ITR
JF-Expert Member
- Sep 22, 2022
- 4,445
- 11,336
Mwanafalsafa wa JF bwana Teikon alishasema usimuonee huruma wala kumtetea masikini na mpumbavu maana unapoteza muda na huenda ukapoteza Uhuru na maisha yako bure na kusiwepo mabadiliko yoyote.
Sasa hii ndo maana halisi ya Watz, watz ni jamii isiyojua wanataka nini.
Kipindi cha nyuma kidogo watu walikuwa wanashinda kwenye mitandao ya kijamii wanalalamika kuwa wapinzani wamekaa kimya wakati nchi imejaa rushwa, mfumuko wa bei, uuzwaji wa bandari, mara wamelambishwa asali, sijui maneno gani mengi tu, lakini cha kushangaza leo hii Mbowe ameamua apaze sauti ya matatizo yanayowakumba watz na kuweka shinikizo la serikali iweze kuyatatua watu lakini hao hao waliokuwa wanalalamika wapinzani kukaa kimya ndo hao hao ambao wapo wanamtukana Mbowe na kumdhihaki, na wakati huo huo ndo wanashinda humu wanalalamika maisha magumu. Hivi waTz tuna akili kweli?
Leo Lissu anaamua kuikosoa Serikali juu ya ugumu wa maisha kwa waTz linatokea jitu moja linasema eti Lissu ni mpiga kelele na mganga njaa.
Hilo jitu linalomuita Lissu mganga njaa unakuta linaishi Mbagala rangi 3 limepanga chumba kimoja, watoto wa lenyewe wanasomea kayumba darasa kama banda la nguruwe na bado hilo darasa lina wanafunzi zaidi ya 150, sale za shule za watoto wa lenyewe zimejaa viraka, mlo wao wa kila siku ni mihogo ya ulojo na utumbo wa kuku.
Wakati huyo Lissu linalomuita mganga njaa mwenyewe anatembelea gari la milioni 400, kwake ndege ni kama daladala, yeye na watoto wake wanaishi kwenye majumba ya kifahari, watoto wake wanasoma Ulaya, wanakula wanachokitaka.
Lissu kipindi anakosoa uvunjwaji wa kiholela wa mikataba bila kufuata sheria kuliko kuwa kunafanywa na Magufuli watu walikuwa wanamshambulia kwa matusi na kila aina kashfa na dhihaka, lakini leo hii Serikali ipo inalipa fidia za upuuzi wa jiwe kwa mabilioni ya fedha za kodi za hao hao walio kuwa wanamkashifu Lissu.
Mimi siyo muumini wa sera za Chadema lakini itoshe kusema kuwa Watz ni jamii iliyojaa masikini na wapumbavu na mara zote umasikini ni laana, hivyo watz tulio wengi ni wajaa laana sasa ukiwatetea watu wenye laana na wewe unalaaniwa.