Nawauliza wana Simba wenzangu, Mohamed Dewji aliwahi kufanikisha lipi kwenye soka?

Mo alipokuwa mdhamini wa Simba club ilifanya vzr kimataifa kumbuka 2003, ilo moja mbili unachopinga ww ni nn haswa? Kwan ata Mo asingeichukua Simba unahc Simba inge improve? Mboma miaka yote mambo ni yale yale tuu

mimi napinga timu za wanachama kuuzwa kwa bepari mmoja.

hivi hamjiulizi barcelona na madrid kwanini haziuzwi ?

hivi hamjiulizi kwa nini ilipouzwa manchester united mashabiki wakaenda kuanzisha FC united of manchester?
 
Mdoa mada uko sawa kabisa kwanza mhindi na mpira wapi na wapi, hapo wanasimba tumeingia choo cha kike,
 
Kwanza ukakiri wewe ni mwanasimba, mwisho unasema watu wasije shikana mashati! Bila shaka wewe umeshajitoa kuwa si mwanasimba. Tunashindwa kuendelea hasa kwasababu ya mawazo kama haya, michezo ni biashara, hivyo kama kuna vilabu vingine vyenye nia ya kukaribisha wawekezaji basi muda ndo huu, muhimu ni kufuata tararibu na serikali iliridhie.
Kwa kawaida mpira wa miguu pamoja na michezo mingine ni frusa hasa kwa wenye pesa.Kufanya biashara na timu ulizotaja wewe ni kazi ngumu kuliko simba na yanga.Hata sport pesa walipo fika walianza na timu hizo kwanza ndipo wakaanza kufikiri timu nyingine.Mpira biashara elewa hivo.
Majina ya Simba na Yanga ni rahisi kuyauza.

Ni ngumu kuweka pesa yako ktk timu zilizo kuwa zinaendeshwa na wahuni wanaowaza kumfunga Njombe mji au Mbao na si mafanikio nje ya Taifa hili.
 
huu mchakato umeendeshwa kihuni sana mtu anasema anataka kuwekeza anataja bei atakayowekeza na hisa anazotaka halafu anawakopesha pesa kabla ya kupewa hizo hisa.kama kweli simba walitaka kubadili mfumo na mchakato wakauendesha kwa uwazi wangepata washindani wengi tena wenye ofa nzuri lakini ni mtu gani angejitokeza wakati mazingira yote yalikuwa ni kumpa mohamed dewji timu.
yeye sio mwekezaji ni mfanyabiashara mtindo aliotumia kununua simba ndio huohuo aliokuwa anatumia kununua viwanda vya serikali ndio maana Adam Malima alimusema juu ya kiwanda cha nguo alichonunua nutex lakini hajakiendeleza naunga mkono hoja
 
Kufanikisha vp yaani na kama nani?? Wakati hakuwahi kujihusisha na udhamini wa soka zaidi ya ushabiki tu. Kama kufanikisha chochote kuhusu soka ndo usubiri sasa hivi baada ya kukabidhiwa rasmi timu ya Simba!
 
Ha ha ha ha ukitaka kuwajua wana Simba toa hoja!! Huku mtaani kwangu ninapata shiida sana kwani wana simba wengi hawajui kuzitetea hoja ikitewa hoja badala ya kuijibu kwa lugha laini wao jazba tu.
 
Kama nawe huwa unachangia timu hela ya kukuwezesha basi nunua zile hisa 51 % zilizobaki ili usaidiane nae.
Unauliza alishindana na nani wakati pale kwenye mkutano walisema yeye alikua only bidder.
Au hukwenda hata kwenye mkutano?
 
Ungekuwa una akili ungeuliza swali hili wakati wa mchakato. Kwa muda huu ungekaa kimya, kumbe viazi bado vipo
 
Swali lingine la msingi. Wamepaje thamani ya Simba hadi waseme billion 20 ndiyo 51%

Mtu akija Yanga lazima ifanyike valuation kwanza
Thamani ya hizo timu za kariakoo hata billion 5 hazijafika.
We timu haijawahi hata kupata faida ya bilioni moja kwa mwaka toka izaliwe inakuaje na hiyo thamani
Mo kawapendelea sana hiyo hela
 
mimi napinga timu za wanachama kuuzwa kwa bepari mmoja.

hivi hamjiulizi barcelona na madrid kwanini haziuzwi ?

hivi hamjiulizi kwa nini ilipouzwa manchester united mashabiki wakaenda kuanzisha FC united of manchester?
Mpira wa sasa ivi ni pesa asikudanganye mtu, na wala sio kuuza timu na ndio maana wamegawana hisa, ingekuwa ni kuuza hisa zote angechukua Mo kama unakumbuka vzr yule mwarabu wa U.A.E aliyetaka kuichukua Liverpool miaka ile alitaka hisa asilimia 90 liverpool ikagoma kwani madhara yake akifilisika na club inakuwa inakuwa mufilisi lakini kwa izo asilimia wala sio mbaya kwa anayejua mpira
 
Kwanza naomba kukiri kwamba mimi ni Mwanasimba ( mmoja wa wachangiaji wa hela za kuendesha timu ) , ambaye sijaridhishwa na mchakato wa kumuuzia hisa za Simba mtu ambaye anayo historia ya wazi ya kushindwa .

Mohamed Dewji aliwahi kumiliki timu ya soka ambayo baadaye ilishuka daraja , hakuna aliyesahau hili , kama timu aliyoimilki kwa 100% iliporomoka , vipi hii 49% ? , kingine ni kwamba , huyu alikuwa mfadhili wa Singida United alipokuwa mbunge , kipi ilichofanikiwa timu ile , mbona ilishuka daraja na kupotea ? Shukrani kwa walioirejesha tena ligi kuu .

Kwenye mchakato wa kummilikisha hisa za Simba alishindanishwa na nani , yeye alipata kura ngapi na huyo mwengine alipata ngapi ? Tunauliza hivi ili baadaye msije kushikana mashati .

Majuto ni mjukuu .
Wewe sio Simba na wala huna mchango wowote kwa Simba kama hujui Dewji kaifanyia nini Simba 2003 na kuendelea.unanonyesha ulivyo mbulula kwenye zabuni unauliza alipata Kura ngapi?zinakutosha kweli
 
Mkuu, hayo yote kwa nini asifanye Mbagala Market au Singida United.
Hapo Simba hata Bakhresa palimshinda kaanzisha Azam yake.
Mbona una point dhaifu sana ktk uwekezaji wa mpira kuna kitu kinaitwa fan base( wingi wa mashabiki) kama timu ina mashabiki wengi kila mwekezaji atataman kuwekeza apo kwa akili yako mbagala market na simba ni klabu ipi yenye fan base kubwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom