Nchi 10 kati ya 14 za Ulaya zasitisha msaada wa kibajeti kwa Tanzania

Ndiyo naanza kuelewa na kupata picha kwa nini alikataa kwenda kwenye mikutano ya ulaya au kujitambulisha, hapa picha inaanza kukamilika!.
 
Mheshimiwa Magufuli Watanzania tupo tayari kula nyasi kuliko kuwategemea wahisani ambao misaada yao inaishia kutunyonya tu na kutu didimiza
 
ukijipa muda wa kufikiria hawa wote si kwamba wanafurahia bali wangi wanakata tamaa na kuamini kama kwa sela zile zile uongozi uleule wa misaada, tutaweza fikia malengo ya maendeleo?

jua pato la tz ni dogo sana, mahitaji ni mengi mno kuliko kipato, je bila misaada tutafika?

kumbuka tunadeni la trion 34 kwa sasa, linatakiwa lilipwe.

nakubali njia ya kufikia maendeleo ni kuachana na misaada yenye kukandamiza kwa mlango wa chini, na mikopo yenye mashart magum. swali je tumejiandaaa?

pia mafisadi wapo watakula wapi? ukifikilia kimazoea utajua ugumu wa hili swala, ila kama magu ni exceptional enough wacha tuone

MUNGU IBARIKI TANZANIA
Sidhani kama unafikiri vizuri. OK umesema deni ni tirion 34 hili deni tumelipata wakati gani? Kunahajagani ya kupewa misaada ingali deni linazidi kukua?
 
NINA WASIWASI SANA NA HUJUMA ZA KIMKAKATI DHIDI YA MAMA YETU TANZANIA,KUNA HAJA YA KUPITIA UPYA BAADHI YA MAAMUZI,MISIMAMO,NA MITAZAMO YA KICHAMA {CHAMA CHENYE ASILIMIA ....

YA WATANZANIA} YENYE MADHARA MAKUBWA KWA TAIFA KIUCHUMI,KIJAMII LEO NA KESHO NA KESHO KUTWA...NCHI HII NI YA WATANZANIA WATOTO,WAKUBWA,WENYE VYAMA,WASIO NA VYAMA.

MAJIRANI WASIOTUPENDA WANAFURAHI SANA KUSIKIA TUNAPATA MATATIZO AMA TUNARUDI NYUMA KIMAENDELEO.
 
Acha mawazo potofu,siku zote mtoto anapo achwa atembee mwenyewe bila msaada ndo anapopata akili zaidi akitaka kuanguka atajua jinsi ya kujiokoa
Hatutakiwi kulaumu sana kwanini hatutapata msaada tujikaze kwamwendo huu ambao serikali yetu inakwenda nao naimani tunaweza piga hatua japo tuta umia kiasi....tutafika
Mkuu ni kweli lakini itategemea huyo mtoto yupo mazingira gani anapojifunza kutembea,kama ni ghorofani ataishia kuzimu.
 
Dua la kuku halimpati mwewe. Umeangalia leo exchange rate ya Tsh vs USD ni kiasi gani halafu linganisha na mwaka Jana.
Unazidi kuonyesha ulivyo zero ila kukusaidia ngoja nikupe hint...hayo mambo huwa hayatokei overnight
 
Sidhani kama unafikiri vizuri. OK umesema deni ni tirion 34 hili deni tumelipata wakati gani? Kunahajagani ya kupewa misaada ingali deni linazidi kukua?

MKUU TULIZA AKILI SOMA VIZURI.

TUKIWA NA MISAADA YA BURE NDO TUKAFIKA KATIKA HILO DENI

JE SASA HAKUNA MISAADA NADHANI DENI LITAKUA DOUBLE (ASSUME MAGU HANA MIUJIZA YA KUTOKA HAPA)

JIA NZURI YA KUPATA MAENDELEO NI KUACHANA NA MISAADA BORA TUKOPE KWA MASHART YA KIBIASHARA.

JE SELIKARI ILIJIANDAA KWA HILI AU NAYO INASHANGAA TU KAMA MIMI?

NAJUA TUTASAVAIVU ILA SI KUFIKIA MALENGO YA MAENDELEO

MTAZAMO TU
 
Mheshimiwa Magufuli Watanzania tupo tayari kula nyasi kuliko kuwategemea wahisani ambao misaada yao inaishia kutunyonya tu na kutu didimiza

SI ANZA KULA YA UPENUNI MWA NYUMBA YA KWA MZEE WAKO MPAKA UMWAMBIE RAIS WETU
 
WAKATI MAREKANI KUPITIA MCC WAKISUSA, CHINA WAJIPANGA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA NISHATI NCHINI

Wawekezaji kutoka katika makampuni yanayojihusisha na uzalishaji wa nishati ya umeme kutoka nchini China, wameeleza nia ya kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini ili iweze kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi.

Waliyasema hayo katika kikao na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)

Akizungumza katika kikao hicho Mwakilishi kutoka Umoja wa Wafanyabiashara katika Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong, alisema kuwa nia ya makampuni yanayojishughulisha na uzalishaji wa nishati ya umeme ni kubaini fursa zilizopo katika sekta ya nishati nchini kabla ya kuja kuwekeza rasmi
Aliongeza kuwa ujumbe maalum wa wawekezaji kutoka nchini China unatarajiwa kuwasili nchini mapema wiki ijayo kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali zenye kubainisha fursa za uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na mpango kabambe (master plan), sera, na mpango mkakati katika sekta ya nishati, kabla ya kusaini makubaliano ya awali kwa ajili ya uzalishaji wa nishati ya umeme.

Zhiyong alisisitiza kuwa wawekezaji kutoka China wako tayari kushirikiana na wawekezaji wa ndani ya nchi kwenye uzalishaji wa nishati ya umeme ili taifa liweze kupata nishati ya uhakika kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.

Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia nishati Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo alishukuru ujumbe huo na kueleza kuwa fursa za uwekezaji kwenye sekta ya nishati ni nyingi na kuwataka kuchangamkia fursa hizo.

“Wananchi wanahitaji nishati ya uhakika ambayo ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo tunawakaribisha kuwekeza katika uzalishaji wa nishati ya umeme kwa kuwa tuna vyanzo vingi kama vile gesi, jotoardhi, makaa ya mawe, jua, upepo n.k,” alisisitiza Dk. Palangyo.

Chanzo: michuzi
Nimekuvuta huku ili ujionee marafiki wanavyoshirikiana kututia adabu. Sifa ya kujigamba eti tuko imara, tutakoma.
China haijawahi kuendeleza nchi yoyote duniani hapa. Waiteni Wachina walete viwanda vya yeboyebo na kusindika nyama za punda
 
Ila mimi najiuliza kitu kimoja, uchaguzi zilizofanyika zanzibar za 1995, 2000, 2005, 2010. kuna misaada ilikatwa na wahisani kipindi hicho???
mi naona its right time kwa wasomi wetu wa uchumi waje na maarifa ya kuendeleza maendeleo ya nchi bila ya kutegemea misaada ya wahisani.
 
Moja ya Sera za nchi za magharibi ni kuhakikisha hakuna nchi zilizoko ulimwengu wa tatu zinajitegemea kwa hali yoyote zikijaribu au kuonyesha muelekeo zinawekewa vikwazo vya kiuchumi ikishindikana zinavurugiwa amani
rejelea kilichotokea Libya ilifikia kuwalipa mshahara wasiokuwa na kazi pia Libya ilikuwa inatoa msaada kwa baadhi ya nchi za kiafrika na kutoa mkopo usio na Riba kwa kukopesha mafuta ya petroli na dizeli
Lakini nini kimewakuta Walibya kwa sasa bila shaka ni mkono wa wazungu


kuna baadhi ya wachangiaji wanahoji mbona Burundi haifatwi fatwi au kuwekewa vikwazo wanasahau Burundi imejitolea miaka mingi huko Somalia kulinda amani na ina jeshi kubwa huko wakati nchi nyingi za kiafrika na hata za dunia hazitaki kwenda Somalia kupambana na alshababu jambo pekee linalompa Nkurzinza nafasi ya kutanua Burundi vinginevyo angeshapinduliwa kitambo
 
Tuko tayari kula nyasi , kuwalamba miguu wazungu sasa basi
Jeuri ya hapo zamani za kale!
Subiri utaona jeuri ya maji safi na umeme, tutaishia nguzo za mikaratusi mitaani. We are weak to say NO! Hii ni nchi isiyo na reserve hata ya miezi mitatu (3)! Amini. Usiige swaga za wanasiasa wanaotaka kura yako ili uwaone ni imara.
 
Back
Top Bottom