Natamani Sana Rais Samia angemteua Dkt Shukuru Kawambwa nafasi yoyote ile serikalini au Chamani

Endelea kutulia chini mpaka akili yako utulie na ufikirie kama ni sawa walichokifanya wale jamaa juu ya udhalilishaji na kutweza utu wa wazee wetu. Vipi kama angekuwa ni baba yako ndio kadhalilishwa vile?

Tunachosema na ninachosema na kusisitiza ni kuwa ni lazima sheria kali na hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Kuacha watu wakitenda maovu na udhalilishaji wa kiwango kile pasipo kuchukuliwa hatua ni hatari sana kwa Taifa.maana inaweza jenga Taifa la watu na wananchi wasiotii na kuzingatia sheria wala kuogopa sheria na hivyo kujichukulia sheria mkononi kiholela.

Nasisitiza tena kuwa ni lazima wawajibishwe kikamilifu tena kikamilifu. Zingatia neno kikamilifu.
unasisitiza wachukuliwe hatua wewe kama nani?
unahisi Mzee hana watoto/familia?

mbona unaakili ndogo sana dogo?
roho yakisasi itakuponza
 
Yule Mhuni wanasema ni Diwani Mstaafu anatakiwa asitoke ndani kabisa angalau hata kwa wiki 2 au 3 alinikera sana kumdhalilisha mtu mzima namna ile,ni ujinga wa hali ya juu sana,mtu amekuwa Mbunge na Waziri mstaafu wewe Diwani mstaafu unapata wapi ujasiri wa kumdhalilisha vile.
Yule inatakiwa afundishwe na kushikishwa adabu kisawasawa mpaka akili zimkae sawa na kuacha mihemuko yake na uhuni uhuni.
 
unasisitiza wachukuliwe hatua wewe kama nani?
unahisi Mzee hana watoto/familia?

mbona unaakili ndogo sana dogo?
roho yakisasi itakuponza
Ni lazima wachukuliwe hatua kali za kisheria.kama Taifa hatuwezi kuacha watu wakawa wanajichukulia sheria mkononi bila kuwajibishwa .kila mtu akifanya hivyo haliwezi kuwa Taifa tena. Kama wewe unaunga mkono basi na wewe umekosa hekima na busara kwa kushabikia ujinga.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeangalia video inayomuonesha Mheshimiwa Shukuru Kawambwa waziri wa zamani na mstaafu katika serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi wa Rais Mstaafu Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete ,nimejikuta moyo wangu unaumia sana kwa namna alivyodhalilishwa na namna alivyotumia hekima,busara ya kiwango kilichovuka ubinadamu wa kawaida. Moyo wangu umesikitika sana,kuhuzunika sana,kupatwa na hasira sana pale nilipoona Mheshimiwa Kawambwa mtu anayelingana na Baba yangu kiumri akidhalilishwa kiasi kile.

Mheshimiwa Kawambwa ameonyesha kuwa yeye siyo binadamu wa kawaida ,ameonyesha utu uzima ni dawa.hekima aliyonayo na aliyoionesha siyo ya kujifunza kutoka darasani bali ni ya kuzaliwa nayo,ni ya kutoka nayo tumboni mwa mama yake,ni hekima aliyopewa na kujaliwa na Mungu wake. Kwa mtu aliyefikia ngazi ya uwaziri tena vipindi viwili ,mwenye kujuana na kufahamiana na viongozi mbalimbali wakumbwa wakumbwa ndani ya chama na serikali ni ngumu sana kumkuta akijishusha kwa kiwango kile na kuwa mtulivu katikati ya udhalilishaji na kutwezwa utu na heshima yake.

Natamani sana Rais Samia angemvuta binadamu huyu mwenye moyo wa kipekee na hekima za aina yake na utulivu wa kiwango cha juu kumsaidia kazi mahali popote pale ndani ya chama au serikalini,iwe ni kwenye mashirika ya umma,vyuoni au hata kwenye bodi mbalimbali. Huyu mtu ni hadhina .bado anazo nguvu za akili na mwili, bado anaishi maisha yenye hofu ya Mungu na yampendezayo Mungu. Mungu amjalie maisha marefu sana Mheshimiwa shukuru Kawambwa.

Naviomba vyombo vya dola viwachukulie hatua kali sana tena sana tena sanaaa kale kakikundi kote kalikofanya udhalilishaji kwa Mheshimiwa Kawambwa na yule mzee mstaafu..hatua kali za kisheria zichukuliwe zitakazo kuwa fundisho kwa wahuni wengine. Hatua ambazo wakitoka huko wakawe walimu kwa wengine.

Pia watu wale waamrishwe kuja hadharani kuomba radhi kwa magoti huku wakibubujikwa na machozi kwa udhalilishaji walioufanya kwa wazee wetu hawa wenye watoto,wajukuu,wakwe,ndugu,jamaa na marafiki. Vijana tuache ujinga na mihemuko ya kijinga,tuache kukurupuka na kujimwambafai .mtu amepata vijisenti kidogo anaanza kudhalilisha watu wengine .ndio maana wakati mwingine inakuwa ngumu sana kwetu vijana kuaminiwa katika mambo makubwa ,kwa kuwa tunatumia moyo na hisia kufanya maamuzi badala ya akili na mantiki.

Mheshimiwa Kawambwa ni darasa tosha na mfano halisia juu na maana ya mtu kuwa na hekima na busara.serikalini na ndani ya chama chetu cha Mapinduzi tunahitaji wazee wenye hekima na busara kiasi hiki,ambao wanajuwa waongee nini na wafanye nini na wakati gani,tunahitaji wazee wa aina hii ambao watatufunda vijana ndani ya chama kimaadili,tunahitaji wazee wa aina hiyo ya Kawambwa ambao hata katika hali ngumu na ya presha na ya udhalilishaji wanabaki watulivu na wenye stamini ya moyo na hisia na kumaliza mambo kwa utulivu.

Mheshimiwa Kawambwa ni mtu na nusu,Mungu aendelee kumbariki sana.natamani ningepata hata nafasi ya dakika tano kuchota na kupata busara zake.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. MAMA ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili kutokana na uchapa kazi wake uliotukuka na kukata kiu ya mamilioni ya watanzania.
Lucas
Jifunze dhana nzima ya kustaafu 😊

Labda apewe ukurugenzi wa bodi
 
kwanza tujue hizo tuhuma alizo tuhumiwa nazo nini?
tusikimbilie kudhalilishwa tukasahau alicho kitenda hadi kufikia mzee mzima kudhalilishwa.
 
Siyo lazima kumpa uwaziri kwa sababu ya kuonewa huruma!
Labda serikali ingefikiriwa kuwapa ulinzi wa kutosha watu wote waliofikia ngazi ya Uwaziri.
Akitaka kwenda ko kote apewe escort na polisi.
Hii itasaidia kuwalinda dhidi ya watu wabaya wenye nia ya kuwadhuru.
 
Imekuwa ngumu kutoa maoni kwenye ustahimilivu wa Dr Kawambwa kwakuwa sijafahamu chanzo kizima cha mzozo huu. Lakini kwa jinsi huyo bwana anayegombana naye anavyomsemesha inaonekana anamjua sana na kuna mambo wanafanya pamoja ambayo yamemfanya amchukulie kama mtu wa kawaida tu.

Shida yangu kubwa ilikuwa ni wapi Kawambwa, waziri mstaafu ametokana na watu wa aina hiyo?

Kuhusu kurekodiwa, hiyo ni kama saratani katika taifa letu kwasasa, unapaswa tu kuwa makini maana kila mwenye simu ni muandishi wa habari.
tafuta ile video clip ya pili ya Dr Kawambwa aliyotoa maelezo kuhusu chanzo cha huo mzozo
 
Ni lazima wachukuliwe hatua kali za kisheria.kama Taifa hatuwezi kuacha watu wakawa wanajichukulia sheria mkononi bila kuwajibishwa .kila mtu akifanya hivyo haliwezi kuwa Taifa tena. Kama wewe unaunga mkono basi na wewe umekosa hekima na busara kwa kushabikia ujinga.
rohombaya Yako unashindwa kuificha na unapiga domo humu upate madaraka pole kalime mkuu
 
Kwa ile video alivyodhalilishwa vile, bado tunasafari ndefu sana ya ethics za uongozi kwa vijana. Madaraka hata madogo tu huwa yanawalevya mno. Sasa yule kijana ndie angewahi kuwa waziri ingekuwaje?? Na kama inawezekana yule kijana atolewe udiwani kabisa kabisa. Ule ni udhalilishaji mkubwa sana. Hana hata chembe ya busara na hafai kuwa kiongozi popote. Na hongera kwa Mh Kawambwa kwa uvumilivu mkubwa vile. Na inawezekana kuna mengi amevumilia kabla ya tukio la juzi. God knows amevumilia mangapi!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeangalia video inayomuonesha Mheshimiwa Shukuru Kawambwa waziri wa zamani na mstaafu katika serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi wa Rais Mstaafu Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete ,nimejikuta moyo wangu unaumia sana kwa namna alivyodhalilishwa na namna alivyotumia hekima,busara ya kiwango kilichovuka ubinadamu wa kawaida. Moyo wangu umesikitika sana,kuhuzunika sana,kupatwa na hasira sana pale nilipoona Mheshimiwa Kawambwa mtu anayelingana na Baba yangu kiumri akidhalilishwa kiasi kile.

Mheshimiwa Kawambwa ameonyesha kuwa yeye siyo binadamu wa kawaida ,ameonyesha utu uzima ni dawa.hekima aliyonayo na aliyoionesha siyo ya kujifunza kutoka darasani bali ni ya kuzaliwa nayo,ni ya kutoka nayo tumboni mwa mama yake,ni hekima aliyopewa na kujaliwa na Mungu wake. Kwa mtu aliyefikia ngazi ya uwaziri tena vipindi viwili ,mwenye kujuana na kufahamiana na viongozi mbalimbali wakumbwa wakumbwa ndani ya chama na serikali ni ngumu sana kumkuta akijishusha kwa kiwango kile na kuwa mtulivu katikati ya udhalilishaji na kutwezwa utu na heshima yake.

Natamani sana Rais Samia angemvuta binadamu huyu mwenye moyo wa kipekee na hekima za aina yake na utulivu wa kiwango cha juu kumsaidia kazi mahali popote pale ndani ya chama au serikalini,iwe ni kwenye mashirika ya umma,vyuoni au hata kwenye bodi mbalimbali. Huyu mtu ni hadhina .bado anazo nguvu za akili na mwili, bado anaishi maisha yenye hofu ya Mungu na yampendezayo Mungu. Mungu amjalie maisha marefu sana Mheshimiwa shukuru Kawambwa.

Naviomba vyombo vya dola viwachukulie hatua kali sana tena sana tena sanaaa kale kakikundi kote kalikofanya udhalilishaji kwa Mheshimiwa Kawambwa na yule mzee mstaafu..hatua kali za kisheria zichukuliwe zitakazo kuwa fundisho kwa wahuni wengine. Hatua ambazo wakitoka huko wakawe walimu kwa wengine.

Pia watu wale waamrishwe kuja hadharani kuomba radhi kwa magoti huku wakibubujikwa na machozi kwa udhalilishaji walioufanya kwa wazee wetu hawa wenye watoto,wajukuu,wakwe,ndugu,jamaa na marafiki. Vijana tuache ujinga na mihemuko ya kijinga,tuache kukurupuka na kujimwambafai .mtu amepata vijisenti kidogo anaanza kudhalilisha watu wengine .ndio maana wakati mwingine inakuwa ngumu sana kwetu vijana kuaminiwa katika mambo makubwa ,kwa kuwa tunatumia moyo na hisia kufanya maamuzi badala ya akili na mantiki.

Mheshimiwa Kawambwa ni darasa tosha na mfano halisia juu na maana ya mtu kuwa na hekima na busara.serikalini na ndani ya chama chetu cha Mapinduzi tunahitaji wazee wenye hekima na busara kiasi hiki,ambao wanajuwa waongee nini na wafanye nini na wakati gani,tunahitaji wazee wa aina hii ambao watatufunda vijana ndani ya chama kimaadili,tunahitaji wazee wa aina hiyo ya Kawambwa ambao hata katika hali ngumu na ya presha na ya udhalilishaji wanabaki watulivu na wenye stamini ya moyo na hisia na kumaliza mambo kwa utulivu.

Mheshimiwa Kawambwa ni mtu na nusu,Mungu aendelee kumbariki sana.natamani ningepata hata nafasi ya dakika tano kuchota na kupata busara zake.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. MAMA ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili kutokana na uchapa kazi wake uliotukuka na kukata kiu ya mamilioni ya watanzania.
Nilidhani utaongelea achievement zake kwenye majukumu aliyowai kupewa kumbe unamuonea huruma. Ok inawezekana ombi lako likasikilizwa coz hapa kwetu hatuangalii mtu ameachieve nini na previous experience yake.
 
Back
Top Bottom