale JKNA wakisubiria kupewa taarifa
 
Unanikumbusha majonzi na mateso ya wananchi baada ya matukio ya mabomu mbagala na gongolamboto.
 
Najaribu kuvuta picha, nini kingetokea kama ndege iliyopotea ingekuwa ni ya Tanzania, kuna baadhi ya matukio yangetokea kama vile: 1. Serikali ingetoa mapumziko nchi nzima 2. Zingeundwa tume kama 700 hivi kutafuta chanzo cha kupotea kwa ndege, na tume nyingine 900 kutafuta ndege ilipo. Endelea na wewe kutuambia unahisi nini kingejiri hapa Bongo...

Pia ingeundwa tume ya kulipa fidia wahanga, ambapo fedha zingechakachuliwa na wajanja wachache .
 
Najaribu kuvuta picha, nini kingetokea kama ndege iliyopotea ingekuwa ni ya Tanzania, kuna baadhi ya matukio yangetokea kama vile: 1. Serikali ingetoa mapumziko nchi nzima 2. Zingeundwa tume kama 700 hivi kutafuta chanzo cha kupotea kwa ndege, na tume nyingine 900 kutafuta ndege ilipo. Endelea na wewe kutuambia unahisi nini kingejiri hapa Bongo...

Wakati yote haya yakiendelea, tungekuwa tushapewa taarifa ya kusitisha utafutaji wa maiti na mabaki ya ndege na kutupa udongo majini kuashiria mazishi
 
na magazeti pendwa nayo yangepiga hela kwa hbari hyo.

mara 'tungesikia misukule ilionekana kabya ndege kupaa
mara kigogo ikulu ahusika na ndege kupotea'
'mara rubani alikataa kurusha ndege alihisi kuna jambo baya litatokea'
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Hapo kwenye tume unanikumbusha nilikuwa nasoma katuni moja ya kipanya kikwete alikuwa anaulizwa na yule kipanya hivi mkuu huoni kwamba hizi tume zinakula hela nyingi tofauti na tatizo la awali tume zilivyoundwa kwa ajili yake???,'akajibu kwamba ngoja niunde tume ichunguze kama kweli tume huwa zinakula hela sana'
 
Wangetafutwa wahandisi wakapelekwa hoteli ya nyota tano kupewa semina ya namna ya kutafuta mabaki ya wahanga wa ndege.

Siku ripoti inakabidhiwa ikulu ingekuwa bonge la sherehe na mukulu lazima apige mapich ya kutosha
 
Back
Top Bottom