Kutokana na ukaribu huu mmewe alianza kuwa na wasiwasi namimi....
....all the way kwenda airpot na kuelekea nyumbani kwao tukawa tunawasiliana na huyu dada......mpaka nilipomaliza mida ya saa2 usiku.
....najisikia vibaya sana kwasababu mimi ndiyo chanzo....
Aaaaaaaah wapi!!!!!!! Huyu bwana tai mimi na yeye tu leo!!!!!!!!!1
Haiingii akilini UMPIGIE MKE WA MTU MIDA YA MUMEWE AFU UTEGEMEE MUMEWE AFURAHIE!!!!!!!! We mtu anaenda airport kwa mumewe njia nzima wewe tu hewani??????????
Nasema hiviiii! Mambo ya kazi ni muda wa kazi! Quality time ya mume ni quality time ya mume!!!!!! Vya Kaisari apewe kaisari na vya Mume apewe mume!!!!!!
Mvaa Tai
Ndoa huwa zinabeba mambo mengi, maelezo yako yangekuwa na msaada sana kama uhusiano wako na huyo dada ungekuwa zaidi ya kikazi, yaani mnaongea hata mambo ya kindoa, maana ungekuwa unatoa maelezo ukiwa na ufahamu wa maisha yao ya ndoa.
Pili, je una hakika pasi na shaka yeyote kuwa huyo dada hana hisia zozote na wewe?
Sikulaumu na pia sikutetei....kuna mambo ambayo tunapaswa kuyawekea tahadhari toka mwanzo hasa tunapokuwa tunawasiliana na wake/waume za watu ..Na wewe inaonyesha uli-mess up from the day go..mfano hata wewe ukijiweka kwenye nafasi ya huyo jamaa ..afu mtu unayemhisi ampigie simu mkeo ..asiongeee..lolz..nahsi utaona ambavyo ni ngumu sana kuaminika kirahisirahisi...
La kwanza jifunze namna bora ya kuishi na mke wa mtu hata kama mnafanya kazi pamoja (distancing)...La pili, kuhusu hili jambo kama una mke mshirikishe kwanza ili ajue kilichokutokea na hata likitokea la kutokea akupe support (manake unaweza kupoteza huku na kule)..Then, usifanye mawasiliano yeyote na huyu dada..hell no...naaamini kama hamkuwa na kitu chochote the truth will set you free..........................
mme wake mjinga,achana nae,huna kosa.Mwanaume unazira?!!!!
Huyu jamaa anampenda sana mkewe kiasi kwamba anakuwa na wivu wa kijinga, na tunaomfahamu huyu dada hapa ofisini hana tabia anazomzania labda huko mtaani kwao...mimi kinachoniuma ni huyu dada ikivunjika ndoa yake ilihali hana kwasababu yangu na akiwa hana uhusiano wowote na mimi
Wadau mwenzenu nipo kwenye wakati mgumu sana psychologicaly, kuna dada anataka kuachika kwasababu yangu ilihali hana kosa lolote....Ishu iko hivi Kuna dada(mke wa mtu) nipo naye karibu sana kikazi, siku asipokuwepo ofisini kuna baadhi ya kazi zake hunachia nimsaidie namimi nisipokuwepo ofisini naye hunipa ushirikiano wa hivyo kutokana na nature ya kazi zetu kufanana sana.
Kutokana na ukaribu huu mmewe alianza kuwa na wasiwasi namimi, kwasababu kuna siku nilimpigia simu mkewe akapokea yeye bila hata kujibu salamu yangu akaniuliza shida yangu ni nini? mimi nikamueleza kwamba shida yangu ni ya kikazi nataka kuongea na mkewe,..... kumbe alikuwa naye jirani akampatia nikaongea naye, yalikuwa ni masuala ya kikazi tu yaliyohitaji ufafnuzi wa sekunde chache tu alafu zilikuwa ni saa za kazi, ishu ni kwamba huyu dada na mmewe walikuwa likizo.
Hivi majuzi huyu dada aliwahi kidogo kutoka ofisini kwasababu alikuwa anawahi kumpokea mmewe Airport alikuwa ametokea nje ya nchi kusimamia matibabu ya ndugu yake, all the way kwenda airpot na kuelekea nyumbani kwao tukawa tunawasiliana na huyu dada kuhusiana na vikazi alivyoniachia pale kazini nimsaidie mpaka nilipomaliza mida ya saa2 usiku.
Nikiwa nyumbani mida ya saa4 usiku mwanangu wa miaka3 alichukua simu yangu ikiwa chumbani mimi nikiwa sebureni akawa anaichezea, kwa bahati mbaya akapiga simu kwenda kwa yule dada ikapokelewa na mmewe kila akiongea simu yangu ilikuwa kimya maana alikuwa anaichea mtoto na hakujua kama kapiga simu. baadaye kidogo akapiga yeye, mwanangu akaniletea simu nilipoipokea kumbe ni yule bwana anapiga akaniambia maneno machache tu "HAJAKWAMBIA KWAMBA NIMERUDI? KUANZIA SASA NIMEKUACHIA" nilipojaribu kutaka kujua zaidi nini kinaendelea akanikatia simu, kila nikipiga simu ikawa haipokelewi, kwenye mida ya saa6 usiku akapiga yule dada akiwa amepigwa na kahifadhiwa kwa jirani ndipo nilipogundua nini kilitokea, nimejaribu kumuomba huyu jamaa tuonane tuongee ameniambia nikae mbali naye.
Wadau naombeni ushauri nimsaidieje huyu dada ili kuokoa ndoa yake maana jana amerudi nyumbani kwake lakini mmewe hamsemeshi kitu chochote, akijaribu kumuelewesha anamuambia aje kwangu yeye hataki kuishi naye, najisikia vibaya sana kwasababu mimi ndiyo chanzo na naofia maisha yangu kujisogeza kwenda kunusuru hii ndoa.