Natamani kumcheki lakini nashindwa kwa kuhofia kuonekana dhaifu kwake

20240409_151452.jpg
 
Hapo inategemeana scenario ya kupishana kwenu, na hilo litaamua kama hicho unachokifanya ni sahihi au ni upumbavu.

1. Kama yeye ndiye chanzo cha mgogoro kisha anataka wewe ndio uwajibike kuweka mambo sawa na anakushinikiza kwa ukimya wake, usithubutu kabisa kuwa wa kwanza kumtafuta na hata akikutafuta usiingie kingi moja kwa moja mpaka pale atakapokubali kulizungumzia kosa lake na akiri kuwa amejirekebisha. Ukijifanya kuendeshwa na hisia ukamtafuta wewe, basi tambua umekubali kuwa chini ya miguu yake kwa kipindi kirefu sana na lazima huko mbele yatakufa hayo mapenzi.

2. Kama wewe ndio uliyemkosea na mpaka sasa wewe ndio unasubiri kutafutwa ili ufukie makosa yako, tambua kuwa unafanya upumbavu kwasababu yeye pia ana haki ya kuumizwa na kile unachomkosea na kusubiri yeye aliyeumizwa ajishushe ni utoto usiokuwa na faida.

Kama wewe ndio ulikosea, mtafute kiume kisha umuombe msamaha kama mwanaume (Sio kwa kujilizaliza na kuomba huruma yake), muelezee nini kilitokea na kwamba kama mwanaume wake utajitahidi kuziondoa hizo dosari. Baada ya hapo kama atakusamehe endeleeni, kama ataendelea kununa na kutaka ujishushe zaidi, ujinyenyekeze na kulialia kwake kwa kuomba huruma, maana yake anatafuta kuku manipulate kupitia kosa lako. Kaa kimya, nawa mikono kisha ondoka kwenye hayo mahusiano.
 
Naomba kuuliza:

Mwanamke
na mwanaume mkikaushiana mfano kama huo, ni jinsia ipi huwa inaumia zaidi na hasa kwasababu gani?
 
Ni vizuri ukajuwa kosa lilikuwa la nani? kwa kuwa sasa hasira zimeisha unaweza kuangalia nani kakosa kati yetu au je alikosa lakini labda nili over react tu haikuwa na haja kuwa vile then Mwanamme(nahisi wewe) then sio aibu kuomba msamaha ndio uungwana lakini ikiwa wewe una uhakika yeye alikukosea na hataki hata kuomba msamaha hapo kuna shida inabidi ukaze sababu kama yeye kakosa na hataki kusema sorry huyo hana mpango na wewe.
 
Yapata wiki sasa tangu tupishane kiswahili na mwandani wangu

Kuna muda wazo la kumcheki linanijia lakini najikaza kisabuni kwa kuogopa ataniona niko so weak kwake.

Ooh my God why this happen to me. Lord give me strength to overcome this

Kilichobaki akili na moyo vinapingana, moyo unanishawishi nimcheki hata kwa kumtext lakini akili inakataa kabisa na kunambia uthithubutu.

Sasa wote tukiendekeza ego nani ataanza kumcheki mwenzake?

Daah nipo dilemma mwenzenu

Mapenzi mapenzi mapenzi

Ni maumivu tu badala ya furaha

Nakufa kijerumani na tai shingoni

Anyway kumpenda nampenda nikizidiwa nitamcheki
Approach ya kiume, kama kosa ni pa kwako mtafute mkae chini myajenge. Masuala ya kuviziana ni utoto sana
 
Kadri unavyokaa kimya ndo jinsi unavyomfanya azoee kuishi bila wewe na mwisho wa siku ka pumbavu ka moja kanavyozidi kuiteka akiri yake kwa vitu vidogo vidogo tu kama kumshauli, kumpa vocha au bando na sms za hap na pale.

Hivyo wewe jivike mabomu mtumie sms tu , mwambie nimekumic chizi wangu .
 
Kadri unavyokaa kimya ndo jinsi unavyomfanya azoee kuishi bila wewe na mwisho wa siku ka pumbavu ka moja kanavyozidi kuiteka akiri yake kwa vitu vidogo vidogo tu kama kumshauli, kumpa vocha au bando na sms za hap na pale.

Hivyo wewe jivike mabomu mtumie sms tu , mwambie nimekumic chizi wangu .
😅😅😅👍
 
Kama utaendekeza hisia, tegemea kuwa mtumwa wa mapenzi, kama angelikua anakuona wew ni wa thaman kwake angelishakutafta. Anakuona wa kazi gan ndo maana na yeye kabunda huko
 
Back
Top Bottom