Hjalte
Member
- Oct 20, 2023
- 25
- 100
Ndugu zangu naombeni ushauri,
Nina tatizo la ajabu linalonitesa kwa muda wa miaka mitatu sasa la mwili wangu kuwa na muwasho mithili ya pilipili hasa ninapolala tu.Ni maumivu makali ambayo yanaanzia katikati ya tumbo na kifua nakusambaa sehemu mbalimbali za mwili,mapajani,mikononi na sasa yanasambaa hadi usoni na kunifanya kila siku nisilale usiku.
Muwasho si wa kujikuna wala kuvimba ila ni WA ndani kwa ndani,kazi yake ni kuvuruga mwili tu na usingizi kupotea.
Nachoshangaa ni kwamba tatizo hili halitokei nikiwa nimeketi wala nikiwa nimesimama,natembea au kufanya chochote,bali nikilala tu na hasa napoanza kupata usingizi huanza kwa ukali!relief yangu ya kwanza huwa ni kuamka na kukaa,ambapo huchukua dakika moja yanapotea.
Nimeshafanya vipimo vingi kwenye Hospitali kubwa hapa Dar ikiwemo Saifei vya damu na Endoscopy, kilichogundulika kilikuwa inflammation bowels pekee (tatizo kwenye utumbo) ambalo sidhani kama ndio chanzo cha muwasho huu kama mtu unavyohisi muwasho wa pilipili halafu si mtumiaji.
Wadau hebu tushare experience ili na Mimi nifurahie usingizi, tatizo hili huja na kuondoka.