Naumia sana kuona vipaji vikubwa vinafia Simba kwa kusugua benchi tofauti na watani, sio sawa hata kidogo!

R-K-O

JF-Expert Member
Jun 27, 2023
482
2,151
John Bocco kwanini apate nafasi , halafu kina Chilunda wakose nafasi ? Kwaninii kina Onana wapate nafasi halafu kina Mohammed Mussa wakose ? Mbona Yanga anatoka Aziz Ki anaingia Zawadi Mauya ?

Hiki ndicho kinasababisha hata wachezaji kupigana misumari , hiki ndiyo kinasababisha wachezaji kuwa na makundi kambini , kwa style hii ni lazima kuwe na kundi la kina Duchu kina Kenedy , Kina Jimmyson mwanuke na Kundi la kina Chama , Miquissone , mwisho wa siku hawa ambao hawapati namba wanaonekana si chochote

Ni tofauti kwa watani, hata kina Crispin Ngushi wanavyopata namba na kina Mkude wanavyopisha wengine wacheze ni lazima waishi kwa ushirikiano na kuwa na juhudi ya mazoezi, hii ndiyo football ilivyo , Hakuna mchezaji anayesugua bench msimu mzima jamani (Jimmyson) na mchezaji huyo huyo aliyesugua Bench mkambakiza tena means kama mmembakiza mshaona anakitu why asipate nafasi ?

Acheni Mambo zenu , wapeni wengine nafasi waoneshe uwezo wao , Pengine mwisho wa siku baada ya kuona uwezo wao tutakuja kugundua Chilunda ni Bora kuliko Onana , Bocco anapataje nafasi mbele ya Mohammed Mussa ? Hapa ndipo naamini Uchawi upo

Kila siku Mohammed Hussein , Kapombe , watapataje Confidence za matches hawa kina Mwenda ?
Moses Phir kukosa nafasi tulipiga sana kelele hii ni kwamba wengi tunaamini ana uwezo , Haya vipi kuhusu Mohammed Musaa ? mbona hatuongei kwamba bwana mdogo hafai ?

Naumia sana kuona Vipaji vikubwa hivi vinafia Simba sc Wallah , Naumia mnooo ndiyo maana niliwaambia nitarekodi video hapa naandika lakini roho inaniuma sana BOCCO ANAANZA halafu Chilunda anakosa nafasiiiiii jamani kweli ?

Hao hao Mashabiki Wa simba wanasema Banda apewe muda , lakini ukiwaambia Chilunda apewe muda hawataki 😀

Naamini maneno ya Okwa Simba coach anapangiwa wachezaji wakucheza , wewe uliona wapi msimu mzima wachezaji ni wale wale tu ?
 
Mtoa Mada sijui kama unafatilia vzr soka letu ok ipo ivi chiruda alienda morroco a karud azam akupata nafasi mbele ya mbombo na dube azam wakamtema akakaa miez 6 bila team simba ndio kumchukua sasa wew kwa akili yako mtu miezi 6 ajacheza uje umpe nafasi kikosi cha kwanza unakili wew ivi mtu ufeli azam uje u win simba chiruda kusajiliwa n simba ni kamali tu simba ilicheza
 
Chama akitolewa mashibiki wanalia hata yeye pie hukasirishwa sana na swala hilo, ukitizama vzr Jana utagundua Aziz ki aliomba sub yeye mwenyw, na akatoka mwenye furaha.

Mfano Aucho ukimtoa hua Hana makasiriko kama wengine.

Mfano mzur muangalie sakho msimu ulopita akitolewa anapiga mateke viti. Kwa chama ndo usisime hapo gusa unase.
 
Na hiyo ndio itaendelea kukugharim mtani... Kocha wako muoga mnoo na anaplan moja tuu uwanjani na ndio maana anataka kikosi chake kiwe kile kile. Nimeona hata kwenye mechi ya Bonanza ambapo ndio mwalim anatakiwa kutest kikosi chake lakin yeye muoga.. sabu zenyewe anafanya tuu kwa sababu zipo ila kama wachezaji wangekuwa robot bas huyu angeend na kikosi cha wachezaji 11 tuu msim mzima.

Hii ni tofaut na Upande wa Yanga unaona kocha anajaribu kufanya rotation ya kikosi kila panapobid kulingana na plan ya Mechi.. hii ilikuwepo kwa Kocha Nabi na sasa Gamondi anafanya hivyohvyo na imekuwa na matokeo chanya maana karibia kikos kizima kinakuwa na mechi fitness tofaut na kutumia wachezaji walewale siku akikosekana mmoja mnaona kabisa kuwa timu ina pwaya
 
Mtoa Mada sijui kama unafatilia vzr soka letu ok ipo ivi chiruda alienda morroco a karud azam akupata nafasi mbele ya mbombo na dube azam wakamtema akakaa miez 6 bila team simba ndio kumchukua sasa wew kwa akili yako mtu miezi 6 ajacheza uje umpe nafasi kikosi cha kwanza unakili wew ivi mtu ufeli azam uje u win simba chiruda kusajiliwa n simba ni kamali tu simba ilicheza
Jaribu kumuelewa mleta mada, anachoongelea ni rotation ya kikosi wachezaji wawe wanapewa nafasi angalau hata Kwa DK 10 za mwisho..

Swali Miquissone amekaa nje bila kucheza Kwa muda gani?? Mbona game na Yanga alianza?? Kama hoja ni kukaa nje muda mrefu??
 
Mleta mada ni utopolo ila ana hoja ya msingi kwa faida ya timu yenu msikilizeni mchangie namna nzuri ya kulinda viwango vya wachezaji vinginevyo ni matumizi mabaya ya pesa kusajili wachezaji wa kukaa benchi.
 
Mtoa Mada sijui kama unafatilia vzr soka letu ok ipo ivi chiruda alienda morroco a karud azam akupata nafasi mbele ya mbombo na dube azam wakamtema akakaa miez 6 bila team simba ndio kumchukua sasa wew kwa akili yako mtu miezi 6 ajacheza uje umpe nafasi kikosi cha kwanza unakili wew ivi mtu ufeli azam uje u win simba chiruda kusajiliwa n simba ni kamali tu simba ilicheza
Hapana nakataa, mbona Mudathir kakaa miezi sita bila timu ila kaja yanga sc kakiwasha? Nakubaluana na mtoa mada
 
Back
Top Bottom