Nauza samaki Sato fresh

Jan 13, 2023
92
99
Samaki aina ya sato ni moja kati ya kitoeo kinachopenda wa na idadi kubwa ya watu Zaidi ya aina nyingine zote za samaki wa maji chumvi na maji baridi kutokana na ladha yake ya kipekee na pia ni good source of protein. Sio hilo tu lakini pia ina kiwango kikubwa cha Omega 3 fatty ambacho ni muhimu sana kwenye mwili wa binadamu, inayosaidia kuboresha uzowe wa akili hasa kwa watoto

Changamoto kubwa kwa watu waishio maneo ya mjini imekuwa ni kupata Samaki fresh ambao ubora wao haujapungua kutokana na kuhifadhiwa kwenye fridge kwa muda mrefu, mfano samaki aina ya sato kutoka Ziwa Victoria hadi kuja kumfikia mtumiaji wa mwisho huchukua muda kati ya siku 3 hadi 7. Mazingira kama haya yanafanya mtumiaji wa mwisho asipate ile ladha halisi ya Samaki aliyotarajia kwa sababu ubora unakuwa umepungua baada ya kukaa kwenye fridge kwa muda mrefu.

Kama unajiuliza ni wapi sasa unaweza kupata Samaki sato fresh kabisa mwenye ubora sawa na yule aliyevuliwa direct kutoka ziwani hadi kukufikia mlaji wa mwisho kwa muda mfupi bila kupungua ubora. Basi mimi niko hapa kukuelezea na kukuelekeza wapi unaweza kupata huduma hii ya kupata kitoweo cha samaki aina ya sato akiwa fresh kabisa bila kupitia kwenye freezer ili upate kitu halisi, ule samaki akiwa na ladha yake halisi.

Nimeleta habari nzuri kwenu wote mnaopenda vyakula halisi ni kuwa Samaki wanapatikana Dar-es-salaam jirani kabisa na Bunju B, Samaki hawa ni wazuri kimuonekano hadi ladha yao, kama utaweza ku fika ofisini kwetu utapata samaki hai wakiwa wazima kabisa na kwa mliokombali au wanaotaka kuletewa hadi ulipo tunafanya delivery.

Bei ni affordable kabisa kilo moja (1kg) ni kati ya Tsh 9,000 – 10,000/= tu. Idada ya samaki kwa kilo moja inategemeana na matakwa ya mteja ila kwa kawaida kwenye kilo moja wanaingia kati ya samaki 4 – 6 kwa kilo moja (1kg/4-6 fish) Samaki mmoja anakuwa na uzito wa kati ya 250g – 150g hata wenye Zaidi ya hapo . ila wateja waliowengi wanapenda samaki wenye size ndogo kutokana na sababu za kibiashara.

Kwa mujibu wa wateja wetu wengi (wenye familia, wazabuni na wenye mahoteli) wanapenda samaki wa size iyo kwa sababu kwenye kilo moja wanaingia wengi lakini pia mtumiaji wa mwisho hupenda kula Samaki mzima peke yake, walio wengi hawapendi kula vipande (sehemu ya kichwa tu au mkia tu) lakini wakinunua mkumbwa let’s say mwenye 500g hadi 1kg + itawalazimu kukata vipande vipande kitu ambacho akiwapendezi watumiaji wengi, sio hilo tu lakini pia wataingia samaki wachache kwenye kilo.

Karibuni sana wote wenye uhitaji, tupo tayari kuwahudumia wasiliana nasi kupitia number za simu zifuatazo na uweke order yako sasa, mzigo utakufikia popote ulipo

What's app number
0758779170 au 0657823408.
 

Attachments

  • video_20210224_121606_540P.mp4
    4.1 MB
  • video_20210224_121606_540P.mp4
    4.1 MB
  • Screenshot_20210801_082639.jpg
    Screenshot_20210801_082639.jpg
    126.1 KB · Views: 17

Similar Discussions

Back
Top Bottom