Nawatakieni Mwaka 2012 wenye Baraka

LD

JF-Expert Member
Aug 19, 2010
3,014
574
Habari za kwenu wana Chit chat, MMU na Wanasiasa, na hao wengine wachekeshaji, walalamikaji na wooooooooooooote wenye mapenzi mema na JF.

Kusema ukweli tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa mema yake aliotujalia kwa kipindi chote cha mwaka huu unaoisha 2011.

Mwaka ulikuwa na vipindi tofauti tofauti......lakini kila jambo na kila tukio na kila wakati una sababu na kusudi mbele za Mungu wetu.

Tulipita kwenye wakati wa Furaha, tukapita kwenye wakati wa huzuni pia, Mfano wale waliofiwa na ndugu, jamaa na marafiki na hata ndugu zetu hapa JF wengine walitutangulia mbele ya haki;

Kwa kumkumbuka mmoja kwa Niaba ya wengine 'CHENTUTU' Mungu amlaze mahali

pema peponi AMINA.

Kuna matukio mengi yalitokea na kutuathiri kama nchi, kama Familia na kama mtu mmoja mmoja. Dah yapo yale mengine ambayo ni la kwako binafsi hata mume/mke/mchumba/rafiki hana msaada isipokuwa Mungu peke yake.

Kuna mengine ni ugonjwa, ajali, njaa na dhiki za hapa na pale. Mmmmh UKATA (Hela ilikuwa ngumu mmh sijui ni kwangu peke yangu?) Ila dah ukichenji elfu kumi saa 2 saa nane huna kitu :(

Lakini tumshukuru Mungu kwa kuwa pamoja na yote ameendelea kutuachia uhai, na uzima na bado tunaishi na kwa Neema yake atatuwezesha kuingia Mwaka 2012.

Yapo ya furaha pia....wengine wameoa, wameolewa, wamepata watoto, wamepata kazi, wamejenga nyumba, wamepata wachumba, wamenunua magari, wame..........................................mengi mengi tu tukitaja hayaishi. TUMSHUKURU Mungu kwa PAMOJA :)
:A S 465::A S 465::A S 465::A S 465:

Basi wapendwa katika jina la JF nawatakieni Miezi 12 ya FURAHA, wiki 52 za BARAKA, siku 366 za MAFANIKIO, masaa 8760 ya AFYA njema na dakika 525600 za AMANI. Ambazo kwa pamoja zinatengeneza mwaka 2012.

Mbarikiwe nyooooooooooooooooote.............
:A S 465::A S 465::A S 465::A S 465::A S 465:..............:A S 465:


LD
:A S-coffee:
:A S 465::A S 465:
 
Thankx and u too na tumshukuru Mungu kwa yote aliyotujalia mwaka huu na kumwomba atutangulie mwaka ujao
 
  • Thanks
Reactions: LD
Kwakweli umesema kila kitu!
Heri nyingi ziwe nawe pia.....
Limwaka witiri lishaisha hili
 
  • Thanks
Reactions: LD
Kwakweli umesema kila kitu!
Heri nyingi ziwe nawe pia.....
Limwaka witiri lishaisha hili

Kumbe huu ni witiri eeeh...umaokuja ni shufwa...mmmh hivi huu unaweza kuwa ni tasa pia?
 
Kila la Kheri LD, Na hopefully come 2012
tutagongana mara kwa mara jamvini.


BEST OF LUCK!


BTW If you don't mind naomba chai namimi....
 
  • Thanks
Reactions: LD
Kila la Kheri LD, Na hopefully come 2012
tutagongana mara kwa mara jamvini.


BEST OF LUCK!


BTW If you don't mind naomba chai namimi....

Chai Karibu Ashadii, kunywa hadi utosheke.

Tuombe uzima tu, huku tutapigana vikumbo sana.
 
Chai Karibu Ashadii, kunywa hadi utosheke.

Tuombe uzima tu, huku tutapigana vikumbo sana.


Ameen LD.... Vitafunwa nitapata Dear? Mie nahitaji na vitafunwa.... (if you don't mind) lol
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom