NBA All Star 2018: LeBron James Vs Stephen Curry watengeneza timu zao. Nani atatisha?

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari wanaJF,

NBA jana ilitoa orodha ya wachezaji watakaoshiriki mchezo wa 2018 NBA All-Star Game, kama walivyochaguliwa na Manahodha wa timu hizo mbili ambapo moja itaongozwa na LeBron James wa Cleveland Cavaliers huku timu nyingine ikiongozwa na Stephen Curry wa Golden State Warriors.

Tukianza na upande wa LeBron James yeye amewadraft DeMarcus Cousins (New Orleans Pelicans), Anthony Davis (New Orleans), Kevin Durant (Golden State) na Kyrie Irving (Boston Celtics) ambao wataungana naye katika Kikosi kitakachoanza .

> Lakini ili kuikamilisha timu yake bwana LeBron, James amewachagua LaMarcus Aldridge (San Antonio Spurs), Bradley Beal (Washington Wizards), Kevin Love (Cleveland), Victor Oladipo (Indiana Pacers), Kristaps Porzingis (New York Knicks), John Wall (Washington) and Russell Westbrook (Oklahoma City Thunder) kama wachezaji wa akiba.

team-lebron.jpg

Aidha, kwa upande wake Stephen Curry amewachagua Giannis Antetokounmpo (Milwaukee Bucks), DeMar DeRozan (Toronto Raptors), Joel Embiid (Philadelphia 76ers) na James Harden (Houston Rockets) ambao wataungana naye katika Kikosi kitakachoanza mchezo huo adhimu kabisa.

Pia amewaongezea Jimmy Butler (Minnesota Timberwolves), Draymond Green (Golden State), Al Horford (Boston), Damian Lillard (Portland Trail Blazers), Kyle Lowry (Toronto), Klay Thompson (Golden State) and Karl-Anthony Towns (Minnesota). Kama wachezaji wake wa akiba

Mchezo huu wa 67 wa NBA All-Star Game utapigwa siku ya Jumapili Februari 18 katika Dimba la Staples Center huko Los Angeles.

team-stephen.jpg

=====

MY TAKE: Kwa upande wangu naona LeBron ameadhimia kummaliza Curry kwa kutumia nguvu na Lay-ups nyingi sana pamoja na 3 Points lakini Stephen Curry amejipanga kuumaliza mchezo kwa kutumia points 3. Lakini LeBron ataibuka mbabe kwa setup ya kikosi chake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom