Plot4Sale Nauza kiwanja Fukayose

Nauza kiwanja chenye ukubwa wa ekari 1 maeneo ya Fukayose.

Kama unahitaji ni PM

Aiseee umenikumbusha Fukayose unapita kile kidaraja cha bati Ruvu unaitafuta Kiwangwa kwenye mananasi kwenye Minara Minne kilimani.
 
Aiseee umenikumbusha Fukayose unapita kile kidaraja cha bati Ruvu unaitafuta Kiwangwa kwenye mananasi kwenye Minara Minne kilimani.
Hilo daraja ilikua njia ya zamani. Barabara mpya ya Msata imechepushwa na kuliacha hilo daraja kwa mbali.Kidomole, Makurunge na hata Fukayosi naona zinakua kwa kasi. Miaka michache iliopita eka moja hapo Fukayosi ilikua inauzwa laki 4 mpaka 5. Hivi sasa huwa naona matangazo eka moja ipo kwenye wastani wa milioni 1. Watu wengi (hasa jamii ya Wachaga) ninaowafahamu walinunua maeneo makubwa huko, eka 10, 20 hata 30. Wengine ndio hawa ambao naona sikuhizi.wanakata viwanja na kuuza. Sio vibaya ( kama hivi sasa pesa ya ziada ipo), unaweza kuwekeza kwenye ardhi maeneo hayo. Ardhi haijawahi kushuka thamani. Naamini, siku za mbeleni, bei za haya maeneo zitakuwa juu sana, pengine tunaweza kuja kujutia kupoteza fursa hizi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom