Stories of Change - 2023 Competition

allan_gobe_tz

New Member
May 31, 2023
3
3
Uwajibikaji ni neno pana hasa pale unapoangalia upande wa utendaji wake Kwa haki madhubuti kwani serikali italaumiwa hasa pale itakapokuwa na mfumo mbovu wa utawala Kwa wananchi wake, mfano; ajira Kwa vijana hutangazwa nafasi zile za kawaida sector ndogo ndogo lakini sector kubwa kama Uchukuzi, TRA, BOT na nyinginezo huwezi kuona zikitoa tangazo la ajiri lakini watu wanaajiriwa je swali ni kwamba huajiriwa Kwa mfumo Gani na utaratibu Gani??. Hapo serikali inaposhindwa kuwajibika kikamilifu Kwa kitenda haki Kwa wote ndipo huweza kuchochea changamoto nyingi Kwa wananchi.

Utawala Bora, pia huweza kuchochea mabadiliko ya nchi hasa kiuchumi kwani watu hufanya shughuli zao na kuendesha maisha yao Kwa uhuru na amani bira tatizo, mfano; tunaona kipindi hiki baada ya taasisi ya mapato TRA ilivoweza kuleta mkanganyikeni nchini baada ya kukosa utawala Bora pamaoja na uwajibikaji wa haki Kwa wananchi wake ambapo serikali ndiyo kipaumbele Cha kumshika mkono mfanya biashara katka kujiendeleza na kuinuka kiuchumi lakini ndyo inakuwa mstari wa mbele kudidimiza maendeleo ya wananchi hiyo yote inatokana na utawala mbovu wa nchi.

Pia, nchi ikikosa utawala Bora huweza kusababisha nchi kujawa na madeni yasiyo ya razima hasa pale anapojichukulia madaraka mkononi na kuamua jambo bila ya kushirikisha upande wa pili mfano: Waziri wa Fedha MH. Mwiguru Nchemba baada ya kukopa mkopo wa takribani ya Trioni kadhaa bila ya kushirikisha Bunge ambalo ndilo lenye mamlaka na wajibu wa kujadili pesa inayoingia na kutoka, hapo huleta mchafuko wa Hali ya hewa katika nchi yetu Kwa sababu ya upotevu na maadili hafifu ya uwajibikaji Kwa Kiongozi Kwa sababu ya Tamaa kidogo.

Utawala Bora na uwajibikaji ni daraja la kuchochea maendeleo ya nchi Kwani huleta amani, upendo, mshikamano, na utendaji kazi Kwa haki.

Kikubwa zaidi serikali katika utoaji wa ajira nngependa kushauri Kwamba serikali iangalie kwanza na historia ya mtu husika kwani kunao wengine wanategemewa na familia zao masikini hususani vijijini masikini yamungu familia Fulani mpaka inauza kiwanja ilimradi tu mwanoa asome Ili badae aje awaokoe lakini Cha ajabu kutokana na utawara Bora kutoweka anaajiliwa kijana wa familia tajiri halaafu kijana wa familia masikini anaachwa mtaani Kwa haki za kibiinadamu siyo sawa hata kama ni Kwa kuangalia G.P.A Bado mtoto wa masikini anayo nafasi kubwa kupewa ajira kwani kapitia magumu na mengi kipindi Cha masomo yake atakama ufaulu wake mdogo. Kwa njia tofauti serikali inaweza kutambua historia ya mtu huska juu ya familia yake kwani aidha masikini au yenye uwezo Ili aweze kupewa kipaumbele katika ajira za mwanzo.
 
Back
Top Bottom